Leo tutakwenda kuangalia jinsi unavyoweza kuonyesha zawadi ya upendo kwa watu, hata kama huna fedha.
Kila mtu anapenda kupendwa, yakupasa kuwa na rafiki wa karibu atakayekushirikisha katika mambo mbalimbali unayokabiliana nayo.
Hivyo
ni vema kuwa na rafiki mzuri na kuonyesha upendo wako kwake, kwa sababu
wakati mwingine unajikuta hata familia yako inakuwa mbali nawe, hivyo
kipindi hicho unakuwa unahitaji mtu wa kuongea naye.
Pia ni muhimu
kuwa rafiki mzuri kwa sababu unajifunza ni jinsi gani ya kukutana na
watu wapya na unajifunza kutokana na makosa yako.
Tafuta watu ambao unapenda wawe rafiki zako, kwa kujitambulisha, kumwacha mtu mwingine kukueleza juu ya mambo anayoyapendelea.
Mwonyeshe
mtu huyo kuwa unamwamini, mwache ajue kuwa ni sawa kupendana, mwache
ajue kuwa uko pale kwa ajili yake na atakuwa rafiki yako wa kudumu.
Mara zote mfanye atabasamu hata kama ana huzuni. Pia mwache ajue kuwa upo tayari kusikiliza chochote atakachosema.
Je?
Unawezaje kuonyesha upendo bila kutumia fedha? Wakati mwingine
tunajitahidi kwa bidii kutafuta zawadi ambayo ni sahihi tunayofikiria
kuwa ina maana kwa yule unayempelekea.
Au, tunaishikilia zawadi hiyo,
tukifikiria kama kuna sababu maalumu ya kutoa zawadi hiyo. Ninakutia
moyo kutoa zawadi yako kwa uhuru na iwe ni mara kwa mara, kumbuka kuwa
utoaji ni shughuli ambayo inamnufaisha mtu kila mara anapofanya hivyo.
Tuangalie
zawadi 10 ambazo zinafaa kwa siku ya kawaida na maalumu. Pia, ni zawadi
ambazo mtu yeyote anaweza kutoa kwa sababu halazimishwi ila ni kwa nia
ya kuleta ushirikiano.
Zawadi ya kwanza ni muda. Kumbuka kuutoa muda wako na kushirikiana na wenzako ni moja ya zawadi kubwa unayoweza kuitoa.
Kama
unatoa dakika 10 kwa kupiga hadithi na mtoto wako, kupata chakula cha
mchana na rafiki yako au kutumia muda wa mchana kwa shughuli za
nyumbani, shambani au nyinginezo, ukiwa na mume au mke wako, unakuwa
unajitolea nafsi yako na kujenga uhusiano mzuri kwa muda huo.
Zawadi
nyingine ni kukiri kwa uaminifu. Tumekuwa tukisikia watu wachache
wakisema kuwa wamepokea shukrani nyingi au pongezi nyingi.
Wote tunajisikia vizuri wakati tunapata taarifa nzuri na shukrani kwa vile tulivyo au tunayoyafanya.
Anza
kuzingatia kuimarika katika hilo na kutoa sifa nzuri kwa wengine na
kujenga tabia ya kukiri jambo zuri linalofanywa na wengine kwa kile
unachokiona.
Nyingine ni Msamaha. Hii ni zawadi nzuri mno yenye
nguvu. Wakati tunasamehe wengine, tunaacha kuwaadhibu. Tunawaruhusu ili
wajisikie hatia au kuona aibu ili waweze kugundua makosa yao.
Msamaha
pia ni zawadi ya kutuweka huru kutoka kwenye uzoefu ulioupata wakati
ulipoumizwa moyo wako au maumivu katika matukio yaliyopita.
Vile vile
upendo. Wakati unapotaka kuuonyesha upendo wako kwa wengine,
usiwahukumu wengine, na uwaone kama ni watu wa muhimu kwako, watakatifu
na wa thamani, hiyo ni zawadi kubwa.
Tunaposhiriki kwa uwazi upendo
wetu na wengine inasaidia kuponya majeraha, kujenga uhusiano mzuri na
kumsaidia mtu katika kupitia changamoto za maisha pia kuwa na maisha
mapya ya uhakika.
Usiugawe usikivu wako. Ingawa tunatoa muda wetu kwa ajili ya wengine, akili zetu zinaweza kuwa popote kutokana na uzoefu.
Jiruhusu
nafsi yako kuwa kwa mtu mwingine, kupanga naye shughuli nyingine,
mawazo au ajenda mpaka utakapofikia malengo yako uliyokusudia.
Kama
utafanya hivyo, watu watakuona unastahili kupata asilimia zote, kwa
usikivu wako na kwa upande mwingine inawezekana ukawa hujafikia kiwango
hicho ila kutokana na hali hiyo uliyojiwekea kwa watu.
Heshima. Mara
kwa mara tunakuwa na shughuli nyingi au tunajishughulisha sana katika
maisha yetu ambayo yamekuwa na matukio mfululizo ya kuvutia ambapo
tunasahau kama kuna watu wengine wanaotuzunguka. Iache nafsi yako ipumue
na kutoa heshima kwa watu ambao unakutana nao kila siku.
Yapo mambo
madogo madogo ambayo yanaweza kufungua milango kwa watu wengine
kuthamini mambo ambayo unawafanyia kama kumpa lifti kwenye gari yako,
kumbebea gazeti lake mpaka mlangoni pake au kusimamisha gari lako mbele
ya mtu unayemfahamu na kumpa lifti kipindi cha msongamano wa abiria
kituoni.
Mambo yote hayo yataonyesha hali ya kujali kwa mtu ingawa wakati mwingine mtu hawezi kuelewa wema wako na kukushukuru.
Shtukiza.
Zawadi za aina hii zinamfanya mtu kuwa mbunifu wa hali ya juu. Je,
unataka kumpa dada yako kadi ambayo inasema unampenda? Unajisikiaje
unapomtumia mumeo maua?
Je, ni kweli utamshtusha? Au labda umechagua
kujitolea kumpa mfanyakazi mwenzako kigari cha kusukuma cha watoto ili
aweze kufurahia jioni anapokuwa matembezi na rafiki zake?
Zawadi kama
hizo zinakuwa tukio kubwa kwa yule unayempelekea katika siku yake ya
kawaida kwa sababu hakutarajia kufanyiwa jambo kama hilo kwa siku hiyo.
Shukrani
ni zawadi pekee kwa yule unayempa, kwani inasababisha mtu huyo kujua
kuwa umekuwa makini kwa lile alilokufanyia. Kama ukiri wa dhati, na neno
jingine ni kusema asante, linaonekana ni jambo ambalo si la kawaida.
Endapo utachagua kusema au kuandika shukrani zako, hii ni zawadi ambayo inakwenda ndani ya moyo wa mpewa shukrani.
Tabasamu
katika dunia ya kisasa, mara nyingi tunaona tabasamu chache na nyuso
zenye furaha ya kweli. Kinyume cha mwelekeo kwa kujivisha tabasamu kama
sehemu yako ya kila siku.
Tabasamu linajulisha moyo mkunjufu,
mapokezi na urafiki. Pia inafanya kuonekana kwa urahisi kwa wote wenye
nyuso za tabasamu. Iache zawadi hii ya tabasamu itoe ujumbe. Mfano “Nina
furaha uko hapa”.
Maombi ya kimya kimya. Wote tunakuwa na maombi ya
ziada na ya baraka katika maisha yetu. Hata kama hufahamu, mtu mwingine
anaweza kukubariki wakati unampa zawadi ya maombi yenye nguvu.
Kama
unajua au la, mazingira ya mtu au dini yake, unaweza kuuliza kwa msaada
au usikivu. Maombi rahisi unaweza kumwombea kwa kutumia “Mungu/Allah,
ninakuomba umbariki mtu huyu na ukutane na mahitaji yake yoyote ambayo
anayo katika maisha yake, asante”.
soursce:blog ya maisha yetu
Categories: