simu nyingi za juu ambazo zina specification za ukweli zinauzwa bei kubwa approximation ni millioni moja kwenda juu. mfano wa simu hizo ni kama nokia lumia 920, samsung galaxy s3, htc droid dna na iphone 5. lakini ukiangalia kwa makini unakuta vitu vingi vinavyofanya hizo simu ziuzwe bei kubwa havina maana kwa mazingira ya kiafrica.

mfano network ya 4g(lte), kustream hd(network yetu ipo slow), vitu kama gps hatutumii na mambo ya location, wengi wetu hatujali toleo la operating system kama ni android hata ikiwa 2.3 inatosha.

kutokana na mambo hayo nikaona niandae hii makala ya kuonyesha aina za simu ambazo kimuonekano ni kama simu za bei ya juu lakini zimenyimwa vitu flani ambavyo si muhimu kwa muafrica kuvikosa na hivyo kufanya bei ishuke. kwa kubase kwa ukubwa wa screen (zaidi ya 4.2 inch) na udogo wa bei (china ya laki 5)

kambi ya htc


hapa kuna simu moja tu

htc inspire 4g

kwanini ununue?


kwa sababu ina screen ukubwa 4.3 yenye resolution ya 480x800, ina gorrila touch screen inayofanya kioo kiwe kigumu kuvunjika. ukubwa wa screen umeizidi iphone 5 na imepitwa kidogo tu na samsung galaxy s3 pia inauwezo wa kuchukua semi hd video 720p na camera ya 8mp.

general perfomance


inakubali android hadi 2.3 gingerbread ikiwa na processor ya 1ghz na ram 786 na internal memory ya 4gb ikisuport memory card ya 32 gb (memory card ya 8gb inakuja na simu). kwa specification hizo zinaifanya hii simu kuwa fair, itarun smooth. pia ina speed hadi 14.4 mbps kwenye internet kwa standard ya 7.2 mbps kwa tanzania simu itakua very fast.

kambi ya samsung


tuwe wa kweli ni vigumu kupata samsung kwa bei rahisi nyingi zinauzwa bei kubwa sana hapa nimepata simu moja tu ambayo haina 3g.


samsung galaxy s wifi

nisiizungumzie sana maana haina 3g wala haitasuport function zozote za simu lakini hii inaweza kua mbadala wa ipod maana ina kioo kikubwa cha inch 5, na storage ya 16gb au 8gb so ni nzuri kuangalizia movies, videos , kuhifadhi picha, kuskilizia miziki na kuchezea games.

kambi ya kaka lenovo


lenovo a800

huyu jamaa lenovo anakuja juu sana mwaka jana ilikua ndo kampuni iliouza sana computer na kwenye simu akampita nokia na samsung kwenye soko la china. hapa anakuja na simu yake a800, ikiwa na screen ya 480x800 kwenye kioo cha 4.5 inch na ram ya 512mb pamoja na processor 1.2 ghz dual core na operating system ya ice cream sandwitch inaifanya hii simu kuonekana bora zaidi.


bei pia sio mbaya sana kwa simu hii maana ni chini ya laki 4

kambi ya micromax


micromax a110

wengi labda mtakua wageni wa hii kampuni lakini ni kampuni ya kihindi ambayo inatengeneza simu cheap sana za android na hii a110 ina screen 5inch ukubwa kama galaxy note ikiwa na resolution ya 480x800 na ram ya 512 mb. processor ni 1ghz dualcore na internal memory ni 4gb. hii nayo bei ni chini ya laki 4.

kambi ya ACER


acer liquid gallant e350

hii ndo simu ya MWISHO ikiwa na screen ya 4.3 ina internal 4gb ram 1gb na proccessor 1ghz. resolution kidogo kubwa ina 540x960
kwa hisani ya my bast friend  Cheaf kwawa jf member

Categories:

Leave a Reply