Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe


Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ametoa siku 90 kwa matrekta yote yanayoingia Bandari ya Dar es Salaam kubeba makontena kuacha mara moja.

Dk. Mwakyembe ametoa agizo hilo jana wakati akifungua Maonyesho ya Kilimo ya Nanenane yanayofanyika kikanda jijini Mbeya yakiwa na kaulimbiu ya “Zalisha Mazao ya Kilimo na Mifugo kwa kulenga Mahitaji ya Soko”.


“Matrekta mengi nimeyaona bandarini yakitumika kubeba mizigo, kwa mfano makontena, natoa miezi mitatu kuanzia sasa matrekta yote yanayotumika bandarini yaende yanakohitajika kwenye kilimo. Ikifika Oktoba 30

mwaka huu matrekta sitaki kuyaona bandarini,”alisema Dk. Mwakyembe.

Asema serikali imeweza kufuta ushuru wa zana za kilimo kama matrekta chini ya kampeni ya Kilimo

Kwanza, lakini matrekta mengi yaliyoingizwa kuwezesha kilimo kukua yameishia kubeba mizigo bandarini.

Alisema uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo katika mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ipo chini

sana ikilinganishwa na viwango vya utafiti, mfano hekta moja ya zao la mahindi inazalisha wastani wa tani tatu lakini utafiti unaonesha kwamba hekta moja ya zao la mahindi inaweza kuzalisha wastani wa tani saba za mahindi.


Alisema kwa upande wa maziwa wastani wa uzalishaji kwa ng’ombe mmoja kwa siku ni lita saba wakati kiwango kinachotakiwa kuzalishwa ni lita 20 kwa ng’ombe kwa siku.


Dk. Mwakyembe alisema upo umuhimu mkubwa wa kuyaongezea thamani mazao kwa njia ya viwanda vidogovidogo ili yauzike kwa haraka na kwa bei nzuri zaidi na kukidhi matakwa mbalimbali ya soko.


Aliongeza kuwa katika mwaka huu wa fedha serikali imeelekeza nguvu kubwa kupeleka umeme kwa wakulima kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA).


Alisema katika utekelezaji wa mradi huo vijiji 590 vya mikoa ya Mbeya, Katavi, Ruvuma, Rukwa, Njombe na Iringa vimetengewa kiasi cha Sh. bilioni 162.5 kwa miradi ya umeme ambayo utekelezaji wake

umeshaanza kwa kazi ya uteuzi wa makandarasi ambao wanatakiwa kuanza kazi ya usambazaji umeme mwezi Oktoba mwaka huu.


Alisema miradi hiyo ya umeme itachochea uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo vijijini vitakavyoongeza thamani ya mazao ya wakulima na kwamba serikali imechukua hatua ya ziada ya kupunguza gharama za kufungiwa umeme vijijini kwa asilimia 70.


Aliongeza kuwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini imetengewa zaidi ya Sh. bilioni 5 kwa kazi ya kukarabati barabara vijijini, matumizi ya fedha hizo yakisimamiwa vizuri itasaidia kuleta mabadiliko katika kusafirisha mazao vijijini.


Kuhusu sekta ya uchukuzi wa anga, reli na majini, alisema serikali inaendelea kuimarisha reli ya TAZARA kwa ushirikiano wa serikali zetu mbili za Tanzania na Zambia, tuko kwenye maandalizi ya ujenzi wa reli

kutoka Uyole kwenda Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira, kuunganisha Tunduma na bandari ya Kasanga katika Ziwa Tanganyika.


Kazi nyingine ni kuimarisha reli kutoka Tabora hadi Mpanda na kuiendeleza reli hiyo hadi bandari ndogo ya Kalema kwenye Ziwa Tanganyika pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwenye mikoa ya Ruvuma na Iringa, na barabara ya kuunganisha mikoa ya Rukwa, Katavi na Mbeya.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

Categories:

Leave a Reply