Nimekuwa naumia sana nikiona mwanafunzi yeyote yule akifeli mtihani wowote ule wa darasani au chemsha bongo za kimataifa,maisha yangu ya shule yalikuwa na furaha sana kwa sababunilikuwa sijui neno kufeli au kuwa namba mbili darasani(shuleni kwangu kote) kwa mitihani ya kitaifa na ndani ya shule.Kila muda nikiona kuna mwanafunzi anafeli naanza kujaribu kuwa naye karibu ili naye aweze fanya vema awe kama mimi Deogratius kilawe,kwa hakika nilifanikiwa sema kwa kiwango sio kikubwa sana kutokana muda kuwa mdogo na miundo mbinu ya kuwafikia wanafunzi wote wanapata haya matatizo ya kufeli au wanaofauli lakini hawajui hata kwa nini wanafanafaulu  na kufikiria ni kitu automatic kutoka sehemu fulani na kuja kwao na siku wakianza feli wanasema kuwa wamerogwa.Kama ilivyo kwa mafanikio mengine kufanikiwa ni juhudi fulani mtu anazifanya ili mafanikio yatokee.Akili ina kazi nyingi moja wapo ni kutunza taarifa,darasani ili uweze faulu inabidi uweze kuelewa na kutunza taarifa kile ulichofundishwa na kutema kwenye karatasi ya mtihani,sehemu hii kutunza kumbukumbu ndio sehemu ukurasa huu wa jinsi ya kufaulu mtihani unahusika.Kadri unavyoweka juhudi ya kutunza vema kumbukumbu ndio mafanikio darasani yanakuwa makubwa na sehemu nyingine.Kama nilivyoeleza vema kwa topic ya jinsi ya kutunza kumbukumbuku napenda kuenda moja  vitu muhimu vya kumfanya mwanafunzi afaulu:

 
  (i)Manzingira akili ulivyo itengeneza,wewe unaonaje masomo?magumu au marahisi?akili ni mjakazi wetu sisi wanadamu hutii kile sisi tunachokiambia mfano kama unaona somo au masomo fulani magumu akili hutii na kuamini hivyo,ukiamini kama masomo fulani au somo fulani ni rahisi nayo hutii hivyo hivyo.Akili hubadilika kulingana na wewe unavyobadilika.Sasa kama mwanafunzi weka mtizamo wako sasa sahihi,Kila somo linawezekana,maraisi,hamna kitu hakiwezekani,kama ni mwanadamu wenzako kaweka mfumo huo na katungua mawazo hayo kwa nini wewe ushindwe?wote mna maasaa 24?wote mna lala na kuamka,wote mnakula na kwenda haja,wote mnaweza kuwa na hudhuzi na furaha,kwa nini kitu fulani aweze wewe uweze?basi nini wewe unatakiwa ubadilike,uanze amini lazima ufanikiwe,maisha yanakupatia kile unawekea umakini kila siku.
  (ii)Material manzuri,Lazima uwe na malighafi nzuri,dadisi material gani wezako wanaofaulu wanayatumia,nenda kwa waliokutangulia mwaka wa masomo uulize,tafuta material yaliyo marahisi kueleweka,kuna waandishi wengine wa vitabu hupenda kufanya mambo kuwa magumu kwa kuandika mambo mepesi sana kwa kutumia lugha ngumu sana ya zamani ili wapate umaarufu na baadhi ya mashulei kuweka vitabu vyenye lugha  ngumu sana kwa maktaba zao na kupelekea wanafunzi kufeli mitihani yao,epuka waandishi wanaotumia lugha ngumu hata yeye mwenyewe ukienda kumuuliza nini maana neno fulani siku hiyo hadi aende kwa kamusi kutizama maana yake,Penda kwenda kuchukua material kwa shule zenye ksifika kufaulisha vema,mimi nilikuwa naenda kuchukua material mbambali kwa shule kama mirian girls,st franscis,Maua seminari, mzumbe,nk Hakikisha kila aina la tirio unalo,usikubali kuingia kwenda kufanya mtihani pasipo kupitia mambo muhimu
  (iii)Muda sio kila muda wa kusoma,kuna muda akili inaingiza taarifa na kuhifadhi kwa haraka sana kuliko muda mwingine,Katika tafiti za taasisi mbalimbali huu ndio muda ambayo ukisoma akili huhifadhi taarifa kwa haraka kuliko muda wowote:


(a)Saa kumi usiku hadi saa nne asubuhi,ukisoma katika muda huu akili huingiza taarifa na kuhifadhi kwa haraka kuliko muda wowote ule.

(b)Saa kumi jioni hadi saa nne usiku, Ukisoma katika muda huu akili huingia taarifa kuliko muda wowote.

Kuanza kusoma usiku kucha ni kukosa maarifa,maana akili inamuda wake wa kufanya kazi kwa ufanisi na baadae kuchoka na muda ambao huchoka ni kuanzia saa tano asubuhi hadi saa kumi jion,na saa nne usiku hadi saa kumi usiku ,katika muda huu hata kama ukilazimisha kusoma akili kiwango cha kuingiza taarifaa ni kidogo sana na hivyo kuishia kushindwa.
Umewahi sikia eti mtu fulani alikuwa anasoma sana lakini siku ya mwisho akafeli?au umewahi sikia watu ambao wanasoma sana muda wote lakini wanafeli sana darsani?umewasikia watu wanasoma muda wa mchana na kukesha usiku na kuishia kupata maksi za wastani darasani?Ni kwa sababu ya ku-time muda ganu akili inaingiza taarifa kuliko mwingine.

 Huo muda mwingine unaweza tumia kwa kuingia madarasani na kumsikiliza mwalimu na pia kufanya discussion.

(iv)Fanya kazi kwa juhudi na kuwa na mentor wako:Ili uweze fanikiwa inabidi ufanye kazi kwa juhudi sana,lakini kwenye mfumo huu wa maisha potote duniani ulivyotengenezwa inabidi mtu ili ufanye vema sana uwe na mentor,mtu ambaye amefanikiwa na amekuzidi kidato au elimu,unapata maelekezo yakeo ili na wewe uwe zaidi ya pale alipofika yeye.
sourcehttp://www.achieversmagazine.blogspot.in/search?updated-max=2013-03-02T01:44:00-08:00

Categories:

Leave a Reply