Kuna watu wengi sana wanaolalamika kushindwa kuanza kufanya biashara kwa madai kwamba hawana mitaji. Ukweli ni kwamba kwa walio wengi madai ya kutokuwa na mtaji siyo ya kweli badala yake ukweli ni ukosefu wa elimu ya ujasiria mali.

Mfanya biashara Reginald Mengi aliwahi kusema, nami nakubaliana naye kwamba, kama mtu hawezi kufanya biashara kwa kutumia laki 1 na kufanikiwa hata akipwe mtaji wa Mil 100 hawezi kuibadilisha kuwa milion 150 - Haiwezekani kwa sababu Kanuni zinafanana.

Utakuta mtu ni mwl, anataka mtaji, wakati mtaji ni sebule ya nyumbani kwake na wanafunzi watatu hadi 5 wa kuanzia.
Niliwahi kumwuliza rafiki yangu hivi ukipata mtaji wo wote unaotaka wewe ungefanya nini? Akaniambia yafuatayo.
Nitanunua kiwanja kikubwa na kujenga shule kubwa ya sekondary yenye kila kitu - yaani madarasa, mabweni, walimu, maabara, vitabu vyote, viwanja nk - yaani kila kitu. Kisha nitatangaza kwa nguvu ktk vyombo vya habari.

Ukweli ni kwamba huyu rafiki yangu atafeli kwa uhakika kwa sababu, mimi siwezi kumpeleka mwanangu kwenye shule ambayo sijui historia yake hata kama ni kubwa namna gani - it is too risky. Lazima uanze chini kidogo kidogo ili ujenge jina zuri ( reputation). Huyu rafiki yangu, lazima angekwama kulipa mkopo. Kama atafanikiwa ni baada ya muda mrefu. Hapo lazima atakuwa ameshagombana na mwenye pesa - benki.

Shule nyingi ninazofahamu mimi hapa mjini zenye majina makubwa hakuna iliyoanza na wanafunzi 100 au zaidi kama alivyotaka rafiki yangu. Wengi wameanza na watoto chini 10 mfano Esacs, kamene nk.

Ndugu zangu, tujifunze kuanza chini na kupanda juu taratibu. Tusitake makubwa kuliko uwezo wetu. Biashara iko kichwani kwanza kabla haijwa halisi ktk hali halisi.

Biashara NI lazima ianze na kila unachokijua wewe ama una uzoefu nacho na kukipenda. Siyo kile ulichoambiwa kinalipa - hapana. kila Kitu kinalipa, hata kuimba au kuigiza kunalipa. Hoja ni kwamba je, unajua,unazoefu, unapenda na una uwezo kuimba au kuigiza? Na kwa kawaida ukishazingatia hilo, mtaji hauwi tatizo kama ilivyo tatizo kwa wengi sasa. Tatizo la wengi ni ufahamu.

Utakuta mwanasheria anatafuta mtaji wa kufungua ofisi ya huduma YA kisheria Ubungo Plaza - Haiwezekani. Ukimwuliza nani wateja wako wa kukuwezesha kulipa kodi na gharama zingine, Hana jibu. Kumbe alipaswa kuanza kutoa huduma hiyo kuanzia sebulen kwake then ofisi ndogo 80,000 mitaani, kabla ya ubungo Plaza.

Utakuta mtu anataka kwenda china kuchukua mzigo wa mil 50, kabla hajafanya biashara hiyo hiyo hapa bongo na kupata uzoefu kidogo kwa mtaji wa milioni moja au laki 1.

Hoja yangu si kwamba mtaji siyo tatizo la hasha, hoja yangu ni kwamba kwa walio wengi humu jf, tatizo ni ufahamu wa kutojua kitu cha kufanya kuliko tatizo la mtaji. Wapo wachache ambao kweli wana uzoefu na uwezo na wana matatizo la mtaji, lakini si wengi kama tunavyoona vilio vingi hapa JF- jukwaa la uchumi na kwinginepo mtaani. Tatizo la wengi ni ufahamu, agree or not.

Hivi unajua kwanini benki zinawanyima baadhi ya watu fedha na kuwapa wengine. Wanataka kujua kama una uzoefu na kama umeanza chini kuja juu au laa. Wengi hatuwaelewi watu wa benki lakini ukweli ni kwamba benki wana nia njema na sisi. Hataki kutupa pesa nyingi kuliko uwezo na uzoefu wetu wa kulipa. Wanajua kuliko sisi. kutunyima sisi mitaji tunayotaka ni kutusaidia kwamba tukaanzie chini kwanza. Kumbuka benki wapo ili kukopesha. Wanaokopa ndo faida, wanaoweka tu fedha siyo deal kwao. Ukiona wanatunyima maana yake tunakosa uzoefu, tunaka kuanzia juu kama rafiki hapo juu. which is wrong.

Nahitimisha kwa kusema tuwe tayari kuanza chini kidogo kwa faida yetu kwa sababu kanuni ya kubadilisha au kufanya biashara kwa mtaji wa mil 100 kuwa mil 150 ni sawa na kanuni ya kuanzia na laki 1 na kuibadisha kuwa laki 2 kibiashara.
Nawasilisha.

source: b Mikael P Aweda 
 http://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/384154-mtaji-siyo-tatizo-kwa-walio-wengi-tatizo-ni-sisi-wenyewe-kutojua-jinsi-ya-kuanza.html

picha kwa hisani ya : http://gillsant.tumblr.com/

Categories:

Leave a Reply