Ndugu mdau wa blog hii yetu leo ningependa tujaribu kuangalia ni mbinu gani unapaswa kutumia ili kudhibiti watu tulio waajiri katika biashara zetu kutotuibia,
jambo ambalo limesababisha wengine wafunge biashara zao au wengine wapate faida wasiyo stahili.
TATIZO LA WATANZANIA BIASHARA ZETU NI PROFIT ORIENTEDSANA, TUNAANGALIA FAIDA TU NA SI KITU KINGINE,

UAMINIFU MDOGO KWA WAFANYA KAZI HUSABABISHWA NA

1. Elimu- kutowapa elimu ya jinsi ya kusimamia vyema biashara

2. Malipo duni- Wafanya kazi wengi sana wanapunjwa, mwajiri yeyeanaangali faida pekee haangalii wafanya kazi wake wanaishi vipi

3. Marupurup/ motivation

MOJA YA NJIA ZA KUFANYA

1. Elimu- Wafundishe kwanza jinsi ya kusimamia mradi wako, wape elimuya wiki moja kama huwezi kutoa elimu ajiri watalaamu watoe elimu hiyo,wafundishe kwamba hiyo biashara ndo itakayo walisha wao so kadri wanavyosimamia vyema na kupata faida ndo na wao watakavyo nufaika

2. Malipo- Jitahidi sana kuwalipa vizuri wafanya kazi wako- usiangaliefaida tu na kuwalipa wafanya kazi wako elifu 60 wakati maisha yenyewe ndo haya,jitahidi kuwalipa vyema, usiangalie tu kwenye kumake super profiti wakatiwafanya kazi wako wakiwa na maisha magumu sana hapo ni lazima wakuibie sana

3. Motivation/ malupulupu- Jitahidi sana kuwapa vitu vingine vya ziadamfano
- Kuwatoa wakaenda hata kutembelea kambuga fulani
- Tenga pesa ya matibabu yao na familia zao
- Kila mwaka uwe unatoa zawadi kwa mfanya kazi bora, zawadi iwe yamaana lakini si zawadi uchwara
- Sometime Biashara yako ikiruhusu wasaide hata katika kusomesha watotowao kwa kuwaambia utatoa kiwango fulani cha pesa
- Uwe unawasiliza mara kwa mara shida zao na kuwasaidia kutatua hizoshida zao
UKIFANYA HAYO WATAKUWA NA MOYO NA KAZI KWA SABABU WANAJUA JINSI GANIUNAVYO WAJALI SANA

kama na wewe unazo mbinu zaidi unaweza kushare na sisi

Categories:

Leave a Reply