Leo
tutaangalia jinsi ambavyo maamuzi mazuri unayoyaamua katika maisha yako
yanavyokupa ujasiri wa kusonga mbele katika kufikia malengo
uliyojiwekea.
Kumbuka kama unataka kuwa mtu fulani katika jamii au
kuwa kiongozi, ni vema ukawa jasiri wa maamuzi yatayokufikisha kwenye
mafanikio.
Pia wapo watu wanaokuwa thabiti katika kufanya maamuzi,
lakini pia, kutekeleza inakuwa shida. “Ni jambo moja kuwa thabiti
kufanya maamuzi, lakini ni jambo Jingine kutendea kazi.”
Unapothubutu
kufanya jambo lolote ambalo unaona kuwa baadaye litakuletea mafanikio,
wewe ni jasiri. Tofauti na hapo unajimaliza mwenyewe, unakuwa mtu ambaye
mipango unayopanga inaishia kwenye mikoba.
Yeyote anayewekeza kwenye
mradi wowote, anayenunua gari au kufanya uamuzi wa kubadili kazi,
anajiwekea mkanganyiko katika maisha yake, lakini mwisho wa yote anavuna
furaha na maendeleo kwa kuwa anakuwa amepiga hatua nyingine katika
maisha yake, ambayo hakuwahi kuwa nayo.
Kwa upande wa watu ambao
hawapendi mabadiliko katika fikra zao kwa jambo lolote, huwa wanakosa
kila kitu. Hata kuwa na mafanikio makubwa katika maisha inakuwa ni
vigumu.
Kuwa mtu wa kupenda kuthubutu kufanya jambo lolote lenye mafanikio katika maisha.
Unapotaka
kusonga mbele, usichukie mawazo ya wengine wenye busara wanaokushauri,
japo wapo wengine ambao mara zote hawapendi kuona wenzao wanasonga
mbele, jiepushe nao. “ Kuwa na chuki ya kupata maoni kutoka kwa wengine,
ni jambo baya ambalo halitakufanya uendelee mbele,” inakupasa uchukue
maoni ya kila mmoja na kuyapima. Kamwe usipoteze muda na nguvu zako
kutafakari maoni yasiyo na maana.
Mara zote penda kujifunza kutokana
na makosa. Kuna msemo mmoja unaosema kuwa, kama umekosea ni vema kukiri
kosa lako. Wala usichukie unapoambiwa kuwa umekosea, jifunze kutokana na
makosa yako.
Kila tatizo lina utatuzi wake. Kwani hakuna jambo
lolote katika sura ya dunia ambalo halina utatuzi. Kila tatizo
linalojulikana kwa mwanadamu linapatiwa ufumbuzi.
Japo wakati
mwingine tatizo lako linaweza kuonekana ni la kipekee, jua kuwa wengine
wameshakabiliana nalo na kulitafutia ufumbuzi.
Matatizo yote yanayompata mwanadamu, ufumbuzi wake unapatikana, kwani kila tatizo lina mlango wake wa kutokea.
Acha
kufikiria matatizo unayokutana nayo, hata kama ni mazito kiasi gani,
kadiri unavyoruhusu akili yako kufikiria matatizo yanayokukabili ndivyo
yanavyozaliwa mengine ambayo hayakuwepo.
Jaribu kupata ufumbuzi wa kila tatizo lililopo mbele yako ili uweze kusonga mbele.
Jipe
nafasi ya kufikiri, jipe nafasi hiyo pale unapokuwa na jambo zito
linalokutatiza. “Jipe nafasi ya kutulia nyumbani kwako, unapokuwa umekaa
kwenye kiti chako, wakati huo utakuwa unapata ufumbuzi wa tatizo
linalokukabili.” Wakati huo ni vizuri ukawa na furaha na ushindi wa
majibu ya matatizo yanayokukabili.
Ondoa hofu, kwa kuwa mara zote
ndiyo inayoharibu uwezo wako wa kuwa na maamuzi ya busara. Kwani hofu
inatokana na uamuzi mbaya wa matatizo yako. “Hofu ni adui mkubwa wa
matatizo yako.” Inafikia hatua watu wengine huogopa kifo, kutokana na
hofu waliyonayo.
Mara nyingine hofu inatokea kwa sababu ya kutokujua ukweli wa jambo, usipoteze nguvu zako kufikiria kitu ambacho haukijui.
Categories: