IDEA
ya Biashara ni moja ya mambo yanayo waumiza watu wengi sana, Na mara
nyingi wazo la biashara linahitaji utafiti wa kina ili kuja na wazo
lenye tija kwako na kwa jamii nzima,
HIZI NI MOJA YA NJIA ZA KUPATA WAZO LA BIASHARA
1. TUMIA UJUZI ULIONAO
Ujuzi ulionao
ndo sehemu ya kwanza kabisa ya kupata wazo la Biashara, Mfano kama wewe
umejiliwa na ni Fundi wa kushona Nguo, why usianze na wewe kuwa na
biashara ya aina hiyo? Kama wewe ni fundi magari why usianzishe gereji
yako?
Ujuzi ulianao ndo
hazina ya kwanza nay a kipekee ya kupata wazo na mara nyingi
wajasirimali wengi waliofanikiwa waliacha kazi wanazo fanya na kwenda
kuanzisha za aina hiyo na kuzimiliki wenyewe
2. BADILISHA HOBY YAKO KUWA PESA
Hobby ni moja
ya maeneo ambayo watu huja kutajilikia, kama wewe hobby yako ni kufuga
mbwa kwa nini usianze hiyo biashara ya kufuga mbwa?
Kama Hobby yako ni Kuogelea, kwa nini usinzishe mabwawa ya kuogelea na wengine wakawa wankuja huko kuogelea?
Kam unapenda gardening unaweza anza biashara ya kufanya landscape gardening
3. NUNUA BIASHARA AMBAYO TIYALI IPO
Ukishindwa
kabisa kupa wazo mwanana unaweza nunua biashara ya mtu mwingine na
kuindeleza, siku hizu kuna biashara kibao zinauzwa kwa sababu mbalimbali
so unaweza nunua nu kuendelea nayo
4. Kununua Franchise
Hii ni moja
ya njiza zinazo tumika kwa sasa na sehemu nyingi sana, Unaweza nunua
Popular Brand na kuifanyia kazi, Ingawa mara nyingi kuna mashariti ya
kuambatana ikiwemo kuhakikisha unatoa huduma sawa na Brandi yenyewe, nah
ii ni popular sana katika MAHOTELI/MIGAHAWA, MASUPERMARKET NA MADUKA
MENGINE
Na usijalibu kutumia Brand ya Kampuni Fulani bila kuwapa Taarifa make inaweza kula kwako na ukajikuta unafilisiwa,
Na ilisha wahi
kutokea kwa Kampuni ya Mabasi ya SABENA baada ya kutimia jina la Shirika
la Ndege la Ubeligiji, Ila sijui walimalizana vipi, make jamaa bado
wanalitumia
5. TUMIA PERSONALITY YAKO
Kuna watu
unakuta either ni Mrembo sana, Handsome na kazalika, unaweza utumia huo
urembo na uhendsaamu kufanya biashara, either za marketing na kazalika
.
6. NINI KINAKOSEKANA MTAANI?
Tazama ni
kitu gani hakipo hapo mtaani and then geuza kuwa opportunity, inaweza
isiwe ni mtaani ikawa ni kazini kwako, Kijijini kwenum au maeneo unayo
enda kustalehe
-Ni kitu gani huwa kinaleta usumbufu kwako na kukuchukulia muda mwingi na pesa nyingi?
- Ni huduma zipi hazipo kabisa mtaani kwako? Na ambazo ni za muhimu?
-Ni bidhaa zipi ambazo ni vigumu kuzipata mtaani kwenu?
-Ni kitu gani, wewe, Ndugu, Majirini huwa wanakilalamikia sana mtaani hapo?
7. UTALII KATIKA MAENEO YAKO
Hii nayo ni moja ya wazo, so unaweza angalia furusa za utalii kwenye maeneo uliyopo au hata kwingine na kuyafanyia kazi.
8. TUMIA TECHINOLOGIA MPYA KUANZISHA BIASHARA
Angalia mfumo
wa maisha wa sasa ulivyo, vitu vinavyo tumika kwa sasa na vinavyo
tumiwa na watu wengi, so mfumo wa maisha wa watu kwa sasa unaweza
kukuongoza kuja na wazo la Biashara
9. ANGALIA MAKAMPUNI MAKUBWA NA TAASISI ZINGINE WANAHITAJI NINI
Unaweza tumia
uwepo wa makampuni Fulani au taasisi Fulani maeneo yako kutengeneza
wazo la biashara, taasisi kama Shule, vyuo, Hospitali, Makampuni kama
Viwanda Migodi na kazalika, angalia ni kipi hawa watu wanaweza kuwa
wanahitaji kwa wingi
10. UNAWEZA KUANGALIA KUHUSU KUUZA BIDHAA ZA WENGINE
Unaweza ukawa unauza bidhaa za watu wengine, unachukua na kuuza
11. ANAGALIA NEWS NA MAKALA MBALIMBALI
Kunachaneli
huwa zina makala mazuri sana ya kiuchumi na biashara, hata TBC huwa
inamakala Fulani nzuri sana, na kuna chaneli za kimataifa siku huzi kazi
yao ni hiyo tu, ni kuonyesja ubunifu wa wajasirimali, so TV, radio na
magazeti yanaweza toa mchango w akutosha kwa wewe kupata wazo la
biashara
12. CPY BUSINESS AIDEA AMBAYO IMEFANIKIWA KWINGINEKO
Hii ni moja
ya njia zinazo tumika kwa sasa, unaweza copya aidea kutoka hata India,
China, na kwingineko na ukaja kuifanyia kazi huku kwa kufanya
marekebisho madogo kulingana na mahitaji ya eneo husika
13. TUMIA NJIZA ZOTE ZA KIUTAFITI KUPATA WAZO LA biashara- maonyesho ya biashara
-Magazeti,
- Kwenye taasisi za uma zinazo husika na biashara
-Kwa marafiki
14. UNAWEZA GUNDUA KITU?Unaweza
ukaja na ugunduzi wako kama walivyo fanya wakina Thomas Edson Michael
Dell na wengineo, na ikawa ndo mwanzo wa mafanikoa kwako
SO HIZO NI MOJA YA NJIA ZA KUTUMIA, INGAWA BADO KUNA NJIA NYINGI TU ZA KUFANYA ILI KUOATA WAZO LA BIASHARA LILILO BORA
by CHASHA friend of mine jf member
Categories: