Watu wengi wamekuwa wakijiuliza biashara za kuanza kufanya, wakati
mwingine kumekuwa na baadhi ya watu ambao huwa na kianzio cha biashara
(mtaji), lakini hawafahamu ni biashara gani wataweza kufanya.
Fursa ya Biashara (Business Oppurtunity) hutokana na mahitaji ya
watu katika eneo husika; kwahiyo katika kutengeneza wazo la biashara
(Business idea) huanza kwanza kwa kuchunuguza fursa zilizopo katika eneo
husika. Baada ya hapo hufuata mpango wa biashara (Business Plan).
Kwa hiyo unapofikiria ni biashara gani ya kufanya ni vyema
kuchunguza mahitaji yaliyopo katika eneo husika (inaweza kuwa mtaani
kwako, katika mji au hitaji la Taifa). Kwa kweli nchi yetu bado kuna
mahitaji mengi ambayo yanaweza kutumika kama fursa ya biashara; hebu
jiulize toka unapoamka ni mahitaji au shida kiasi gani umekutana nazo,
naomba kuorodhesha baadhi ya maeneo ambayo tunaweza kuchunguza mahitaji:
1. Unapotaka kwenda kuoga asubuhi nyumbani kwako, unapata maji kwa
urahisi?
2. Je unapotaka kupata kifungua kinywa, unapata kitafunio kwa
urahisi?
3. Je unapotaka kwenda kazini au kwenye shughuli zozote, usafiri
kutoka eneo lako uko vipi?
4. Unapofika katika eneo lako la kazi au shughuli yeyote kuna
vitendea kazi vya kutosha?
5. Vitu gani vinakufanya kushindwa kutekeleza majukumu yako ya kazi
au shughuli za kila siku?
6. Unapotaka kupata chakula cha mchana, je unapata katika mazingira
gani?
7. .............................
8. .............................
Wengine wanaweza kuendeleza, mambo ambayo tunaweza kuchunguza
kutokana na mazingira husika.
Jambo lolote ambalo utaliona ni hitaji kwa watu basi hiyo ndio fursa
ya biashara, kwa hiyo unapaswa kutengeza wazo la biashara. Tuache
kuyachukulia mazingira yanayotuzunguka na mambo yanayoendelea katika
jamii kuwa ni kawaida, kwa mfano unaweza kuwa unakwenda kupanda daladala
kila siku kwa kugombania na ukachukulia hiyo ndio hali ya kawaida,
lakini tunaweza kutumia hiyo hali kama fursa ya biashara na kutengeneza
wazo la biashara.
Tunapoaangalia mahitaji ya watu na kugeuza kama fursa ya biashara,
basi hapo tutakuwa tunafanya biashara lakini vile vile tutakuwa
tumekutana na mahitaji ya jamii inayotuzunguka na taifa kwa ujumla, kwa
kweli jamii yetu bado ina mahitaji mengi; itashangaza kusikia kwamba
hatujui nini cha kufanya na jamii inayotuzunguka. Hebu tuige mfano wa
Mjasiriamali Bakhresa na kampuni yake ya AZAM, kwamba amekuwa
akichunguza mahitaji ya jamii na kuleta bidhaa ambayo itakutana na
hitaji hilo, mfano; CHAPATI, MIKATE, TUI LA NAZI na nyinginezo.
Vile vile tujifunze kutofautisha fursa za biashara katika nchi
zilizoendelea na nchi zinazoendelea kama ya kwetu; kwani upatikanaji wa
fursa za biashara ndani ya Marekani ni tofauti na Tanzania; ndio maana
katika nchi zilizoendelea wamekuwa na biashara za mitandao na biashara
nyinginezo ambazo zisikiri kama zinaweza kuwa na ufanisi mkubwa zaidi
kutokana na mazingira yetu; kwani nimeshawahi kuona baadhi ya link
zikielekeza jinsi ya kutengeza fedha ka jinsi ya mtandao n.k. Nafikiri
bado jamii yetu ina mahitaji mengi ambayo yanahitaji mtu wa kuyatatua.
Nawatakia kila la kheri wajasiriamali wenzangu, katika kukutana na
mahitaji ya jamii inayotuzunguka na kupunguza hili wimbi kubwa la
kutegemea bidhaa kutoka nje; yaani tumeshindwa hata vijiti vya kusafisha
meno, miti ya kuchoma mishikaki n.k, vimekuwa vikitoka China; hawa watu
wamekuwa wakitoka mbali na wakifika hapa wanabaini fursa za biashara na
kurudi kwao kutendea kazi.
source:Mgombezi member of jf
Categories: