USHAURI KWA VIJANA: Kila mtu chini ya hili jua amepewa na Mwenyezi Mungu masaa 24 kwa siku, siku 7 za wiki, siku 30 kwa mwezi na siku 365 kwa mwaka (ukijaaliwa kuishi mwaka mzima!). Hakuna mtu yeyote duniani aliyependelewa masaa zaidi ya mwingine. Sote wakubwa, wadogo, waafrika, wachina, wamarekani, nk tumepewa masaa yaleyale 24 kwa siku. Jinsi utumiavyo hayo masaa yako, ni uamuzi wako mwenyewe.

MAMBO YANAYOSAIDIA KATIKA KUOKOA MUDA MWINGI;
Jana tulitaja baadhi ya mambo yanayopoteza muda mwingi wa vijana. Kila kijana atasema kati ya hayo ni baadhi yanayomkuta. Hata kama ni moja au mawili yanayokukuta, ni muhimu kufahamu maujanja ya kukusaidia kuokoa muda wako ili uutumie kwa mambo yatakayo kufaidisha. Mbinu zilizoelezwa hapa chini zimewapa watu mafanikio makubwa sana na hutumiwa na watu kuanzia ngazi za chini - masecretari, manesi, madaktari, mameneja, CEO hadi marais wa mataifa makubwa. Hivyo, usipuuze!

Unayo masaa 10 kati ya kila masaa 24 ambayo unaweza kuamua jinsi ya kuyatumia, ukitaka 'success' tumia busara zako katika kufanya uchaguzi huo.

- Chora jedwali lenye orodha ya mambo yote unayotaka kufanya na uweke nia ya kuifuata kama ulivyo orodhesha kwenye jedwali. Anza kwa kuandika vinote vyenye shughuli zisizokwepeka kama vile madarasa, muda wa kula, kazi na mikutano.

- Andika tarehe za lini kozi zako zitaisha, assignments, tests na mitihani ya mwisho itakapofanyika

- Fanya kazi zilizopo kwanza, acha tabia za kujichelewesha kwa makusudi, mfano kwenda dukani, kuanzisha kazi za usafi, matumizi ya simu yasiyokuwa ya lazima, nk

- Chagua muda utakojisomea na muda utakaofanya mambo ya ziada baadae utakapomaliza uliyo yaorodhesha kwenye jedwali

- Vunja muda wako katika vipisi vidogo vidogo – ni rahisi kwako kuhitimisha mambo kwa haraka ikiwa una muda wa kutosha kuyafanya.

- Unapoanza siku andika kwenye daftari au note book yako “TO DO" yenye orodha ya mambo muhimu zaidi ya kufanya kwa siku hiyo.

- Ukitimiza kila moja unatia tiki kwenye orodha yako ya ‘to do’ – hii itakupa hisia ya mafanikio na kuku ‘motivate’ ukiendelea na kumaliza mengine ambayo yanafuata kwenye orodha.

- Jitahidi kila siku utimize kazi chache – itasaidia kutokujilimbikizia mambo

- Tumia nyenzo kama ‘outlook calendar’ kwenye computer yako, diary au jedwali kwenye ukuta wako ili ikusaidie kupanga muda wako vizuri

- Jiwekee system ya ku file vitu vyako kwa umakini, weka pen, karatasi, na file kwenye box. Ukiwa na sehemu safi na nadhifu, itakupa mothisha wa kufikiria malengo yako na mambo mengine muhimu ya kutimiza

- Orodhesha majukumu au kazi ngumu zaidi ukiwa bado una nguvu na uwezo wa kutafakari (concentrate) zaidi (inaweza kuwa ni asubuhi au mchana, itategemea wewe huwa alert zaidi nyakati zipi). Usianze na kazi au majukumu ya rahisi na usikwepe kazi ngumu.

- Usiache kuweka mambo ya kukujenga kiroho itakusaidia sana. Tenga muda wa kumuabudu Mwenyezi Mungu pia.

- Husisha members katika familia yako kwenye jedwali (timetable), ili waweze pia kukusaidia vitu vichache unavyo ona.

- Uwe mkweli na makini katika kutenga muda muafaka wa kuyatimiza mambo na kazi zako katika muda utakaopanga. Usiweke kazi itachukua dakika 15 wakati ukijua fika inahitaji masaa mawili au zaidi.

- Pata usingizi wa kutosha, fanya mazoezi ya mwili na ule chakula bora

- Mwisho, usisahau kujiwekea ‘Me Time’ , muda wa kujifurahisha binafsi ni nzuri ili uweze ku enjoy vitu uvipendavyo binafsi – maisha ni zaidi ya kazi tu!

Kumbuka, muda ni pesa, ukichezea muda ni sawa na mtu anachezea pesa - jinsi utakavyo budget muda wako vizuri ndipo mafanikio yako yataongezeka. Tunakutakia siku njema!

kwa hisani ya shear illusions

Categories:

Leave a Reply