Name:  love.jpg
Views: 0
Size:  5.4 KB

Hi


wanajamvi wenzangu natumai mko fiti na mnaendelea
na majukumu kwa wale walioko job, wafanyabiashara na
wasomi pia ilakwa wale ambao wanajipumzisha kila lakheri

Weekend hii nimefurahi sana kuwaambia kitu ambacho ni
muhimu sana hasa katika mahusiano yetu yawe ya mmoja,
urafiki, undugu, ujamaa, ujirani na hata mahusiano ya
kwenye Ndoa. Jambo la muhimu kwenye mahusiano ni
hili la kuzingatia kuwa na Upendo wa dhati na sio wa
unafiki kwa yule umpendaye hasa hasa. Huna budi kuonesha
kuwa umekubalika kwake na kuwa mmojawapo katika nafasi
yake na vilevile huna budi kuonesha Upendo wa vitendo kwa
huyo umpendaye au uwapendao ili kudumisha hisia, penzi, na
undugu wa kweli kati yetu.


Zipo baadhi tu za dokezo ambazo zaweza kuwa sababisho la
wewe kufanya yule umpendaye awe mume, mwenzi, au rafiki
yako wa karibu kuvutiwa nawe na kuona kuwa wewe unamjali

Dondoo za Upendo wa agape:-

a) Huna budi kuwa nae karibu huku ukimpa maneno yenye
nyama ya ulimi usiokuwa na mfupa yaani kumbembeleza
kwa laini na yenye mvuto huku ukimwambia kuwa
unampenda hata kama amekukosea au pale unapoona
kuwa yu mashakani au ameumizwa uko alikotoka/ au
kapatwa na jambo la huzuni au furaha wewe onesha
uko pamoja nae.

b) Kuonesha kwa hisia za karibu sana tena kwa vitendo
kwa yule umpendaye japo kumnunulia kazawadi kawe
kakubwa au kadogo kutokana na jinsi mfuko wako wa
wa fedha kile kidogo ulichonacho kitamfanya aone kuwa
unajali na kumthamini vile yeye alivyo.

c) Onesha kujali pale ambapo anataka kuongea au kusema
na wewe na onesha kuwa uko pamoja nae katika yale
ayaongeayo yawe ni mambo yahusuyo maisha au ninyi
kazi, masomo, na hata biashara pia wewe kuwa msikivu

d) Jali na penda ndugu au familia yake au jali wale ambao
huko katika familia yako kwa ujumla, na hata marafiki zako
onesha kuwa uko pamoja nao katika furaha na huzuni hata
katika mambo mazito na magumu wewe kuwa mfumbuzi wa
hayo matatizo yaliyowapata wenzako wengine.

e) Jiheshimu na waheshimu marafiki, ndugu , jamaa, jirani hata
huyo uliyenaye kwani unapowaheshimu na kujiheshimu wa
leta kupendwa zaidi na hao wakuzungukao. na unaleta
amani, furaha kwao.

f) Kuwa mtu mwenye kudadisi na kubuni jambo ambalo wengine
hasa marafiki zakio watalipenda na kukupa support kwa jambo
hilo kwakufanya hivyo utajiletea na kujiongezea marafiki wengi
na wengi watakuita bora.

g) Kuwa mtu mwenye uchangamfu na mpole kwa kiasi na usipende
makuu hata kama uwezo wako ni mdogo ishi vile ulivyo na sio
kuiga wengine walivyo. Ukifanya hivyo utajiongezea kupendwa
na wale ndugu, jirani hata mwenzi wako naye atafurahi kuona
kuwa niliyenaye si mtu anayependa makuu na mwenye kujitukuza

TAMATI:
wapendwa wangu marafiki zangu napenda kuwashauri kuwa uwe
mtu mwenye mfano wa kuigwa na wengine kwa kuonesha upendo
usio na unafiki wala choyo kwani utakapokuwa hivyo utajijengea
heshima, kupendwa, na hata kuwa na marafiki wengi na pale
utakapopita katika magumu hao marafiki zako au ndugu zako
watakufaa zaidi.

Sitamsahau laaziz wangu Mentor anayenipa usingizi mwororo na
kunifanya niwe kila wakati nikimuwaza yeye kwa kumSURPRISE
namna hii kwa kazawadi kadogo haka hapa pokea bestito
Click image for larger version. 

Name: orange.jpg 
Views: 0 
Size: 12.0 KB 
ID: 93214

Mwisho kabisa acha niseme kuwa nawapenda marafiki zangu na
pokeeni zawadi hii ya upendo wangu kwangu Name:  ilove u.jpg
Views: 0
Size:  7.0 KB
kwahisani ya lady furahia my best friend member of jf

Categories:

Leave a Reply