**KUTOA SIO KWA TAJIRI TU BALI HATA MIMI NA WEWE TUNAPASWA KUTOA KILE
TULICHONACHO KIWE KIDOGO AU KIKUBWA KUWASAIDIA WALE WASIONACHO**
NAMBA 1: BILL GATES
Jamaa ameendelea kushikilia namba moja,nafasi ambayo aliipata mara ya
kwanza tangu 1994. Na mwaka huu kiasi cha utajiri wake kimeongezeka
kufikia dola bilioni 72 ukiachilia kiasi cha bilioni 28 alizotoa
kusaidia jamii. Hapo ndio tunaona nguvu ya kutoa.(The power of giving).
NAMBA 2: WARREN BUFFET
Mzee huyu utajiri wake umeongezeka kufikia dola za marekani bilioni 58
licha ya matatizo ya kiafya aliyonayo. Na ikikumbukwa mzee huyu alitoa
hisa zenye thamani kiasi cha bilioni 2 kwenda kusaidia jamii kupitia
mfuko wa Bill and Melinda Gates. Na kiasi ambacho ametoa kusaidia jamii
mpaka sasa ni dola bilioni 20. Na mwaka huu pekee kiwango cha ukuaji wa
hisa katika kampuni yake ni asilimia 34. (The power of giving)
NAMBA 3: LARRY ELLISON
Utajiri wake sasa unafikia dola bilioni 41 na ni mmiliki mwenza na CEO
wa Oracle corporation kampuni inayojishughulisha na utengenezaji wa
software za kompyuta.
Na jamaa ametoa kusaidia jamii kiasi cha dola za marekani milioni 445. (The power of Giving).
TUKITAZAMA HAO MATAJIRI NAMBA MOJA MPAKA TATU TUTAONA KUWA WANATABIA YA
KUSAIDIA JAMII KUPITIA KILE WANACHOKIPATA,HIYO NI MOJAWAPO YA NJIA
AMBAYO INAWAWEZESHA KUENDELEA KUKUA KWA UTAJIRI WAO.
MFANO BILL GATES AMEENDELEA KUWA JUU KWA MIAKA MINGI MFULULIZO NA HATA
UTAJIRI WAKE UNAENDELEA KUONGEZEKA KILA MWAKA LICHA YA KUENDELEA
KUSAIDIA JAMII. MFANO TAASISI YAKE YA BILL AND MELINDA GATES INAFADHILI
MIRADI MINGI SANA BARANI AFRIKA IKIWEMO TANZANIA.
**KUTOA SIO KWA TAJIRI TU BALI HATA MIMI NA WEWE TUNAPASWA KUTOA KILE
TULICHONACHO KIWE KIDOGO AU KIKUBWA KUWASAIDIA WALE WASIONACHO**
Categories: