Hapo zamani za kale kulikuwa na kijiji Fulani, kilikuwa kizuri sana kwa kuishi isipokuwa tatizo hakukuwa na majim ya uhakika mpaka mvua inaponyesha.

Hili kutatua tatizo hili wazee wakijiji waliitisha kikao na kuazimia kutafuta mzabuni atakayekuwa akikipatia maji kijiji kila siku.

Watu wawili walipatikana kufanya kazi hii na wazee wa kijiji waliamua kuwa zabuni hii wote wawili. wakiamini kuwa ushindani utaweka bei kuwa chini na uhakika wa maji kijijini.

Mmoja wa wa zabuni wale akiitwa Kibwana, haraka haraka alienda kununua ndoo mbili za chuma na kuanza mara moja kwenda na kurudi kuchota maji, kutoka katika ziwa lililokuwa mbali kidogo na kijiji na kusambaza kijijini, akaanza kutengeneza pesa chapchap, akitaabika alfajiri ata jioni akituta ndoo za maji.

Alikuwa akituta na kujaza katika tanki kubwa ambalo kijiji kilijenga kwa ajili hiyo, siku zote aliamka kabla ya wanakijiji wote ili kuhakikisha kuwa maji yanakuwepo kabla hawajaamka, ilikuwa kazi ngumu, lakini alikuwa na furaha kwa sababu alikuwa akiingiza kipato kwa biashara hii.

Yule mzabuni wa pili akiitwa Ben alipotea kwa kitambo kidogo, hakuonekana miezi kadhaa, hii ilimfanya Kitwana kuwa na furaha sana maana hakuwa na ushindani, alikuwa akipata pesa zote za kijiji kwa Wakati huo.

Badala ya kununua ndoo mbili hili kushindana na Kibwana, Ben alikaa chini na kuandika mpango wa biashara, akatengeneza Shirika, akaajiri msimamizi wa mradi, akatengeneza timu ya kazi, alirudi miezi sita baadaye akiwa na watu wa ujenzi, ndani ya mwaka Mmoja wajenzi wale walijenga mtandao mkubwa wa mabomba uliounganisha ziwa na kijiji.

Siku ya ufunguzi Ben akijua ya kuwa watu walikuwa wakilalamikia uchafu wa maji ya Kibwana, alitangaza kuwa maji yake ni masafi kuliko ya Kibwana, pia ya kuwa anaweza kusambaza maji kijijini masaa 24, siku saba za wiki, Wakati Kibwana anaweza kuleta siku za kazi tu, na zaidi akatangaza kushusha bei kwa asilimia 75 ya ile anayotoza Kibwana, watu walifurahi sana, woote wakawa wanateka maji kwa Ben.

Kibwana kuona vile aliamua naye kushusha bei kwa asilimia 75 pia, akanunua ndoo mbili zaidi, akaongezea na mifuniko katika ndoo zake, akaanza kututa ndoo nne kwa mpigo, ili kuwahudumia vyema wanakijiji aliamua kuwaajiri wanae wawili wa kiume ili wasaidiane naye, ilibidi pia kufanya kazi mpaka usiku na siku za mwisho wa wiki, ilipofika muda wa wanae kwenda vyuoni, aliwaasa wakimaliza warudi haraka nyumbani kwani hii itakuwa biashara yao siku za usoni.

Kwa sababu hii ama ile watoto wale hawakurudi baada ya kumaliza masomo, mwishoni Kibwana aliajiri watu kufanya naye kazi, lakini akaishia kupata matatizo na umoja wa wafanyakazi, Umoja ulimtaka kuwapa maslahi mazuri, kubeba ndoo moja kwa safari na kuwapa marurupu zaidi.

Ben, kwa upande wake alitambua kuwa ikiwa kijiji hiki kinahitaji maji bila shaka na vijiji vingine vinamahitaji pia, hivyo akaandika mchanganuo wa biashara yake ya maji safi, salama, uhakika na gharama nafuu kwa vijiji vyoote duniani, anaingiza pesa ndogo tu kwa kila ndoo lakini anauwezo wa kuuza mabilioni ya ndoo kila siku, haijalishi kama amefanya kazi au la, mamilioni ya watu watapata maji na mabilioni yataingia katika akaunti yake ya benki, Ben amatengeneza bomba la kumletea pesa yeye mwenyewe na pia kuwaletea wanakijiji maji.

Ben aliishi kwa furaha zaidi na Kibwana alifanya kazi ngumu maisha yake yoote na kuishia kuwa na matatizo ya pesa milele,
Swali je, Ungali watuta ndoo za maji au wajenga mtandao wa mabomba?
Katika kazi ama biashara uifanyayo, wajenga bomba au watunta ndoo za maji??
Jeni Biashara au kazi gani chini ya jua inaweza kukufanya ujenge Bomba, bomba la kipato? yaani itakayokuwezasha kuingiza pesa masaa 24, siku saba za wiki, pasipo kuangalia ikiwa umefanya kazi au la?

Nitwangie 0716927070, au ni-email: brwebangira@gmail.com kwa swali lolote.

Nakutakia mafanikio katika kila ufanyalo.

Categories:

Leave a Reply