(a)Jinsi ya kujiandaa na mahojiano (Interview)
Kuna hatua zifuatazo ambazo unatakiwa
kuzifuata kwenye mahojiano;
1.Kuelewa nini maana ya mahojiano
2. Jinsi ya kujiandaa na mahojiano
3.Jinsi ya kufanya vizuri katika mahojiano
4.Namna ya kufuatilia baada ya mahojiano
(a) Nini maana ya mahojiano
Mahojiano ni njia ya kukutana na kufahamiana
kati yako na mtu anayekufanyia mahojiano
yaani mwajiri na jopo lake la mahojiano. Pia ni
fursa ya kuonyesha hatua chanya kuelekea
kuendeleza taaluma yako. Uzoefu kazini na
elimu yako si kigezo pekee cha kuonyesha
kuwa wewe ni mtu sahihi kuajiriwa. Matokeo
mazuri ya mahojiano ni jinsi utakavyoweza
kujieleza.
Jee madhumuni ya mahojiano ni yapi?
Mahojiano ni njia ya mwajiri ya kuchagua
mwombaji ajira sahihi toka kwa waombaji
wenye sifa zinazolingana ambapo mchujo
utasababisha mshindi kupata kazi.
Yafuatayo hapa chini ni madhumuni ya
mahojiano;
1. Mwajiri anataka kujiua kama wewe unafaa
kwenye kampuni/taasisi yake. Anataka kujua
mambo matatu;
– Jee unaweza kuifanya kazi yake?
– Jee utaifanya kazi yake?
– Jee utamfaa?
2. Unataka kujieleza na kumshawishi mwajiri
kwamba unafaa kuajiriwa na unataka kujua
kama Kampuni itakufaa katika kuendeleza
taaluma yako.
3. Mahojiano ni fursa ya kuonyesha ujuzi na
uzoefu wako katika kazi unayoiomba.
Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuonyesha
katika mahojiano;
– Kujitambulisha
– Kuonyesha ujuzi wako kwa kujibu maswali
ya kitaaluma yanayohusiana na kazi uliyoomba,
yanaweza kuwa ya kujibu ana kwa ana au
mtihani wa maandishi.
– Eneo gani uko imara
– Una mapungufu gani
– Ni jinsi gani unaweza kuifanya kazi
– Unataka kufanya kazi kwenye kampuni kwa
muda gani?
– Nafasi hii inakufaa vipi?
– Kwa nini unataka kuhama huko ulikotoka na
kujiunga na kampuni mpya?
4. Mahojiano ni sehemu ya kuangalia kama
hiyo kampuni ni mahali sahihi kufanya kazi.
Mambo yafuatayo unapaswa kuyaangalia;
– Jee hii ni sehemu unayotaka kufanya kazi
– Jee utatoa mchango wako kikamilifu?
– Jee kuna fursa ya kujiendeleza na kupata
ujuzi mpya?
(b) Mambo ya kufanya kabla ya mahojiano.
Yafuatayo hapa chini ni mambo ambayo
unatakiwa kuyafanya kabla ya mahojiano.
– Kusanya habari kuhusu kampuni inayotaka
kukuajiri.
– Andaa mpango wa jinsi utakavyokwenda
kwenye mahojiano ikiwa ni pamoja kuwa na
orodha ya wadhamini ukitakiwa kutaja
wadhamini.
– Jiandae na mavazi utakayovaa siku ya
mahojiano. Vaa nguo safi ya heshima
iliyopigwa pasi, kiatu kilichongarishwa na kiwi
na soksi safi. Usivae jeans, nguo ya kubana
nguo za michezo, vitop au Tshirt nguo hizo
haziruhusiwi sehemu za kazi zinaweza
kukukosesha kazi na kuonekana mhuni.
– Jiandae na mahojiano hasa katika mambo
yafuatayo; Uzoefu wako kazini kama umewahi
kufanya kazi kama unayoomba,elimu yako,ujuzi
ulionao kama vile umekwenda chuoni ukasoma
na kupata cheti au Diploma na Digrii ya
uhasibu nk. Ufahamu wako kuhusu kampuni
unayotaka kuajiriwa nayo, mipango yako ya
kujiendeleza, mambo gani umeshafanya au
malengo yako binafsi uliyokuwa umejiwekea
umeyatimiza? Vitu gani vinakuvutia, mshara na
marupurupu. Jiandae kujibu maswali
yanayohusiana na taaluma yako kama
unaomba kazi ya uhasibu jiulize kazi za
mhasibu ni zipi pitia topic za (definition)
maana ya neon mhasibu, kazi zake ni zipi,
changamoto zinazoweza kukukabili kazini nk.
– Andaa majibu ya maswali yaliyoyatajwa
hapo juu.
– Fanya mazoezi ya jinsi ya kujibu maswali
kwa kujiangalia kwenye kioo au mtafute mtu
wa kukuuliza maswali na wewe ujibu.
– Fanya mazoezi jinsi ya kujitambulisha.
Mfano mimi ni Charles Paul ni kijana mwenye
umri wa miaka 21 nimesoma hadi kidato cha
sita, nina Diploma ya uhasibu toka chuo cha
Biashara CBE. Sasa hivi ninafanya kazi ya
Mhasibu msaidizi Kampuni ya ya Matunda
LTD. Nina uzoefu kazini wa miaka 5 kazini.
– Unatakiwa kujua ilipo ofisi utakapokwenda
kufanya mahojiano.
– Unatakiwa kuwahi kwenye mahojiano, ufike
angalau saa 1 au nusu saa kabla ya muda wa
mahojiano hali hii itaonyesha kuwa uko makini.
(c)Mambo ya kufanya wakati wa mahojiano
Kuingia kwenye mahojiano.
Wakati unaingia kwenye chumba cha
mahojiano jiamini, unyesha uchangamfu na
uwe mwenye furaha. Waangalie watu machoni
na uwasalimie kwa kuwapa mikono kama fursa
hiyo ipo. Hapa ndipo umuhimu wa kuwa msafi
unatakiwa, unapaswa kuwa na nguo safi za
heshima na zimepigwa pasi, umepiga mswaki,
nywele na ndevu zimekatwa na kuonekana u
nadhifu.
Mara nyingi mwajiri atajitambulisha kwako na
kwa wanajopo waliopo. Pia watakutaka
ujitambulishe. Kisha wataanza kukuliza
maswali.
Maswali ambayo unaweza kuulizwa ni kuhusu;
– Ufahamu wako kuhusu kampuni unayotaka
kuajiriwa nayo.
– Kwa nini unataka kujiunga na kampuni hiyo?
– Kwa nini unahama.
– Unafahamu nini kuhusu nafasi ya kazi
unayoiomba, kwa mfano kama unaomba kazi
ya uhasibu, utaulizwa nini maana ya mhasibu
kazi zake ni zipi. Unaeza kuulizwa kwa undani
ukapewa maswali ya mtihani wa maandishi
kuhusu topic Fulani kwa mfano bank
reconciliation, kusahihisha makosa kwenye
vitabu vya mahesabu nk.
– Unaweza kuulizwa kuhusu habari
zinazoendelea duniani au nchini (Current
affairs)
– Ni eneo gani uko imara
– Mapungufu yako ni yapi
– Ukipewa kazi unahitaji mshahara wa kiasi
gani.
– Ukipata kazi unaweza kuanza lini. Jibu ni
mara moja.
– Unaweza kupewa fursa ya kuuliza maswali.
Uliza maswali kutaka kujua zaidi kuhusu
ufafanuzi wa mambo muhimu na uelewa wako
kuhusu kampuni.
Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa
kufanya mahojiano.
– Unatakiwa kuwa msikilizaji mzuri
usimkatishe mtu kwa kuingilia swali kabla
hajamaliza kuuliza.
– Fuatilia kwa umakini kile kiachoulizwa.
– Uwe na utulivu.
– Ujiamini ila usijiamini kupita kiasi.
– Zungumza taratibu na kwa utulivu.
– Mwangalie muulizaji swali machoni
usiangalie pembeni au kuinama.
– Uwe huru.
(d)Mambo ya kufanya baada ya mahojiano
Baada ya mahohiano mtafahamishwa kuhusu
utaratibu mtakaofanyika kukufahamisha kama
umepata kazi au hujapata kazi. Si vyema
kumfuatilia mwajiri kwa simu au kwenda ofisini
kuulizia kuhusu majibu ya mahojiano, ni vyema
ukasubiri kufahamishwa kama umefanikiwa
kupata ajira au hapana.
Mwandishi wa makala hii ni Mkurugenzi wa
Kampuni ya CPM Business Consultants,
Mjasiriamail,Mshauri wa biashara na mtunzi
wa kitabu cha mbinu za biashara , Kupata
ushauri wa biashara, Ili Kupata mafunzo ya
ujasiriamali bila malipo kwa email bofya hapa
kujiunga; http://tinyurl.com/mshauriwabiashara
au Piga simu namba 0784394701

Categories:

Leave a Reply