LEO TUMECHUKUA TOPIC KUPITIA FACEBOOK
Lazima
kufahamu kuwa hata kama mazingira yanayokuzunguka yanakuonyesha kwamba
wewe ni wa kushindwa kwasababu wengi kwenu wameshindwa na wala hakuna
kitu cha ushindi chaweza toka kwako bado hustahili kuuondoa kichwani
kwako ukweli kwamba historia ya ushindi kwako haijaanza leo bali ilianza
tangu siku ile mbegu moja ya uzazi ya baba yako “sperm” iliposhinda
mbio katikati ya mbegu zaidi ya
mamilioni zilizokuwa zikishindana kuingia katika yai la mama yako kwa
kasi ya ajabu, nyingine nyingi zikafa nyiani baada ya kushindwa
kukabiliana na kasi pamoja na ugumu wa safari ile. Mbegu moja tu,
inayoitwa “wewe” ndiyo ilishinda na alama ya ushindi huo ni kuwepo kwa
“wewe” unayesoma ujumbe huu. Kwahiyo basi upitapo katika ugumu na
vipingamizi tele vya maisha, paza sauti yako kuyaelekea mazingira hayo
magumu na uyaambie “kushinda sijaanza leo” – Chris Mauki
Categories: