Maisha ya biashara ili yaweze kufanikiwa vema na kuepuka kushindwa yanahitaji ubunifu wa hali ya juu wa kipawa chako na pia uzoefu wa huduma nzuri wa kutoka kwa watu wengine alisema Brian Adam,Hii ni kweli kabisa kwa maana huwezi fanya kila jambo wewe,unategemea kutoka kwa wengine,Maisha haya yote tunayoishi tunategemeana,Hivyo kama wafanyabiashara tunahitaji msaada kutoka kwa watu wengine,Ndio maana makampuni huwa hukodi wakala wa kuajiri wafanyakazi wapya wazuri,pia hukodi kampuni ya kufanya usafi,kuhusika na technologia na taarifa,kuhusika na ushauri wa kiongozi wa managementi,kutoa ushauri wa kifedha wa kampuni nk.
Kama wewe ni mfanyabiashara unataka fanikiwa sana inabidi uwe mwangalifu sana jinsi ya kuchagua timu kazi utakayoshirikiana nayo kwanjia moja au nyingine ili kufikia pale unapopataka,Hii ni timu amabyo kama mfanyabiashara unatakiwa uwe nayo:

1.Muhasibu:Muhasibu aliyebobea na mwenye weledi juu mambo kodi ni mmoja wa watu muhimi sana mfanyabiashara unatakiwa uwe nayo,Muhasibu atakusaidi kukuokolea fedha kubwa ambayo ungeweza kulipa kodi pia na ni muhimu sana katika ushauri wa uwekezaji.

2.Banki:Chagua benki ya chagua lako kwa uangalifu,tengeneza urafiki wa karibu na manega(manager) wa benki husika,Weka fedha zako benki mara kwa mara usijali hata ikiwa ni fedha ndogo kiasi gani,Hii itaonyesha upo makini sana katika kuweka fedha benki,Hiki ni chanzo cha manega(manager) wa benki kukupatia kiasi chochote cha fedha unachokihitaji kwa ajili ya upanuzi wa biashara yako.

3.Wakala wa bima:Bima ni chanzo cha ulizi na uwekezaji wa biashara yako,Tafuta wakala wa bima mwenye weledi ya kazi hiyo katika hali ya urafiki

4.Wakala wa shamba na nyumba:Biashara ya majumba imetengeza matajiri wengi sana duniani,wengi wamekuwa waki nunua mashamba,majengo na majumba yasiyoendelezwa kwa bei ndogo na kuyaboresha kwa gharama ndogo kisha kuyauza kwa bei kubwa na kuwa matajiri wakubwa sana duniani,Mawakala wa majumba na mashamba wanajua majengo gani yanauzwa na kwa bei gani na faida yake baadae.

5.Mshauri wa sheria na mwanasheria:Mwanasheria mwenye uwezo mkubwa na weledi mkubwa ni uwekezaji mkubwa unaweza fanya.Tafuta mmoja kwa ushauri katika mikataba yako yote na mambo mengine ni muhimu sana ili usije ukapata hasara kubwa sana.

6.Daktari:Hutoweza fanya kazi siku zote kama siku ukiwa unaumwa,kuna sababu kuuumwa tumbo,kiuono,meno,,nervous tension,vidonda vya tumbo,daktari anajua sababu za kuumwa.Penda kumuona daktaari mara kwa mara kwa vipimo mbalimbali ,pia jisikie vizuru na kufuata elimu daktari wako anakupati ambayo inaenda kwenda kukusaidi kimwili na kiakili.
7.Mshauri wa maswala ya kiroho:mshauri wa maswala ya kiroho ni muhimu sana kukuongoza katika kujitambua,pia kukupatia ukweli juu ya mambo mbalimbali ya kukongoza safari yako ya kiroho,kuna wakati katika maisha unashindwa songa mbele lakini ukipata ushauri wa kiroho unaweza songa.

8.Msiri/mwaminifu wa mambo yako binafsi:Kila mtu anahitaji walau rafiki wa kuabadilishana ushauri juu ya mambo yako binafsi,kukupatia msaada kipindi cha dharura na huyu ndio rafiki yako daima na hapa mara nyingi huwa mkeo au kama mwanamke huwa mumeo au mzazi wako.

9.Mwaminifu wa mambo yako ya biashara:Tengeneza uhusiano na wafanyabiashara wezako katika ofisi yako au kampuni unayofanya nayo kazi,na mmoja wapo ambaye atakupatia ushauri wa mambo mbalimbali ya biashara.

10.Wakala wa hisa:kama unataka kuingia kwa soko la hisa unahitaji mtu amabye atakupatia ushauri wapi ununue hisa na kipindi gani gani uuze hisa.Tengenza urafiki na mawakala wa hisa sasa kwa kuwa hawa wana taarifa zaidi na kujua mfumo unavyokwenda.
source: http://achieversmagazine.blogspot.com/

Categories:

Leave a Reply