Katika maisha haya tunayoishi,niliwahi kuambiwa mafaniko ni matokeo ya
utekelezaji wa mawazo na utumiaji wa fursa sahihi katika wakati
sahihi,yaani kwa ki ulaya "money follows great ideas", katika kupitia
magazeti ya 'kizungu' nikakutana na sentensi hii pia "The starting point
of all achievement is desire. Weak desire brings weak results" yenye
maana chanzo cha mafanikio ni ile hamu ya kufanikiwa,hamu hafifu uleta
matokeo hafifu,yawezekana tafsiri yangu isiwe sawa ila kwa jinsi ilivyo
hapa kwetu itakuwa imeeleweka
Kufanikiwa kibiashara katika ulimwengu wa sasa kuna maanisha uwepo wa
wazo lenye kuleta suluhisho kwa wengine yaani falsafa ya tatizo lako
kipato changu, uwepo wa wazo lenye kurahisisha kazi kwa wengine linaweza
kukuhakikishia kukuwa kwa biashara yako kwakuwa kunahakikisha uwepo wa
wateja wa uhakika
Uwezekano wa kuwapata wateja unafanya uhitaji wa biashara kusajiliwa
kwenye mamlaka mbalimbali ilikuweza kuwa na 'uhai wa kisheria' hapa
itategemeana na aina ya biashara ambayo mtu ameamua kuianzisha,uhai wa
kisheria unatoa fursa biashara kuwa huru kutafuta fursa sehemu yoyote
ile na hapa ndiyo hatua ya biashara inapoanza.
Kuanza kwa biashara hakumaanishi kufanikiwa katika soko husika; siri ya
kufanikiwa katika soko ni kufahamu aina ya wateja unaowataka na
uliowachagua,kufahamu upatikani wao na mahitaji yao;gharama ya wao
kupata huduma,namna unavyoweza kuwahudumia tofauti na wafanyabiashara
wengine,namna unavyoweza kuheshimu muda wao na jinsi unavyoweza kuwa
'flexible' katika huduma zako kulingana na aina ya mteja.
'Flexibility' inakuhakikishia wateja wa uhakika kwakuwa kila atakayekuja
anajua tatizo lake litapata ufumbuzi.Jukumu la kuitangaza biashara
linaweza kuwa dogo kwakuwa waliowahi kuwa wateja wako watakuwa mabalozi
wazuri na kukutengnezea 'customer network' ambayo ni muhimu kuliko
matangazo.
zipo namna nyingi za kufanikisha biashara, Kwa leo,naomba niishie hapa wanajamii.
maswali na majadiriano kkmarketing61@yahoo.com
BY Patrick Nkandi
CEO
KK Marketing and Foreign Trading Ltd,
Categories: