IMEANDIKWA NA MAKIRITA AMANI WA AMKA MTANZANIA
Wengi tunajua matajiri wakubwa wa Tanzania, wa Afrika
na hata wa dunia kwa ujumla. Na baadhi yetu tunajua thamani ya utajiri
wanaomiliki matajiri hawa, japo yule wa kwanza. Huenda umeshawahi
kuingia kwenye ubisha na wenzako kuhusu nani tajiri namba moja ama
kiwango cha utajiri matajiri wakubwa wanachomiliki.
Ni vizuri sana kujua takwimu hizi za watu matajiri, ila je umewahi
kuziandika takwimu za utajiri wako? Ama unafikiri huna utajiri unaoweza
kuuandikia takwimu? Ama unafikiri kwakuwa huna fedha walizonazo matajiri
wakubwa basi wewe huna utajiri wowote unaomiliki?
Kama unafikiri wewe sio tajiri basi unakosea, kama unaweza kusoma hapa basi wewe unamiliki utajiri mkubwa sana.
Hebu kaa chini na utathimini thamani ya vitu hivi ambavyo umepewa bure kabisa.
Maisha, unaweza kusoma hapa kwa sababu unaishi, na una afya njema. Je
akitokea mtu mwenye fedha nyingi akakuambia umuuzie moyo wako utamwambia
akupe shilingi ngapi?(soma; thamani ya uhai wako). Maisha yako na afya yako ni utajiri mkubwa sana kwako.
Viungo vya mwili ulivyonavyo, akili timamu, macho, masikio, mikono na
miguu. Ni gharama kiasi gani unaweza kumtoza mtu atakaetaka kununua
baadhi ya viungo hivyo kutoka kwako? Kama una viungo hivyo na vinafanya
kazi vizuri basi wewe ni tajiri mkubwa sana. Hata kama kuna vyote ila
kuwa tu una akili timamu ni utajiri tosha. Kuna watu wengi ambao hawana
baadhi ya viungo kama mikono, miguu, ama macho ila wamefanya mambo
makubwa sana. (Soma; kama unadhani wewe una bahati mbaya na nini hasa ulichokosa)
Jua thamani ya utajiri unaomiliki ili uweze kuubadili kuwa utajiri wa
kifedha. Tumia ulichonacho na vinavyokuzunguka ili kufikia mafanikio
unayotaka. Umasikini ni hali ya fikra na wala sio kukosa umiliki wa
vitu.
Categories: