Watu wengi wamekuwa na shida ya kupata ama kutambua ni biashara gani inayofaa kufanya kulingana na kiasi cha pesa wanachokipata, na hili limekuwa janga kubwa idadi kubwa ya wafanyabiashara hujikuta wakianzisha biashara zisizokuwa katika mzinguko wao wa maisha ya kawaida hivyo hujikuta wanafeli na kushindwa.



Wazo la biashara sio kitu cha kumuomba mwenzako ili ufanikiwe, unaweza kumuomba mwenzako
aliboreshe lakini sio akupe wewe wazo kwa sababu kila mtu huwa ananjia zake za kukamilisha ndoto zake, hivyo mipango yake na yako inatofautiana sana. wazo la biashara yako unalo mwenyewe kichwani kwako ila unalipuuzia aidha kwa kuliona ni kubwa au hujiamini kulikamilisha.


Baadhi ya mambo ambayo unayotakiwa kuyafatilia unapotaka kuanza biashara au unapotaka kutafuta wazo la biashara zingatia sana vitu vifuatavyo


1. Elewa maana ya Biashara
Biashara ni mchezo wa kubadilishana bidhaa kwa mtindo wa pesa au kitu chochote kutoka
kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine kukiwa na thamani ya hicho kitu ndani yake.


Lakini biashara pia husimamiwa na makubaliano, wazo la muendelezo, na uwezo wa ukinzani hivyo
biashara yako inahitaji sana makubaliano kati yako wewe mwenye biashara na biashara yenyewe, na
pia inahitaji muendelezo baada ya makubaliano hayo, pia biashara yako inahitaji sana uwezo wako wa ukinzani ili kuipatia nafasi katika soko na aina ya kipengele unachohudumia.


2. Itambue Branding
Branding kwa maana moja tunaweza kusema ni muonekano wa biashara yako, branding ni muonekano wako Kuhusu biashara yako na jinsi gani biashara yako inajitofautisha na washindani wenzako.




Pamoja na hiyo maana pia brand inamisingi yake na aina zake ambapo ndani ya aina za Brand utapata uwezo wa kujitambua mwenyewe kutambua ni jinsi gani biashara yako inatakiwa iwe na pia

ni vitu gani vinafaa kwa biashara na vipi havifai kutokana na uelewa utakao kuwa nao tayari utakuwa na uwezo wa kuchagua na kuona ni biashara gani inayokufaa kwa kipengele chako. aina hizo za branding ni Brand ya mtu, bidhaa, mfumo na alama ambapo vitu hivyi huenda pamoja ili biashara ikue na kuleta mafanikio.






3. Tumia makosa ya wengine kupata nafasi
Baada ya kuelewa maana ya biashara na branding utakuwa na uwezo mzuri wa kupata wazo zuri la
biashara kutokana na kuangalia ni sehemu gani unayotaka kuanzisha hiyo biashara hivyo hizo elimu mbili zitakupa mwangaza wa kutambua ufanye nini, na kunamakosa gani ambayo ndio wewe utayarekebisha.


4. Fanya brand yako mwenyewe (personal Branding)

Ndani ya aina za Branding kuna aina nne za branding ambazo zote hutumika pamoja lakini kwa
kuanzia unaweza kuanza na brand ya mtu kwa sababu hiyo ndio inayotengeneza biashara yako
hata kabla haijaanza kufanya kazi .

Elisha Chuma: Jinsi ya kupata wazo la biashara

Categories:

Leave a Reply