http://25.media.tumblr.com/tumblr_md5b7i6cOw1r2d3v2o1_1280.jpg

Leo naanza kwa kuweka bayana hili, ifahamike dhahiri kuwa sina maana ya kutaka kuzuia au kushiriki katika kuhakikisha watu wananyimwa ajira na 'wajasiliamali wapya' bali ieleweke nia yangu ni kuwajuza waajili wapya namna ya watu wanaoweza kuwafaa katika biashara zao kuanzia hatua za mwanzo wa biashara zao.

Biashara inayoanza inafanana sana mtoto mdogo anayehitaji uangalizi mkubwa sana,kwa mtoto wazazi ujitahidi sana kumwangalia mtoto kwa umakini na ukaribu sana...kwa upande wa biashara zinazoanza,kwa hapa kwetu Tanzania nimebaini kwa kutumia utafiti usiyo rasmi kuwa wenye biashara wengi ni wale walioajiriwa sehemu nyingine,yaani wanaichukulia biashara kama kipato B katika maisha yao.

Wale wanaochukulia biashara zao kama Kipato B wanakawaida ya kufanya maamuzi ya watu wanaowaajili bila kuzingatia mambo mengi,si wao tu hata wale ambao wanategemea biashara zao kama chanzo kikuu cha mapato wanapaswa kufahamu mambo kadha wa kadha kuhusu watu wakuajiri.

Wajasiliamali wanatakiwa kufahamu kuwa si kila mtu anastahili kuajiliwa katika nafasi fulani,watu wenye vitu vifuatavyo wanafaa sana kuajiliwa na wajasiliamali:

  • Mtu anayejiamini,mwenye uwezo wa kuchukua maamuzi haraka
  • Mtu mwenye kuwa na hali ya ujasiliamali (Entrepreneurship Spirit)
  • Anayeweza kuvaa uhusika wa mteja
  • Kuwa tayari kujitoa zaidi kwa mteja hata kuzidisha muda wake wa kazi
  • Mtu mwenye kujali na kufahamu kuwa biashara hiyo ndiyo ajira yake,ikikuwa naye atakuwa kiuchumi
  • Awe mtu mbunifu na mwenye uwezo wa kuziona fursa nyingine
  • Awe mtu kuweza ku'interact na watu' na mwenye kuelewa kuwa wateja wanatofautiana
  • Awe na tabia ya kutoa mrejesho wa vitu
  • Awe 'mbaili' (Natural Economist)
  • Awe mwenye kuweza kutimiza ahadi zake



Watu wenyesifa za namna hii ni watu wanaofaa sana kuajiliwa na wajasiliamali kwakuwa wanaweza kuikuza biashara. Ingawa ifahamike dhahiri watu wa namna hii ni changamoto sana kuwa 'retain' katika biashara kwa kuwa wanaonana na watu wengi ambao upenda ufanyaji kazi wao na uwaahidi maisha bora kuliko hata yale ambayo sisi tuliwahi kuahidiwa hivyo yatakiwa kubuni namna ya kuweza kuwa 'retain' katika biashara vinginevyo wawezakujikuta unakuwa 'stepping stone' ya wengine

Biashara iliyokuwa iliyokuwa,imekuzwa na watu na ile iliyodindoka imedondoshwa na watu, hivyo uamuzi wa mmiliki uweza kupelekea hali yoyote kati ya hizo mbili.

Tuondoe ile dhana ya kwamba 'nina mdogo wangu kamaliza form 4 ngoja anisaidie' anagalie asijekukusaidia kuiua biashara kwa kuweka Bora mtu na si mtu bora katika biashara yako.

Mambo ni mengi na wakati umeisha,yanipasa niendelee na majukumu mengineyo.

Naomba kuwasilisha,

Majadiliano,ushauri na mikakati: kkmarketing61@yahoo.com

Categories:

Leave a Reply