Wengi huamini kuwa lazima uwe na fedha
ndio uanzishe biashara na ndio sababu yao kuu ya kukaa bila
kujishughulisha,Ukweli ni kwamba mtaji ni moja ya kitu muhimu sana katika
kuanzisha biashara,lakini kuna aina ya biashara ambazo zinahitaji gharama ndogo
sana kuanzisha na kukupelekea kupata faida kubwa sana.Kama mfanyabiashara unaweza kutoka kwa kishindo sana kwa kuanza ukiwa huna kitu na kufanya kazi kwa
juhudi sana ukiwa upande wa huduma(services)
na kufanikiwa kutengeneza faida kubwa na kutokea hapo na kuanza kufikiria
kuanza kukodi ofisi yako,kuajiri watu wengine nk ,ingawa ni rahisi kutoka ukiwa
upande wa huduma lakini inahitaji ujuzi
au weledi Fulani hivi ili uweze fika kilele cha mafanikio hapa simaanishi
lazima uwe umesoma chuo kikuu maana ujuzi au utaalamu wa jambo halihusiani na
degree ya chuo kikuu.
Unaweza pata ujuzi kwa kuhudhuria
semina mbalimbali,workshop mbalimbali,au kufundishwa na mtu wenye ujuzi husika
na baada ya kupata ujuzi kuanza fanyia kazi katika maisha yako ya kawaida kila
siku na kuwa bora kwa upande huo.
Nimejaribu kuorodhesha aina zaidi ya 14 unaweza anzisha pasipo kuwa
na mtaji kabisa au mtaji kidogo sana.Hizi ni aina ya biashara ambazo
nimezifanya kwa muda sasa na kuona matunda yake na nyingine nimeshuhudia watu
wakifanya na kufanikiwa.
Kama kweli una shauku la kweli kuanza leo biashara
soma kwa umakini sana na kuona je ni
wapi pa kuanzia ili uweze timiza lengo lako la maisha:
i. Huduma za
kuandika miradi biashara(business plan),kama ilivyo kwa tafiti za
uchanganuzi yakinifu(hali halisi ya biashara)wajasiriamali wengi huwa huepuka
kufanya kazi hii ngumu ya kuandika mradi biashara(business plan) yao.Ukweli ni
kuwa wajasiriamali wengi hawajui hata kuandika business plan katika uwezo wa
kuwashawishi wawekezaji kuja kuwekeza na huwa hawawekezi muda wa kutosha
kujifunza kwa hilo.Kama unaweza timiza hitaji hili biashara ipo mikononi kwako.
ii. Mshauri wa mambo
ya biashara:Wewe ni unauzoefu wa ujasiriamali au mmliki wa biashara?Unajua
nini kinahitajika ili uanzishe biashara,kujenga biashara,kuingoza biashara na
kukua?Sasa unaweza kuanza kazi ya ushauri wa biashara.Unaweza saidia kampuni au
biashara mbalimbali kutoka chini ya uvungu na kwa kutoa ushauri na maelekezo
muhimu.Unaweza kuwasaidi watu walioajiriwa kuanza kutoka kwenye ajira na
kuingia kwa ujasiriamali kwa malipo.
iii.
Huduma za
kuandaa vitabu vya mahesabu.Wewe ni mzuri katika kuandaa vitabu vya uhasibu
vya kampuni au biashara mbalimbali?unaweza weka ulingano kwa vitabu kwa vya
uhasibu(hili ni jambo huwa na shauku kulipata)? Sasa hamna kitu kinaweza
kukuzuia wewe kuanza huduma za kuandaa vitabu vya mahesabu anza sasa.
iv.
Kutoa huduma ya
kuandaa nakuendesha matukio(Event management),kampuni nyingi kila mara huwa
na matukio mbalimbali mfano semina,siku ya familia,sherehe mbalimbali mara
nyingi kampuni kama kampuni haiwezi kufanikisha kwa ufanisi uandaaji wa matukio
haya,na hivi ndivyo ilivyo kutokana na wafanyakazi wao kuwa na majukumu husika
tofauti na kuandaa matukio ya kampuni na kuyasimamia,hivyo ili kuwa na ufanisi
hapa inabidi kampuni zikodi watu wan je wenye ujuzi wa kuandaa shughuli husika
kwa uhakika,wewe kama una ujuzi na uzoefu wa kuandaa shughuli kama hizo mwanzo mpaka mwisho uwanja
ni wako.Mfano kuna matukio kama siku ya familia,semina kwa wafanyakazi,maonyesho
ya biashara ndani nan je ya nchi kwa kampuni husika nk
v.
Kuanzisha tovuti
kwa huduma mbalimbali,Kwa afrika watu kunufaika na tovuti ndio kwanza ipo
steji za mwanzoni,Unaweza anzisha tovuti na kutoa huduma ya taarifa watu
wanatafuta ,baada kuwa mmiminiko wa watu wengi wanaotembelea tovuti
yako,unaweza sasa ongea na kampuni kadhaa kuja kutangaza na wewe na kutengeneza fedha za kutosha.Kama hujui
jinsi ya kutengeneza tovuti usijali kuna tovuti za bure kabisa ambazo zimetengenezwa tayari kinachohitajika
ni wewe kujaza fomu zao na ndani ya dakika moja unakuwa na wewe tovuti yako,na kama unahitaji nunua
domain unaweza ikawa moja kwa moja tovuti yako.Tovuti unazoweza ingia na
kutengeneza tovuti yako bure ni www.webs.com
nk au pia unaweza tengeneza blog ikawa ni
unaweka taarifa watu wanatafuta na kisha kutafut wadhamini wa hiyo blog.
vi.
Mshauri wa
masoko,Je wewe unaweza nionyesha mimi njia ya gharama ndogo ya kuongeza
wateja wangu kuanzia aslimia 30% -70% au
zaidi?kama ndio biashara ipo mikononi mwako.Unaweza jiweka wewe mwenyewe katika
ushauri wa masoko kwa wamiliki biashara
ndogo na kati hata kubwa jinsi ya kuteka na kuwavuta wateja na kuongeza mauzo
ya bidhaa kwa ada Fulani ,kutokana huduma husika.
vii.
Mtafasiri wa
maandiko mbalimbali kwenda lugha ya wazawa;Kampuni nyingi za nje zinazokuja
hapa nchini,huwa wanahitaji kutafsiri taarifa zao kwenda lugha ya wazawa,mfano
mradi Fulani,tovuti zao,mfano kama ni kampuni ya vitabu mwandishi mmiliki
angependa ili auze kwa wazawa inabidi atafasiri kwenda lugha ya wazawa,Pia
mfano kuna hata miradi mbalimbali ambayo inatakiwaiangaliwe na wazawa nk.
viii.
Kutafiti fursa
mpya za biashara,Nina marafiki wangu ambao walianza kutoa huduma ya kutafi
fursa mpya na wanafanya vema kwenye hii biashara.Wanachofanya kutupia jicho kwa
mambo yajayo,mwelekeo,mahitaji aua fursa za biashara;na kuandaa mradi/mpango
kuhusiana hilo na kuuza hilo wazo kwa makampuni makubwa.Wakati mwingine
wanakuja na mawazo ya bidhaa na mawazo ya biashara yenye soko moja kwa moja
kubwa la kutosha;na kuuza hayo mawazo kwa makampuni kwa ajili ya
kuayaendeleza.Kama kazi hii unaipenda unaweza anza kutoa hudumu kutafiti fursa
mpya za biashara
ix.
Kutoa huduma za
ku-print,Biashara hii inafahamika sana na wengilakini bado inalipa
sana.Unaweza kuanza kutoa huduma ya ku-print business,banner sposters
card,viperushi,flyers,catalogues kwa biashara ndogo na za kati.
x.
Kutoa huduma za
kuajiri,Siku hizi kazi za managementi
za rasilimali watu kwa kampuni nyingi hutolewa na tenda kwa kampuni za nje ya
kampuni husika kufanya hiyo kazi ili kuongeza ufanisi kwa kampuni husika na
hivyo kupelekea kampuni husika kuweka umakini wake wa kutimiza lengo lake
mahususi.Kama una uelewa na ujuzi wa kutosha wa kushughulika na maswala ya rasiliamali watu uwanja ni
wako,kwa sasa hapa Tanzania kujisajili kuwa wakala wa kuajiri ni bure unatakiwa
uende pale wizara ya ajira na vijana kujisajili.
xi.
Mshauri wa
mitandao ya kijamii (social media consultancy),Kwa hii dunia mitandao ya
kijamii imechukua asilimia kubwa sana.Je wewe unajua jinsi ya kutengeneza
foleni kwa mitandao ya kijamii?Unajua jinsi ya kuboresha na kuelimisha umma juu
ya chapa(brand) za makampuni ndani ya
mitandao ya kijamii kama facebook,twitter na linkedin?Basi unaweza kuwa mashauri
wa mitandao ya kijamii na kutengeneza fedha
zako.
xii.
Kutoa huduma za
kuandikisha majina ya kampuni,Je wewe ni mzuri katika kuandika katiba za
kampuni?unajua jinsi ya kuchagua jina
sahihi la kampuni?unajua stepu zinazohitajika ili ukamilishe uandikishe
jina la biashara?Anza sasa fungua biashara yako ya kutoa huduma za kuandikisha
majina ya kampuni .
Huduma
nyingine unaweza fanya ili kutengeneza fedha:
xiii.
Kutoa huduma za kuandikisha hakimili za bidhaa au
huduma yako
xiv.
Huduma za ushauri kwa biashara ndogo
Imeandikwa na
:Deogratius kilawe
:Mshauri wa mambo
ya biashara
:deogratiuskilawe@yahoo.com
:+255717109362
SOURCE http://www.achieversmagazine.blogspot.in/search?updated-max=2013-02-15T04:12:00-08:00&max-results=20&start=
Categories: