Mawasiliano ni zaidi ya kuongea na pia ni kuhusu kiwango chako katika kusikiliza, kuelewa lafudhi mbalimbali za sauti na mfumo mzima wa lugha yako – yaani ni jinsi gani unavyocheza na lugha yak
o katika kuongea na kueleza.

Hivyo, yatupasa kukabili katika kufikia uelewa huu – kwakuwa mawasiliano ni jambo muhimu sana ndani ya ndoa zenye mafanikio. Mara nyingi mambo yanayosababisha hata kutokea kwa matatizo ndani ya ndoa zetu ni pamoja na matatizo ya ukata wa fedha, uwajibikaji ndani ya familia, na matukio mbalimbali ya watoto na familia kwa ujumla. Hali hizi zote uboreshwa katika kuzidi uharibifu hasa pale suala la mawasiliano linapokuwa pia ni tatizo kubwa, maana bila mawasiliano yaliyotandazwa kwa hekima na maarifa utashindwa kuwasili katika kufanya kazi ili kutatua matatizo kwa njia za kujenga kwakuwa nyinyi wanandoa hamuwasiliani vizuri kwa maana ya kule kuwasiliana kwa namna zinazodhihirisha uwepo wa upendo na amani.
Fahamu kuwa kuwasiliana vyema na kwa sahihi zake ni chachu iliyo njema katika kuimarisha mahusiano yenu na kwakweli huku pia ni aina mojawapo ya nyunyizo la mahaba kwa furaha zenu.
by  Simon TheDon my friend on facebook

Categories:

Leave a Reply