Saikolojia na maisha Hapa najaribu kukuchambulia baadhi ya tabia zetu ambazo wengi huzifanya pasipo kuyajua madhara yake na kujikuta zikituharibia ama kuua ubongo au maini ambazo ni sehemu muhimu mwilini mwetu.

Miongoni mwa tabia zinazoweza kuharibu ubongo wako
1.Kutopata kifungua kinywa
Watu wenye tabia ya kutopata kifungua kinywa asubuhi wana hatari

ya kushusha kiwango chao cha sukari katika damu na hivyo kusababisha virutubisho viendavyo kwenye ubongo kupungua, hali hii husababisha ushindwe kufanya kazi.

2.Hasira na hamaki za muda mwingi
Watu wenye tabia hii husababisha pia mishipa ya ubongo kuzidiwa nguvu na hivyo kupunguza uwezo wao wa akili kufanya kazi ipasavyo.

3.Uvutaji wa sigara na vitu vingine vya moshi
Tabia hizi husababisha sehemu nyingi za ubongo kugandamana na hivyo kudumaa na kusababisha ugonjwa unaoitwa ‘Alzheimer’.

Kumbuka pia chembe za sumu ya moshi ziendazo kwenye ubongo baada ya kupita mapafuni huharibu mishipa midogo ya kumbukumbu na hivyo kumfanya mtumiaji awe na uwezo mdogo wa kukumbuka vitu na wakati mwingine kumbukumbu zake kufa kabisa.

4. Matumizi makubwa ya sukari
Matumizi makubwa ya vitu vya sukari huharibu mchakato wa protini ya mwili na virutubisho vingine kusambaa vema mwilini na hivyo kusababisha ukosefu mkubwa wa virutubisho vinavyokuza na kuuwezesha ubongo kufanya kazi.

5. Mazingira ya hewa iliyochafuliwa
Hii huhusisha mazingira machafu tuishiyo ambayo huathiri hewa tunayovuta. Uchafu huu wa hali ya hewa kupunguza kwa kiasi kikubwa kiwango cha hewa ya oksijeni katika hewa. Tukumbuke kuwa ubongo ndiyo mtumiaji mkubwa wa oksijeni, sasa tunapovuta hewa iliyochafuka tunapunguza kiwango cha hewa ya oksijeni iendayo kwenye ubongo na hivyo ukosefu wa hewa hii muhimu katika ubongo huathiri ufanyaji kazi wa ubongo wa mtu.

6. Tabia ya kukosa kulala vya kutosha
Usingizi huruhusu ubongo wetu kupumzika na hivyo kujirutubisha na kujipanga vyema. Kukosa usingizi kukizidi huuwa seli za kweye ubongo kwa kiasi kikubwa.

7.Tabia ya kulala tukiwa tumejifunika vichwa
Najua wengi wetu wakilala hupenda kujifunika gubigubi. Wengine ni mazoea tu na wengine ni kwa ajili ya hofu. Tunapolala vichwa vyetu vimefunikwa tunaongeza msongamano wa hewa chafu ya kabon dayoksaidi na kupunguza msongamano wa hewa safi ya oksijeni katika mazingira ya kichwa. Hewa hii chafu inapozidi maeneo ya kichwani huuwa uwezo wa ubongo.

8. Tabia ya kuufanyisha kazi na kuuchosha ubongo wakati tunaumwa
Wako watu wenyetabia ya kujilazimisha kuwaza au kufanya kazi wakati wanaumwa, watu hawa hawataki kupumzika hata kama mwili umekataa. Kufanya kazi sana au kusoma wakati unaumwa husababisha kupungua kwa ufanisi wa ubongo na hivyo kuharibu au kuua nguvu ya ubongo.

9. Kukosa mawazo yenye hamasa
Siyo vizuri kukaa tu bila kuwaza vitu vyenye maana, au kuzubaa kizembe zembe tu. Kufikiri ni njia nzuri sana ya kuuweka ubongo wetu kwenye mazoezi. Kwa kukosa kuuamsha ubongo wako kupitia kuwaza au kufikiri basi unasababisha ubongo kunyong’onyea na kuganda.

10.Tabia ya kuzungumza kupita kiasi
Wako watu ambao huongea kama vyerehani, wao hujifanya kila kitu wanakijua, kila sehemu wamekwenda, kila mtu wanamfahamu hamna hadithi wasiyoweza kuiongelea.

Categories:

Leave a Reply