TEMINO-CLOUDS FM WITH ABELLA NA HARIS KAPIGA; 

"Dunia inahitaji wanadamu wanaoishi, wanaoamua maisha yao na kung’ang’ania mpaka mwisho, mpaka kieleweke"


  

TOPIC:Kamwe Usikate Tamaa, Endelea Kusonga Mbele
Maisha ni safari ya malengo yetu duniani. Na safari huanza pale unapojua kwanini unasafiri, unaenda wapi na kwa usafiri upi. Na katika safari ya malengo na ndoto zetu kuna mabonde, mawe na milima njiani. Wapo wale wanaokata tamaa kutokana na mabonde na milima ya maisha  na hupotezwa njiani na wapo wale ambao huendelea kupambana  bila kukata tamaa na watu hawa hula mema ya nchi, duniani. Maisha si kutuwama kama maji taka dimbwini kutokana na mabonde na miinuko njiani bali ni kutembea na kuendelea bila kukata tamaa.  

Mambo makubwa ya maisha yamefanywa na watu walioendelea kujaribu,kupigana hata katika mazingira ambayo hayana matumaini kwao.  Waswahili husema Kabla ya kukata tamaa katika maisha, jaribu tena.

Ili uweze kuishi kimafanikio katika maisha, CHAGUA cha kwako maishani yakabili maisha uso kwa uso; pambana na kila aina ya magumu na maumivu yake, jenga imani ndani yako; hasa imani ya wewe mwenyewe katika kile ukitakacho maishani. NA USIKATE TAMAA. Maisha ni magumu sawa, lakini hayawezi kuwa na nguvu kwa mwanadamu aliyeamua kuwa mgumu, anayepigana na kuendelea mbele pasipokukata tamaa.  Kumbuka kuwa wanadamu wanaofanikiwa siyo tu wale wenye vipaji pekee bali ni wale walioamua kupambana na kila aina ya mawaa bila kukata tamaa. USIKATE TAMAA. Dunia inahitaji wanadamu wanaoishi, wanaoamua maisha yao na kung’ang’ania mpaka mwisho, mpaka kieleweke. Usikubali kubebwa na matatizo yako na kukubali kushindwa na kupelekwa kokote kama mzoga.

Ukitaka kufanikiwa maishani chagua kitu chako, jiendeleze katika hilo,kuwa bora zaidi ya wengine na zaidi ya yote kamwe usikate tamaa. Slogan ya maisha ni : ENDELEA KUSONGA MBELE UKIKATA TAMAA UNAPOTEZWA BILA HURUMA. Watu wengi hushindwa maisha kwani hukata tamaa pasipokujua kuwa wapo karibu na mafanikio yao. Maisha ni kuendelea mbele bila kuvunjika moyo. 

Wapo watu waliopitia magumu kama yako na zaidi yako duniani, hawakukata tamaa na mwisho wa siku walishinda; jifunze kwa watu wafuatao na katika yote usikate tamaa;

Colonel Sanders: Akiwa na miaka   6  baba yake alifariki akamwacha yeye kama baba wa familia, yeye , mama yake na wadogo zake wawili. Alilazimika kujifunza kupika akaweka usharobaro pembeni bila kujali ni mwanaume na akaweza. Alifanya kazi bila kuchagua bila lawama ili kupata pesa za kukidhi mahitaji ya familia. Alitukanwa na kudharauliwa katika kazi hizo, lakini hakuvunjika moyo. Alipofikisha miaka 40; alianza kupika chakula kwaajili ya wasafili wa treni. Umaarufu wa utamu wa mapishi yake ulitapakaa mjini akaanzisha hoteli yake. Mwaka 1950 Colonel akiwa na miaka 60, hoteli yake ilivunjwa na Serikali kwani ilikuwa barabarani, akarudi kuwa maskini wa kutupwa na kudharauliwa. Hakukata tamaa, hakukubali kushindwa. Akiwa na miaka 60, alianza kupika kuku na kupeleka katika mahoteli ili auziwe kwa mkataba, kila hoteli aliyopeleka alikataliwa. Karibu hoteli 1009 zote zilikataa kuingia mkataba wa kuuza kuku wake. Hakukata tamaa. Akaendelea.  Mwisho alikubaliwa na hoteli moja. Baada ya hapo alianza kukubaliwa tena, akaingia mikataba na mahoteli mengine mengi na akawa tajiri tena. Leo hii anafahamika kwa kampuni yake duniani iitwayo KFC ( Kentucky Fried Chicken). Katika yote usikate tamaa.  

Opra winfrey: Dada huyu anafahamika sana katika TV ni mwanamke pekee tajiri duniani. Katika enzi za ujana wake alipatwa na matatizo yenye machungu sana kwa kutendewa vibaya kijinsia pamoja na kufukuzwa kazi kama mtangazaji baada ya kushindwa kazi. Hakukata tamaa, alijaribu njia nyingine tena na sasa anakula mema ya dunia

Winston Churchil:Huyu ni mmoja wa wanasiasa ambaye hatasaulika nchini Uingereza milele. Alifeli mara nyingi akiwa sekondari. Akafeli katika biashara na siasa. Na baadaye mke wake alifariki. HAKUKATA TAMAA. Alipigana na kuendelea kupigana; na akafanikiwa kuwa waziri mkuu wa uingereza akiwa na miaka 62. Alisema maneno haya: “Katika maisha, usikate tamaa, usikate tamaa iwe katika madogo ama makubwa usikate tamaa, usikate tamaa, usikate tamaa na usikate tamaaa”

Abraham Lincoln: Akiwa kijana alipata nafasi ya kwenda vitani kama kapteni baadaye akarudi. Baada ya hapo alianza baishara yake akafirisika na kufeli kabisa.HAKUKATA TAMAA. Akaamua kuwa mwanasheria akashindwa na kufeli.. Akawa mwanasiasa, alipogombea kwa mara ya kwanza kama kiongozi wa chama, alifeli. Akaamua kugombea   UKamishna wa Ofisi ya Mkuu wa Ardhi akashindwa tena. Mwaka 1854 aligombea Useneta akaangushwa vibaya na kufeli tena.HAKUKATA TAMAA.  Mwaka 1856, akagombea umakamu wa rais akaangushwa na kufeli tena. HAKUKATA TAMAA.Mwaka 1858 alirudi na kugombea useneta tena, aliangushwa na kufeli tena. Aliumia sana akamtumia barua rafiki yake ikisema  " Mimi ni mwanadamu duni, nisiye na maana duniani kama haya ninayoyapitia wangepewa binadamu wengine wayaishi, hakika kusingekuwa binadamu anayecheka dunia”. Rafiki yake akamwambia USIKATE TAMAA. Akajaribu tena kugombea urais, na mwaka 1860 alichaguliwa kuwa rais wa marekani. Ni raisi pekee duniani aliyeweza kuifanya marekani kuwa nchi pekee duniani. USIKATE TAMAA

KUMBUKA: Tunaishi katika dunia iliyojaa sababu nyingi zinazoweza kutufanya kukata tamaa na kuyapokea matokeo yoyote kwa kutoa sababu za kushindwa lakini kwa mwanadamu aliyedhamiria, hachoki,kutafuta njia mpya,kujaribu kitu kipya na kamwe hakati tamaa. Hivyo basi katika yote maishani kabla hujakata tamaa jaribu tena.

Asanteni sana….

MUNGU IBARIKI AFRIKA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
Na Geophrey Tenganamba, Director& founder of Perfect Path Innovators
www.treasurehousewithinyou.blogspot.com and www.ppi.co.tz
Kwa semina, mafunzo na ushauri karibu katika ofisi za Perfect Path Innovators; nipigie kwa simu :0714477218. 

Categories:

Leave a Reply