Katika ulimwengu tumezungukwa na mambo mengi na kila wakati tunafanya uchaguzi. Katika moja ya chaguzi tufanyazo kwa kujua ama kutokujua ni aina ya maisha ya kuishi. Waweza taka ishi kitajiri ama kimaskini. Nasema kujua ama kutokujua maana yawezekana hakuna afanyaye maamuzi ya kutaka kuishi kimaskini lakini kutokana na njia atumiazo maishani kwa kutokujua hujikuta akiishi maisha ya kimaskini na sio kitajiri. Sasa kuna maana nyingi ya utajiri na umaskini, lakini leo nataka tuangalie katika njia tofauti tofauti.
Mtunzi wa mithali anaposema utajiri hufanya marafiki wengi anamaanisha ukiwa na vingi unavuta wengi. Hii ni katika nyanja tofauti kuanzia karama, uwezo wa kifedha, busara, upako na vingine vingi. Yakubidi kuwa makini maana kama unavuta wengi yamaanisha kati yao kuna wa kwako na wasio wako, nikimaanisha kuna mnao nia mamoja na msio nia mamoja. Umakini ni muhimu kwani lazima uweze kuwatambua na kujua jinsi ya kuwachuja. Ukiwa na vingi lazima uwe na busara ya Kimungu inayokukumbusha kutokuweka ulivyonavyo kuwa mungu wako. Lazima ukumbuke kuwa mnyenyekevu kwanza kwa Mungu wako alafu kwa watu walio wako hasa mnaonia mamoja.
Ukiwa na vichache sasa pia sio nuksi lakini pia sio baraka. Uchache huondoa mvuto na hivyo kuondoa watu. Uchache hukuondolea nguvu ya kutumika shambani mwa BWANA na hata kuwatumikia watu maana kila wakati unakuwa busy ukitafuta zaidi. Uchache pia hukuongezea lawama na manunguniko kwa Mungu wako na hivyo kukuondoa katika lengo lako la kuwepo duniani la kumtukuza na kumhubiri kwa wengine. Uchache hukuondolea furaha na pia hamu ya kuishi. Na ndio maana Suleiman akasema unibariki kwa kadri. Nisiwe na vingi nikakutukana na wala nisiwe na vichache nikakulaumu. Ni vyema kumuamini Mungu kuwa anatujua, na anajua kipimo chetu cha baraka ambacho kitatuweka kwake siku zote na kumshukuru na kumtukuza. Anatupandisha ngazi moja ya baraka baada ya nyingine, kwa imakini kabisa tusije tungeuka. Toka tumezaliwa Mungu hutupitisha kila ngazi ya ukuwaji kwa ufasaha, yaani ukizaliwa utaanza kutambaa muda ambao magoti yashapata nguvu ya kutosha kubeba mwili, utaanza kutembea muda ambao ushapata balance ya kutosha kuweza kusimama kwa miguu yako. Vivyo hivyo kuongea, kukimbia, kusoma,kupenda na kuanza maisha ya familia. Kila jambo huja ukiwa umeshakuwa tayari ukiwa ndani ya Mungu.
Anasema anatuwazia yaliyo mema na kwa hivyo tujiweke kwake naye atatuongoza salama katika baraka atupatiazo. Mungu hawezi kimbia kazi aliyoianza. Hawezi kukuacha. Nawatakia siku njema
No comments:
Post a Comment