http://sphotos-f.ak.fbcdn.net/hphotos-ak-ash3/c67.0.403.403/p403x403/581446_438748409509728_1156507522_n.jpg


Ndugu mwana blog leo tumebahatika kuwaletea mahojiano na ndugu Geophrey Tenganamba ambaye ni
mkurugenzi mwanzilishi wa Perfect Path Innovators tuunganewote kama utakuwana maswali usisite kuuliza au kumuulizandugu yetu hapa nayeye ataujibu

1-Tafadhali tupe japo historia yako kwa ufupi?
Mimi ni Geophrey Tenganamba, mtoto wa tano katika familia ya Marehemu Mzee Antony Tenganamba, ni mzaliwa wa mkoa wa rukwa lakini kwa sasa makazi na biashara zangu zipo hapa Dar es salaam na morogoro. Nina Shahada ya Uhasibu na masoko niliyoipata kutoka  katika chuo kikuu Zanzibar,2009. Ni mshauri wa maisha au mwanamapinduzi wa maisha, biashara,mahusiano na uwekezaji. Ni mhasibu wa tume ya vyuo vikuu, mkurugenzi mwanzilishi wa Perfect Path Innovators inayotoa huduma na utalaamu wa biashara na masoko,computers  na mengineyo. Ni mhamasishaji mwenye kipawa kikubwa na nimefanikiwa kufanya semina na Erick Shigongo, Chriss Mauki,Felix Majangilla na wengine wengi. Ninapenda maisha ninapenda kuishi tofauti na kuonyesha tofauti.Ni mtunzi wa vitabu vikubwa hapa nchini na watu wanavinunua sana; kama “Kichwa Chako Ni Dhahabu ya utajiri”, the richest Goldmine in You na Nguvu ya kujitajirisha ndani yako. Vipo sokoni.

2-ni jambo gani ktk maisha unapenda kulifanya au unajutia kulifanya?
      Napenda kuishi, sana kuishi kwa malengo na kusababisha kitu kwa binadamu wanaonizunguka. Nimewahi kufanya makosa lakini kamwe sipendi kujuta, hakuna jambo ninalolijutia maishani.
3-hivi mafanikio ya kweli yanaweza kupatikana nje ya MUNGU?
Binadamu wote wapo ndani ya Mungu, ndani ya duara la Mungu, na hakuna mtoto wa shetani hapa duniani. Kila binadamu anaweza kufanikiwa, ila kufanikiwa kwa njia ipi na kwa matakwa ya nani ni muhimu. Na mafanikio ni kulingana najinsi mtu mhusika anavyoyachukulia, yeyote Yule ambaye anasema amefanikiwa lakini hajui amefanikiwa kwa matakwa ya nani hajafanikiwa bado, mafanikio ni pamoja na furaha ya moyo, tumaini la kufika huko tuendako na fedha za kukutosha na kuwasaidia wengine. Kila mmoja anaweza kufanikiwa lakini lazima achukue hatua kwanza.
4-kwa nini wasomi wengi wa hapa nchini wanapenda kuajiriwa kuliko kujiajiri?
    Wasomi wengi wanapenda kuajiriwa kwasababu ya mazoea waliyoyakuta, mara nyingi sana msomi akiamua kujiajiri huonekana kama anapotea. Ni aina ya uoga wa wasomi wengi, na uoga ndiyo mchawi mkuu wa mafanikio ya binadamu yeyote. Kuajiriwa ni raisi lakini matunda yake ni madogo au twaweza kuita ni makaburi ya vipawa na uwezo wa binadamu. Binadamu anayefikiri na kukumbana na mambo katika kujiajiri hufufua uwezo wa ndani yake na kuwa mkubwa hata kiakili. Hivyo ni uoga tu wa kuona makubwa. Nchi hii ina fursa nyingi sana kama wasomi wakiamua kujiajiri.
5-nini ushauri wako kwa wasomi wa hapa nchini kwetu?
Tanzania bado inahitaji binadamu wanaodiriki, wanaoamua maisha yao kwa mfumo wanaoamini wao hasa kwa kujiajiri. Ni muhimu sana kuwa na tabia ya kutaka makubwa ili upate makubwa; kwa mfano
“Mpaka lini utaendelea kuwa mtumishi wa wahindi kama punda wakati uwezo wa kuyatengeneza makubwa kama wao unao? Kwanza nchi ni ya kwako ni vema utumie fursa hiyo. Kuna siku tulikutana na MODESTA MAHIGA, aliniambia kuwa hakuna nchi raisi kujiajiri na kupata makubwa kama Tanzania, ukishaamua kuwa na ndoto yako na kung’ang’ania kuifikia.
6-nini siri ya mafanikio yako?
 Ni kuamua tu, yaani unaamua unachotaka na unahakikisha kinapatikana basi. Naomba wasome link hii katika blog yang kujua nini maana ya kuamua   http://treasurehousewithinyou.blogspot.com/2011/11/amua.html

7-Unajisikiaje pale unapofanya kitu na kukifanikisha?,na kama
haujakifanikisha unajisikiaje?
Najisikia  kufurahi, nauona uwezekano wa kuyafanya mengine zaidi. Kuhusu kutofanikisha, yakitokea hayo najiona kuwa nahitaji kuongeza mwendo zaidi.
8-Upi ushauri wako kwa mtu ambaye anafanya kitu na kushindwa kukifanikisha?
Hakuna binadamu aliyewahi kukuta vitu mteremko, lazima alijaribu akashindwa, akajaribu kwa njia nyingine akashindwa tena, lakini hakukata tama na mwisho wa siku akashinda. Huwezi kusema umeshinda wakati hakuna jasho ulilotoa. Maisha siyo rahisi, lakini yanawezekana kwa Yule asiyekubali matokeo na kuanza tena.
9-nasikia wewe ni mwandishi wa vitabu? kama ni kweli umeshaandika
kitbu kipi na kipi?
10- pia wewe ni Director and founder of Perfect Path Innovators,hii
inausika na nini hasa?
Inatoa ushauri wa biashara, masoko, uwekezaji na mengine mengi kama nilivyosema mwanzo kaka Godlisten
11- kama mtu akihiitaji kitabu chako anaweza kufuata utaratibu upi? ua
vinauzwa wapi?
 Vitabu nilivyotunga ni kama kichwa chako ni dhahabu ya utajiri, nguvu ya kujitajirisha ndani yako, the richest goldmine in you. Kwasasa vimeisha bookshop lakini tumeshaanza kuvisambaza tena. Lakini kwa anayehitaji, anaweza kupiga simu +255714477218, email:gtlivemore@gmail.com, ataletewa mahali popote alipo. Na kwa taarifa zaidi wapite katika blog hii:   http://treasurehousewithinyou.blogspot.com/search/label/SWAHILI%20INSPIRATIONS
Asante

asante ndugu Tenganamba kwa ushirikiano wako

Categories:

4 Responses so far.

  1. nice one i like this interview..

  2. kazi nzuri nimeipenda hii!!!

  3. Asanteni sana kwa kuonyesha ushirikiano blogger wa Wamtaani

  4. asante dada Yasinta.
    karibu tena hapa na nafikiri muda si mrefu utakuwa mwoja wao tunakusomakama hivi

Leave a Reply