Wadau,
Nawasalim...

Kutokana na mjadala mrefu unaoondelea kwa siku kadhaa kwenye jukwaa hili, kuhusu apartments kutokuhitajika mikoani, nimeona niweke chapisho hili la utofauti kati ya sales na marketing, ili kuepuka aina ya upotoshaji uliopo kwenye chapisho la mleta mada aliyesema kuna mikoa Tanzania apartments hazihitajiki. Chapisho lenyewe linapatikana hapa YES Tunahitaji Apartments Tanzania Lakini si kila Mkoa

Wadau,
Marketing inachokifanya ni kuangalia kwenye kundi kubwa la watu/jamii ni product/service gani wanahitaji, lakini marketing haiishii hapo, inaenda mbali zaidi na kuangalia kuna potential kiasi gani ya kuwafanya consumers waikubali product husika na kuipa thamani inayoendana na matakwa ya entrepreneur. Mtaalam wa marketing then anatengeneza strategy ya jinsi ya kuinfluence consumers of the product.


Mfano: wataalam wa marketing wamefanikiwa kufanya tabia ya kuvuta sigara ionekane kama sign of freedom and success, hii inasababisha vijana wengi kuvuta sigara not because they need it but because kuvuta sigara kwao inawapa feeling kwamba wamekuwa wakubwa na wanaweza kujiamulia mambo yao. Hivyohivyo kwa beer. Vijana wengi wameanza kunywa bia chuo mainly because ndio wameanza kuwa na some income and freedom. Utawasikia wakisema "bia yangu inashuka taratibu" wanataka kuonyesha kwamba kuwa na bia kwao ni sign ya kuwa wako fine. Ni symbol ya mafanikio. Hiyo haijatokea tu hivihivi, imekuwa influenced by marketing ya bia.
That is what marketing does.

Sales on the other hand iko limited. Mtu wa sales anatakiwa kuuza product ambayo tayari imeshatengenezwa. Mtu wa sales hawezi kubadilisha product characteristics, kwa sababu inakuwa imeshatengenezwa kutokana na ushauri wa mtaalam wa marketing. Mtu wa sales anachokifanya ni kudefine specific group of potential customers na kubuni mbinu ya kuwafanya wainunue product hiyo.

Kwa lugha nyingine ni kwamba mtu wa marketing anavuta kundi kubwa la watu towards the product halafu mtu wa sales anaipush hiyo product kwa wateja watakaokuwepo kwenye kundi hilo.

Kwahiyo hapa unaona kwamba mtu wa marketing anaivuta jamii yote halafu mtu wa sales sasa anachambua katika wale waliovutwa ni wepi wenye uwezo wa kuinunua product husika and then anatengeneza strategy ya kudeal nao one-on-one.

Kwa mfano, watu wa marketing wametufanya watu tuipende na kuithamini Mercedes Benz, wamefanya kazi hiyo kwa uhodari mkubwa, as a result watu wengi duniani wanapenda Mercedes. Mtu wa sales wa Mercedes though hawezi kutarget watu wote duniani. Hawezi kutarget kuwauzia Mercedes wakimbizi walio kwenye refugees camp Somalia kwa mfano (ingawa nao wanaweza kuwa wanaipenda Mercedes). Atawatarget mabalozi, ma CEO,mawaziri, wafanyabiashara wakubwa na wengine anaoona wanaweza kuinunua Mercedes Benz.

It is important to note kwamba marketing na sales vyote lengo lake ni kuongeza revenue lakini sales ndio ultimate goal of marketing.

Turudi kwenye mfano wa apartments. Mtu wa marketing anapaswa kuingia field na kusoma mahitaji ya watu na kubuni marketing strategy ya kuwafanya wawe tayari kununua apartments.
Akishafanya hivyo successfully entrepreneur anajenga apartments na kumpa mtu wa sales uziuze.

Mtu asiyekuwa na utaalam wa marketing hana authority ya kusema kuwa product/apartments hazihitajiki.


Nafasi ya mtu wa sales inakuja baada ya kuwa product imeshakuwa designed, then anaweza kusema this particular type of apartments sitaweza kuiuza.


Taarifa yake hiyo (ya kushindwa kuuza apartments) itakuwa valid kwa aina hiyo ya apartments in that particular location na si kwa apartments zote mkoa mzima, kwa sababu kwenye real estate nyumba hiyo hiyo ikiwa just 1 km away mahitaji yake yanaweza kubadilika largely. Nyumba ambayo broker anapata shida kuiuza kwa bei fulani msasani akivuka bonde tu na kuikuta nyumba inayofanana na hiyohiyo Oysterbay anaweza kuiuza kwa bei kubwa mara tatu zaidi. Kwahiyo aliyeshindwa kuuza nyumba msasani asiseme kwamba nyumba za namna hiyo Dar es Salaam hazihitajiki!

Vilevile sales ni kipaji kama zilivyo fani nyingine. Product atakayoshindwa kuiuza broker mmoja, asishangae mwenzake akaiuza kwa mafanikio makubwa. Kwahiyo kushindwa kwake kuuza kunatoa fursa kwa broker mwingine kupewa tenda na kujitangaza.

Wito: Ndugu zangu watanzania. Hii ni dunia ya ushindani. Katika dunia ya ushindani kauli na attitude za kukata tamaa na kulalamika hazina manufaa. Mara nyingi huwa kuna options nyingi sana hazijajaribiwa kabla mtu hajasema jambo fulani haliwezekani.

Vijana tusikubali kusema neno HAIWEZEKANI kirahisi rahisi. Tena inafaa neno HAIWEZEKANI tulisahau kabisa.

Lazima tuwe wabunifu. Tuwe tayari kujifunza mambo mapya na kujaribu njia tofauti tofauti mpaka tufanikiwe. Mwisho wa kujaribu jambo unalolitaka iwe siku unayoenda kaburini, if you are still alive always try to figure out the other way you can make it happen.

Nawatakia Maadhimisho Mema ya Sikukuu ya Iddi...

by friend of mine komandoo jf member

Categories:

Leave a Reply