Mara baada ya kupata Tip#3 kwamba kila kijana anapaswa kuelewa
umuhimu wa Kujithamini (Self-esteem) na Kujiamini (Confidence) na kuwa
mambo haya mawili yanaweza kumjenga na kumbomoa mtu. Tulielezea baadhi
ya mambo yanayoendelea kichwani mwa mtu asiyejiamini wala kujithamini
(negative self-talk) huchangia katika kumrudisha mtu nyuma katika
maendeleo yake binafsi.
Unataka kujua jinsi ya kujisikia
vibaya na nafsi yako? Tunakudokezea kiduchu mambo yatakayo kufanya
ujisikie vibaya - tena vibaya kinoma kuhusu wewe na nafsi yako.
i) Jilinganishe wewe na kila mtu au kila kitu kilichokuzunguka. Chagua
vitu walivyonavyo ambavyo huna. Fikiria jinsi walivyo na bahati na wewe
ulivyo na mkosi
ii) Ukipata fursa yeyote ya kujiangusha, wewe
jiponde tu. Epuka kusema au kuamini kuwa wewe ni mtu wa pekee na huna
kasoro yeyote ile
iii) Kataa unaposifiwa. Waambie watu kuwa “ni
kitu kidogo tu hicho, usijali…” au wewe sio mtu wanaostahili kumpa sifa
au pongezi. Usimshukuru mtu yeyote anapokusifia, jifanye kama
hujasikia.
iv) Kila mara jiambie “mimi ni balaa tupu”, “mimi mjinga”, “sina mvuto”, “sipendwi” au “sifai”.
v) Jichanganye au jihusishe na vitu ambavyo vitakuangusha, kudhalilisha
na kukuvunjia heshima. Hii itasaidia hayo yaliyotajwa hapo juu kuzama
ndani yako zaidi.
vi) Kaa kila mara na orodha ya mambo
yaliyosababisha uanguke, ufeli, kukuaibisha, mambo uliyokosea na uziweke
kwenye kumbukumbu zako kwenye diary yako, chumbani umezibandika au
sehemu yeyote unayotaka wewe.
vii) Jitenge, kaa kivyakovyako
na usizoeane na watu wala usitake watu wakujue jue. Acha kumsifia mtu,
kusaidia watu wala kuchangia katika shughuli yeyote ile.
viii) Epuka kitu chochote kinachokuburudisha na unachopenda kufanya.
ix) Ishi maisha yako kwa kuwaridhisha watu wengine. Fanya maamuzi yako
yote kutokana na vitu watakavyo idhinisha na watakacho kifurahia
x) Usifanye kitu chochote kigeni kwenye maisha yako. Kaa nyuma na
usubiri miujiza au kitu kitokee na kiweze kuyabadilisha maisha yako.
Kuna wakati mwingine, tena bila hata kujitambua wenyewe, tunajikuta
tunafanya maamuzi ya kujiumiza tu. Hali halisi ni kuwa ungependa
kukaribisha hisia za kujiamini na kujithamini katika maisha yako.
Kuna njia nyingi sana za wewe kukaribisha hali ya kujithamini ndani ya
maisha yako. Badili kwanza fikra na mtazamo wako. Jipende wewe binafsi!
Acha kujiadhibu na kujipa wakati mgumu na anza kwa kujipongeza mwenyewe.
Matatizo, dhiki na shida za dunia zipo tangia enzi za manabii na
zitaendelea kuwepo siku nyingi baada ya wewe kuiaga hii dunia. "This is
your time, we only live once, live and embrace life". Wewe ni mtu
‘unique’ kwenye hii dunia. Hakuna mwingine kama wewe kati ya watu
billion 7 duniani. Nenda China, Nigeria, Rwanda au India ukatafute mtu
mwingine aliye kama wewe kabisa! Hakuna kama wewe.... uko peke yako - a
‘unique’ being. Zaidi ya mama aliyekuzaa, nobody atakupa ‘first class’
love zaidi yako mwenyewe kwanza. Jipende mwenyewe kwanza, ili wengine
wakupende vilevile. Ukianza kujilinganisha na wengine au mwingine,
lazima utajikuta unayo mapungufu kimaumbile, kimapato, na kwenye maisha
vile vile.
Hayo mambo 10 tuliyo orodhesha hapo, uyatumie
kuyabadilisha yawe katika "positive self-talk" na kama kichwa chako kina
mitazamo hiyo 10, uzifute moja moja kila siku kuanzia sasa, ili baada
ya siku 10, hata moja tena zimetoweka kichwani mwako. Achana na feelings
za kukupa ‘low self-esteem', hazitokusaidia chochote katika maisha
yako. Usiache ikatambaa na kukuganda na kukuharibia maisha yako. Pigana
kuanzia sasa na ubadilike uwe na mtazamo chanya. Kumbuka, hakuna SIRI ya
utajiri wala mafanikio, uliza kila mtu mwenye mafanikio ya hali ya juu.
Ataanza kukuambia, fikra, fikra, fikra... fikra zako ndizo zitakazo
kujenga au kukubomoa.
Tembelea ukurasa wetu kesho tukijaaliwa
tutazungumzia mbinu zitakazokusaidia katika kujijengea tabia za
kujiamini na ujifunze jinsi ya kuzifanya ziwe za kudumu katika maisha
yako. Tunakutakia siku njema!
kwa hisani ya shear illusions
Categories: