UFUPISHO.
Samuel
na Sadiki wametoka katika familia zilizokuwa za dini. Samuel alikuwa
mtoto wa mchungaji Kipelele wa kanisa la Praise and Worship lililokuwa
mwenge jijini dar es Salaam huku Sadiki akiwa mtoto wa Imamu wa msikiti
wa kichangani uliokuwa magomeni jijini Dar es Salaam. Wote wanasoma
katika shule ya Uhuru mkoani Kilimanjaro. Kutokana na kupenda sana dini,
muda wote wanaonekana kuwa watakatifu huku walimu wakiwataka wanafunzi
wote shuleni hapo waige maisha yao.
Mambo
yanaonekana
kubadilika, uwepo wa msichana Catherine Mushi na Mariamu Saidi
unaonekana kuanza kubadilisha kila kitu. Wote wawili wanajikuta
wakiangukia katika ulimwengu wa mapenzi, wanaziacha dini zao, wanagoma
kwenda msikitini na kanisani. Mapenzi hayo yaliyowafanya kuziacha dini
zao ndio mapenzi ambayo yaliwafanya wawili hawa kuingia katika mtafaruku
mkubwa, mtafaruku ambao unaibua chuki kubwa mioyoni mwao huku wakiwa
wamejiingiza katika kitu ambacho kiliwapa utajiri mkubwa ambao kwa
muonekano tu, haukuwa utajiri wa halali kabisa.
MAPENZI.
Yakawafanya kuchukiana, mapenzi yakaonekana kusababisha kifo maishani
mwao, ila hayo hayo mapenzi, yaliwafanya kumsahau MUNGU wao.
Unajua nini kilitokea katika maisha ya watu hawa?
Pata nakala yako.
Kitabu
kitatolewa siku ya Ijumaa. Kwa wakazi wa dar es salaam watafikishiwa
walipo na kwa wakazi wa mikoani, watatumiwa huko huko kupitia kwa
mawakala wetu. Kitabu kimoja kitapatikana kwa sh 7000/= tu. Kama unataka
kuweka oda na kupata maelezo mengine unawaza kupiga simu hii 0718 069
269.
Categories: