Jinsi ya kupata wasomaji wa kudumu
Leo nilikua nasikiliza marketing radio moja hapa nikakuta kipindi chao
kilikua kizuri sana hivyo niliyoyasikia huko naona sio vibaya kama
nitashare na wengine humu labda moja au mawili yatakusaidia.
Topic yao ilikua inazungumzia jinsi ya kupata wasomaji wa kudumu.
Walikua wanasema watu wengi wenye websites au blogs ambazo haziuzi kitu
chochote (information) hawafahamu kuwa wasomaji wa blogs au websites
zao ndio wateja wao. Wengi wanajitahidi kupost kila siku lakini hawajui
bila msomaji wa kusoma basi wanayoyaweka huko ni bure tu.
Sasa wakasema kama una blog au website na umeshaweka post kadhaa na
wasomaji wachache wameshaanza kupitia blog yako kuna mambo mengi ya
kuzingatia na kufanya ili wasomaji wako wawe wanahamu ya kusoma
blog/website yako kila mara na hata kuwaambia watu wengine kuhusu blog
yako..
1. Quality
Hili nadhani kila mtu anafahamu kama unaweka vitu visivyo na quality
kwenye blog yako ni kama unawadharau wasomaji wako hivyo ni heri upost
vitu vichache vyenye quality nzuri kwa week kuliko kupost vitu vingi
visivyo na quality.
2. Unique
Na hili pia wengi tunaelewa kama blog au post zako sio unique basi ujue chance ya mtu kustumble kwenye blog yako halafu arudi tena au akubookmark ni next to none. Hivyo uniqueness ni muhimu...
3. Respect
2. Unique
Na hili pia wengi tunaelewa kama blog au post zako sio unique basi ujue chance ya mtu kustumble kwenye blog yako halafu arudi tena au akubookmark ni next to none. Hivyo uniqueness ni muhimu...
3. Respect
Hata kama huwasiliani na wasomaji wako in a personal level ni muhimu
sana kuonyesha kuwa unawaheshimu. Onyesha heshima kwa kusikiliza maoni
yao, kujibu maswali yao kama wanafanya hivyo na pia kuweka vitu ambavyo
hata wewe ungependa kusoma kama ungekua msomaji. Na kama wasomaji wako
hawatoi maoni au kuuliza maswali yeyote basi tone ya post zako
zionyeshe heshima na sio kiburi na kejeli. Kumbuka wasomaji wako ndio
wanakuweka hapo sasa kama huwaheshimu utajikuta huna mtu wa kusoma blog
yako.
4. Write what they want to read
Kama watu wameishaijua blog yako na wanajua wewe blog yako inazungumzia
mambo gani sana basi stick to that..eg sports, politics, beauty,
fashion, family, women, children etc Sio leo uzungumzie michezo kesho
urudi kwenye siasa, kesho kutwa upo kwenye fashion etc etc na kama blog
yako sio ya breaking news basi jitahidi uweke news za aina moja tu..Sio
kukopy na kupaste kila news unayoiona kwenye blog nyingine.
5. Be professional
Kama una blog inazungumzia kitu fulani basi act like a pro in that
topic. Kama hujui research. Ili ukiulizwa swali upate kulijibu. Na pia
be professional katika blog template yako au website yako. Ukiweka vitu
color au gadgets za kitoto basi watu watakuchukulia hivyo hivyo. Sasa
punguza clutters, mavitu mengi na templates yenye rangi rangi nyingi
itawakimbiza wasomaji wako. Wanasema jitahidi sana background yako iwe
solid color (1st choice). Kumbuka kila unachopost kwenye blog yako
kinakurepresent wewe.
5. Multiple platforms
Wanasema kila mtu ni tofauti na kila mtu anaprocess information kwa
njia tofauti sasa kwa vile siku hizi kuna platform nyingi za kupeleka
habari basi usiache kuzitumia. Wamesema kwa mfano kwenye site unapopost
kitu fulani basi kama hiyo post ina picha tumia Instagram kuweka picha
ya hiyo topic huko halafu link hiyo picha kwenye hiyo post yako kwenye
blog..Wanasema kuna watu wanaelewa habari zaidi kwa kuangalia picha.
Hivyo wakiona picha kama inawavutia watataka kusoma zaidi basi wataenda
kwenye blog au website yako. Lakini alisema hakikisha link unayopost
kwenye hiyo picture ni ya hiyo post na sio ya blog yako yote in
general. Wengi wanakosema na kulink blog yao as a whole na mtu akifuata
ile link akakuta kitu kingine kinamkaribisha basi hatakua na hamu ya
kusoma blog yako tena bali akikuta hiyo topic aliyoifuata kwa kutumia
ile link basi akipendezwa nayo atajikuta anasoma post zingine ulizonazo
katika blog au site yako. Hivyo akasema katika topic moja unayopost
tumia Instagram, halafu kama una uwezo wa kurecord basi soma hivyo
habari hata kwa ufupi uiweke kwenye podcast au blogradio na huko nako
pia link your blog.
6. Easy to navigate
Amesema kuna watu wengine wana website au blog lakini wanafanya iwe
ngumu kwa wasomaji wao kuweza kuona post za nyuma au hata mambo
mengine. Amesema ili watu wapende kuja kusoma kila siku hakikisha blog
au website yako iko easy kunavigate around.
7. Give credit when it's due
Amesema ukitaka watu wakuheshimu na kukuamini basi toa heshima kwa watu
unaotumia info au picha zao. Amesema watu wengine wanafikiri wasomaji
ni wajinga kuwa kile wanachoweka basi kama wamekitoa mahali pengine
hakuna mtu atakayejua. Sasa amesema kama umetoa picha mahai fulani
usijifanye ni yako wewe original weka heshima. Kama umetoa habari
mahali fulani basi link hiyo sehemu ulipoitoa. Na kama umeiandika hiyo
habari in brief basi weka link ya mahali unayojua wakienda huko
watapata habari yote kwa kirefu zaidi. Hiyo itawaongezea wasomaji
uaminifu kwako na pia kuwarahisishia kama kitu hawajaelewa wataenda
kwenye hiyo link na kupata habari zaidi. Pia faida ya kuweka link na
credit za mahali unapotoa habari zako ni kuwa kama watu wakigoogle ile
blog au site uliotoa information pia na ya kwako itapop up kwenye list
na the more blog yako inakuwa searchable mara nyingi the more inapanda
juu katika search. Hivyo hata siku kama umepost habari ambayo watu
wengi pia wamepost lakini watu wakigoogle blog yako itakua juu kwa
habari hiyo. Na la muhimu wengi watakua wanatumia blog yako kwa kujua
kuwa ni unapata mambo memgi ya muhimu na unawalink kwenye habari
nyingine zaidi zamuhimu na utaonekana uko pro.
Watu wanachokosea
1. Alichochosema watu wanakosea na kujipunguzia wasomaji bila kufahamu
ni kuwa mtu anaweza kuwa na blogspot, wordpress na tumblr sasa anapost
habari hiyo hiyo kwenye sehemu zote hizo na kufikiria kuwa watu wengi
wataona na kusoma. Amesema hiyo ni kupoteza nguvu kwa vile watu
wanaopenda kusoma na kujua habari zako ni nzuri watakufuata tu hata
ukiwa na mahali pamoja tu. Na kama unataka habari yaku iwe juu mapema
kwenye search engine basi iweke mahali pamoja tu. Blog yako ikiwa watu
wanaingia mara kwa mara katika kila wanachosearch basi itajikuta inakua
juu tu lakini zikiwa tatu nne zenye habari hiyo hiyo basi zingine
hazitaonekana bali ile moja yenye watu wanayoingia mara kwa mara. Hivyo
kuweka kwenye platform nyingine zenye muundo mmoja ni kupotea muda tu
na kupoteza wasomaji.
2. Kingine wamesema kama unatumia social network kama Twitter, Facebook
au G+ set platform moja tu iwe inatweet kwa wakati mmoja. Au kama
unataka ziwe zinatweet zote basi set kwa muda tofauti. Ukiwapata watu
wa nchi mbalimbali kwa masaa yao. Mfano kama unataka watu walioko
Marekani, Africa na Asia wasome habari yako asubuhi basi set hizo ziwe
zinapost kwa wakati tofauti lakini usije ukatumia mfano blogspot,
instagram, facebook, podcast, tumblr kupost habari hiyo hiyo kwa mara
moja kwenye twitter au kama unashare kwenye G+ ...Amesema ukifanya
hivyo watu watakuchoka na hata hawatasoma habari zako tena. Kama ni
habari hiyo hiyo share kwenye twitter kwa masaa tofauti na kama ni G+
share zile za maana tu zingine watakuja kuzifuata wenyewe huko. Sio
kila kitu unashare. Share vichache vilivyo interesting halafu watu
watajikuta wanaenda kuangalia nini tena unacho huko kwenye blog yako.
Kama unafahamu lingine ambalo sijaliweka hapa feel free kuchangia kwenye comment hii yote ni kujaribu kutafuta njia ya kuboresha blog zetu za watanzania popote pale walipo..
http://www.tanzanianblogawards.com/2012/07/jinsi-ya-kupata-wasomaji-wa-kudumu.html
Categories: