HII ILITOKEA NCHINI KONGO
Kuna mwanaume alikuwa masikini wa kutupwa.
Alikuwa akiishi na mke wake na mtoto wake
mmoja. Maisha yalimpiga kwa kipindi kirefu,
alipoona sasa hakuwa na kitu cha kufanya huku
akiwa hayupo radhi kujiona anakufa na familia
yake, hapo ndipo alipoamua kusafiri kuelekea
migodini ili mradi apate japo dhahabu, auze
apate fedha.
Akaiaga familia yake, wakati huo mtoto wake
alikuwa na miaka miwili tu. Akaondoka zake
huku moyoni akiwa na hasira ya kupata
dhahabu, aiuze na hatimae awe tajiri.
Aliendelea kusafiri, mawazo yake yaliifikiria
zaidi familia yake, baada ya safari ya wiki
nzima, akafika katika mgodi huo na akaanza
kazi rasmi.
Mwaka wa kwanza ukakatika, hakupata kitu
chochote kile, mwaka wa pili ukakatika,
hakupata kitu. Hakuwa akiwasiliana na familia
yake ambayo aliiacha katika maisha ya shida.
Mwaka wa tatu ukakatika, wa nne, wa tano, wa
sita mpaka wa saba. Bado hakuwa amepata
kitu chochote kile.
Baada ya miezi kadhaa huku ikiwa imebakia
miezi michache mwaka wa nane uingie huku
akiwa mgodini, akafanikiwa kupata dhahabu
moja kubwa kama kiganja chake, akafurahi mno
kwa kuona kwamba sasa alikuwa ameuaga
umasikini.
Kesho yake, akavalia koti kubwa, akaiweka
dhahabu ile kwenye mfuko wa koti na kuelekea
ziwani kupanda boti ya kurudi nyumbani. Ndani
ya boti kulikuwa na watu zaidi ya mia moja,
wengi walikuwa watalii kutoka nchini Marekani.
Walipofika katikati ya ziwa, upepo mkali
ukaipiga boti ile, ikaanza kuyumba,
ikapasukapasuka na hatimae maji kuanza
kuingia, watu wakaanza kupiga kelele, boti
ikaanza kuzama.
Kwa sababu jamaa alikuwa akijua sana
kuogelea, hakuogopa, akaanza kupiga mbizi
huku dhahabu yake nzito ikiwa kwenye mfuko
wa koti lake.
Akiwa anaendelea kupiga mbizi huku watu wote
hadi wale watalii kuwa wamekufa, jamaa
akaanza kusikia sauti ya mtoto ikilia, binti wa
miaka kumi na mbili, mzungu alikuwa
akitapatapa.
Jamaa akaona haiwezekani, asingeweza
kumuacha msichana yule afe, akaanza
kumfuata kwa lengo la kumuokoa, alipomfikia,
akamshika mkono na kuanza kuogelea naye, ila
baada ya dakika tano, kutokana na uzito ule wa
dhahabu na mtoto, alitakiwa achie kitu kimoja.
Yaani kama iliwezekana, amuachie mtoto afe ili
aokoe dhahabu yake aliyoitafuta kwa miaka
saba au aiachie dhahabu yake na kumuokoa
mtoto yule.
Huo ulikuwa mtihani mgumu, aliifikiria familia
yake masikini ambayo ilimsubiri kwa miaka
saba ili aweze kupata dhahabu, aiuze na apate
utajiri. Leo hii, dhahabu ilipatikana na utajiri
ulikuwa ukinukia, lakini mbaya zaidi, alitakiwa
kuiachia dhahabu hiyo, hakika ulikuwa mtihani
mkubwa kwake.
Baada ya dakika zaidi ya tano kujifikiria, jamaa
akaona haina jinsi, akaiachia dhahabu na
kumshikilia mtoto yule.
Moyoni ilimuuma mno lakini hakuwa na jinsi,
kwa sababu alijitolea kumuokoa mtoto yule,
alifanya hivyo. Akaogelea naye mpaka boti
nyingine ilipofika na kuwaokoa.
Boti ilipokaribia na nchi kavu, wakatoka na
jamaa kuelekea nyumbani kwake huku
akimuaga binti yule ambaye alifiwa na wazazi
wake na kurudi Marekani.
Alipofika nyumbani, mke wake alikuwa na faraja
kubwa, akampokea na kumuuliza kama
iliwezekana kuipata dhahabu, jamaa akamjibu
kwamba iliwezekana lakini kutokana na ajali ya
boti, aliamua kuiacha ziwani na kumuokoa
mtoto wa kizungu.
Mke wake akaanza kulalamika kwa kumuona
jamaa kuwa mpumbavu kwa kile alichokifanya.
Akawatangazia majirani juu ya ujinga alioufanya
mume wake, watu wakamshangaa.
Mke hakuishia hapo, alichokifanya, akachukua
kila kilicho chake na kuondoka nyumbani hapo
na mtoto wake, hakutaka kuishi tena na mume
wake.
Maisha ambayo aliyaacha ndiyo yakaanza tena,
umasikini ukamjaa, kila siku akawa mtu wa
kulia tu lakini kamwe hakujilaumu. Mwili wake
ukaanza kudhoofika, vipele vikaanza kumtoka,
njaa ikamkamata na katika kipindi hicho
hakukuwa na mtu aliyemsaidia kwa kuwa
alifanya ujinga mmoja mkubwa wa kupoteza
dhahabu kwa mtu asiyemfahamu.
Baada ya miaka kumi kukaa katika hali hiyo,
siku moja akapata ugeni, alikuwa msichana
mrembo wa kizungu ambaye alikuja
kumtembelea baada ya kumtafuta kwa kipindi
kirefu. Msichana yule alipomuona,
akajitambulisha kwamba alikuwa ndiye yule
binti aliyemuokoa miaka ile ya nyuma, sasa hivi
alikuwa tajiri mkubwa nchini Marekani baada ya
kuziendesha biashara za wazazi wake na
kumilika kampuni zaidi ya tano.
Akamshukuru kwa yote aliyomfanyia na kila
siku alitamani kuonana naye tena. Jamaa
akafurahi mno na kwa sababu alikuwa katika
maisha ya kimasikini, msichana yule hakumtaka
kuishi Kongo tena, akamchukua na kuelekea
Nchini Marekani kuishi naye.
Mpaka leo hii ninapoandika maneno haya,
jamaa ana hisa yake katika Timu ya mpira wa
kikapu ya Heat, yeye ndiye anayeshughulikia
jengo la World Trade Center ambalo lililipuliwa
baada ya kugongwa na ndege, kampuni yake ya
Omutimba Company Limited ambayo ni
maarufu kwa ujenzi wa majengo ndiyo
iliyofanya kazi kubwa ya kulisimisha tena jengo
hilo japo kazi haikukamilika kama ilivyokuwa
mwanzo.
Pia, yeye ndiye mtu aliyetaka kuinunua mtandao
wa WhatsApp lakini akaja kupigwa bao na huyu
jamaa wa Facebook.
Kwa sasa hivi, ana miaka 56 lakini akakula bata
baada ya kufanya kitu kimoja kilichomgombani
sha na familia yake, majirani zake na kumpa
umasikini mkubwa zaidi.
UMEJIFUNZA NINI?
Kuwa na stori hii moyoni mwako, kuna siku
inaweza kukusaidia katika maisha yako.
Nyemo Chilongani
Categories: