USHAURI KWA VIJANA: Kila mtu amepewa na Mwenyezi Mungu masaa 24 kwa siku, siku 7 za wiki, siku 30 kwa mwezi na siku 365 kwa mwaka. Mfano, Bill Gates, Wayne Rooney, Rihanna, Masanja, mimi, yule na wewe, sote tuna masaa 24 kwa siku. Jinsi utumiavyo hayo masaa yako 24, ni uamuzi wako mwenyewe. Mara nyingi kijana hujikuta hana muda wa kutosha kwa siku kumaliza mambo yote aliyopanga kuyafanya. Kijana hujikuta ana ahirisha shughuli au kazi alizopanga kufanya na kufanya mambo yasiyokuwa na maana. Ukiwa kijana, umewahi kufikiria kama muda hautoshi kuhudhuria madarasa yako yote, kujisomea kwa ajili ya mitihani, kusubmit assignments zako kwa wakati, kusoma facebook posts, ku-update status yako kwenye instagram, facebook, twitter, Whatsup, nk..., kufanya kazi part-time na kubakiza muda kwa ajili ya kujiangalia mwenyewe?

Wengi watatoa jibu kuwa 'ndiyo', muda hautoshi kufanya baadhi ya hivi vitu vyote kwa wakati. Leo tunakupa mbinu chache za kuweza kukusaidia jinsi ya kubalance na kumudu muda wako.

MAMBO YANAYOPOTEZA MUDA MWINGI WA VIJANA;
- Kila wakati kubadili ratiba au mambo uliyopanga kufanya
- Kushindwa kukamilisha kazi za muhimu
- Kushindwa kuwa na malengo ya wazi
- Kujiwekea mbinu za kuchelewesha mambo kwa makusudi, mfano kwenda kununua soda dukani au kufanya usafi wa chumba au kufua, matumizi ya simu bila sababu badala ya kutimiza mambo ya maana yanayokusubiri.
- Kusumbuliwa, wageni bila taarifa, maongezi yasiyo na mpangilio
- Kujilimbikizia mambo mengi kuliko uwezo kwa wakati mmoja
- Kushindwa kufahamu kuwa kuna baadhi ya mambo huhitaji muda mrefu kukamilika kuliko uliopanga
- Kuahirisha vitu bila sababu na kusahau kuviweka kwenye ratiba tena
- Kurukaruka toka kazi moja kwenda nyingine bila kumaliza uliyo anza kwanza
- Kuangalia TV, kusikiliza muziki, kucheza game, kuperuzi kwenye mitandao ya jamii (unapaswa utenge muda kwa ajili ya haya mambo – angalau lisaa limoja tu kwa siku)
- Kushindwa kusema ‘Hapana’ kwa vitu visivyo kuwa na msingi ulivyo ombwa kufanya
- Kukosa nidhamu binafsi (self-discipline) – na kushindwa kufuata Plan yako uliyojiwekea

source :shear illusion facebook page

Categories:

Leave a Reply