source of this photo
 http://www.flickr.com/photos/colourblindartist/8504075836/
Bado tuna tatizo kubwa sana katika huduma (customer service) iwe katika ofisi,maduka,hosp nk..katika pitapita nakumbuka kuna siku nilipita mtaa wa posta dar kulikuwa na duka walikuwa wanauza iphone kipindi tu zimeingia sokoni..niliingia na kuuliza bei nilishangaa mwuzaji alivyoniangalia sijuhi alijua sina pesa ya kuinunua au alikuwa amegombana na mwajiri wake alikuwa anajivutavuta tu kama amelazimishwa kukaa pale dukani,lakini baada ya kutembelea maduka mengine nikagundua kuwa bado tunapaswa kujifunza sana ktk customer service..majibu ya mwuza duka kuwa sina chenji ni kitu cha kawaida sana...maofisini tatizo ni lilelile ikifika saa 5 asubuhi hakuna mtu maofisini..oooh bosi yupo lunch au meeting ndio majibu ya kawaida kutoka kwa ma secretary wao...nenda bandarini utajuta kwanini umeagiza mzigo kuutoa itachukua mda mwingi sana ooh system ipo down ni majibu ya kawaida kila siku !!!mtoa huduma iwe dukani au ofisini anaangalia vitu vidogovidogo ili akuchangamkie..umevaaje ??umeshika simu gani ??umeshuka na gari gani nk...banks zetu pia tatizo ni lilelile foleni kubwa tellers wawili tu wengine lunch!!!!makampuni ya utumaji mizigo (parcels) tatizo ni lilelile mzigo wa mteja umefika contacts zake zipo lakini hawawezi mpigia simu mteja kumwambia mzigo wako huu hapa..kampuni kubwa kama dhl walipaswa wampelekee mteja mzigo wake mpaka nyumbani(ndivyo wanavyofanya nchi nyingine)lakini kwetu ata kukupigia simu na kukwambia mzigo wako umefika njoo uchukue ni tatizo...mahospitalini napo yaleyale ...daktari hayupo msubiri kidogo saa mbili asubuhi!!!!!dr remmy ongala aliimba saa mbili asubuhi foleni kwenye supu ofisi ipo na nani?????wanatoa biz card wakipigiwa simu hawapokei!!!nenda kwenye baa wahudumu kama hawajakuona vile!!t ubadirike jamani..nakumbuka niliwahi kupata tatizo wakati nasoma mkwawa iringa nilikuwa nakwenda wizara ya elimu kila siku ili nimwone mheshimiwa kipindi kile kapuya ilichukua mwezi kumwona lakini nashukuru alitatua tatizo ndani ya dk 5 tu....kwa wenzetu ule usemi mteja ni mfalme ni mfalme kwelikweli..ukiingia dukani au ofisi ya mtu atafanya juhudi zote ili kesho urudi tena...+971504374387 dubai
source: lucky sabasaba jf member
pa unganisha na comments za mdau wangu wa karibuCHASHA also jf member
Mkuu huu ndo Ugonjwa wa Watanzania, na that is why Makampuni ya Nje yanakuja na wafanya kazi wao kabisa, sababu kuu ni hiyo hapo, Na tatizo kubwa ni ajila za kujuana, Unakuta Secreatary ana undugu na Mkurugenzi, usitarajie kabisa kazi kufanyika hapo,

Na ndo maana baadhi ya makampuni/Mashirika wakisha gundua kwamba katika wafanya kazi wao kuna wenye uhusiano wa Kimapenzi, hapo inabidi nyie wenye uhusiana mchague ni nani kati yenu aache kazi na msipofikia mwafaka wote mnapigwa Chini, na hii ni ili kuweka Uwajibikaji,

Kwenye Maduka mengi utakuta walioko kule ni Mala mke wa mwenyenmali, Mara shemiji yake, mara mtoto wa Dada sijui wifi, so hakuna kinacho fanyika ni story watu unahudumiwa huku anaye kuhudumia akiwa ameweka airphone masikioni, au anasoma gazeti, some time utakuta wanasukana au anakuhudumia huku anacheza na batan za simu, kwa Wenzetu kitendo kama hicho kina weza kulisabibishia Kampuni matatizo makubwa kabisa na ni balaa kwa kampuni ila huku kwetu hayo ni mambo ya kawaida kabisa,

Maofisi watu ni story za Ligi ya Uingereza, Ukiingia kutaka Huduma wanakuona kana kwamba umeenda kuomba kazi pale,

Mimi some time huwa naunga mkono wawekezxaji kuja na wafanya kazi wao make kwa Tanzania ni Vigumu kabisa, unamfuta Secreatary anajishedua utazani unamtongoza,

Nakumbuka kuna Mgahawa mmoja huku Arusha tuliwahi kwenda ila kabla ya kuingia tu kuna mdada akaja Mlangoni na kutuuliza kama tutaweza bei ya humom ikabidi tumuulize kwani sisi ni Vichaa? Je wewe unamtambua vipi mtu mwenye pesa? ni mpaka aje na Gari? Jamaa angu alishikwa na hasira lakini ni kamsii ttuingie na tukaagiza na ikabdi hata Chenji tuwaachie make hawajui walitendalo


Categories:

Leave a Reply