KWA MUJIBU WA FORBES MPAKA TAREHE 23 AUGUST LIST ILIKUWA KAMA IFUATAVYO

NAMBA 1: BILL GATES
Jamaa ameendelea kushikilia namba moja,nafasi ambayo aliipata mara ya kwanza tangu 1994. Na mwaka huu kiasi cha utajiri wake kimeongezeka kufikia dola bilioni 72 ukiachilia kiasi cha bilioni 28 alizotoa kusaidia jamii. Hapo ndio tunaona nguvu ya kutoa.(The power of giving).

NAMBA 2: WARREN BUFFET
Mzee huyu utajiri wake umeongezeka kufikia dola za marekani bilioni 58 licha ya matatizo ya kiafya aliyonayo. Na ikikumbukwa mzee huyu alitoa hisa zenye thamani kiasi cha bilioni 2 kwenda kusaidia jamii kupitia mfuko wa Bill and Melinda Gates. Na kiasi ambacho ametoa kusaidia jamii mpaka sasa ni dola bilioni 20. Na mwaka huu pekee kiwango cha ukuaji wa hisa katika kampuni yake ni asilimia 34. (The power of giving)

NAMBA 3: LARRY ELLISON
Utajiri wake sasa unafikia dola bilioni 41 na ni mmiliki mwenza na CEO wa Oracle corporation kampuni inayojishughulisha na utengenezaji wa software za kompyuta.
Na jamaa ametoa kusaidia jamii kiasi cha dola za marekani milioni 445. (The power of Giving).

TUKITAZAMA HAO MATAJIRI NAMBA MOJA MPAKA TATU TUTAONA KUWA WANATABIA YA KUSAIDIA JAMII KUPITIA KILE WANACHOKIPATA,HIYO NI MOJAWAPO YA NJIA AMBAYO INAWAWEZESHA KUENDELEA KUKUA KWA UTAJIRI WAO.
MFANO BILL GATES AMEENDELEA KUWA JUU KWA MIAKA MINGI MFULULIZO NA HATA UTAJIRI WAKE UNAENDELEA KUONGEZEKA KILA MWAKA LICHA YA KUENDELEA KUSAIDIA JAMII. MFANO TAASISI YAKE YA BILL AND MELINDA GATES INAFADHILI MIRADI MINGI SANA BARANI AFRIKA IKIWEMO TANZANIA.

**KUTOA SIO KWA TAJIRI TU BALI HATA MIMI NA WEWE TUNAPASWA KUTOA KILE TULICHONACHO KIWE KIDOGO AU KIKUBWA KUWASAIDIA WALE WASIONACHO**

Categories:

Leave a Reply