Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya
Juu (HESLB), imefungua maombi ya mikopo
kwa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na
Taasisi za Elimu ya Juu zinazotambulika, kwa
masomo ya shahada mbalimbali kwa mwaka
wa masomo 2014/2015.
Akizungumza na waandishi wa habari katika
ofisi za HESLB jijini Dar es Salaam jana,
Mkurugenzi wa Habari, Elimu na Mawasiliano
wa HESLB, Cosmas Mwaisobwa, alisema
maombi ya mikopo yanafanyika kwa njia ya
mtandao (OLAS) yamefunguliwa kuanzia
Aprili 23 na yatafungwa rasmi Juni 30, 2014.
Mwaisobwa alisema kuwa Bodi inatarajia
kutoa mikopo kwa wanafunzi takriban 35,000
wa mwaka wa kwanza, watakaodahiliwa
kujiunga na masomo katika vyuo mbalimbali
vya elimu ya juu.

Categories:

Leave a Reply