Tumeona katika post iliyopita tafsiri
mbalimbali za neno hili MINDSET, kwa tafsiri ya kibantu isiyo rasmi
naweza kusema ni "Mitazamo ama tabia za watu katika kufikili ama
kukabiliana na jambo fulani", hii ni tafsiri yangu.
Mwandishi wa vitabu Carol Dweck amejaribu kuelezea katika kitabu chake cha Mindset sababu mbalimbali za kwanini-
source:http://bongopicha.blogspot.com/
Mwandishi wa vitabu Carol Dweck amejaribu kuelezea katika kitabu chake cha Mindset sababu mbalimbali za kwanini-
- Akili na Kipawa amam kipaji pekee haviwezi kumletea mtu mafanikio,
- au ni jinsi vinaweza kusababisha mtu kutokufanikiwa,
- na je ni kwanini kupongeza hivyo tu hakuleti utashi wa ndani ama mafanikio bali kuyahatarisha tu,
- na je ni jinsi gani kwa kumfundisha mtu ama kuifunza akili wazo dogo tu kwaweza kupandisha kiwango cha ufanisi wa akili na kuleta uzalishaji zaidi.
Mwandshi Dweck anatanabaisha kuwa kuna mawazo mgando fixed mindset na mawazo endelevu ama Growth Mindset, "In a fixed mindset, people believe their basic qualities,
like their intelligence or talent, are simply fixed traits. They spend their
time documenting their intelligence or talent instead of developing them. They
also believe that talent alone creates success—without effort. They’re wrong."
Mfano wa picha hapo juu ni sawa na
watu wenye Fikra ama mawazo mgando, Tembo hawa wa India wakiwa wadogo
ufungwa na mnyororo huo na kigingi hicho, kwa sababu wanakuwa wadogo
wanakuwa hawawezi kujinasua katika kigingi hicho, watajaribu mara kadhaa
wakishindwa wanaacha, wanakata tamaa, wanaamini kuwa hawawezi, kwa
wakati huo kwao kinakuwa ni kikubwa na hakiwezekani.
Kuna msemo kuwa "Tembo uwa hasahau" hivyo
ata anakupokuwa mkubwa kama nyumba anafungwa katika kigingi kile kile
na kwa sababu hasau, Tembo huyo hatofanya juhudi yoyote kujinasua hapo
japo hakika anaweza akiamua kwa sababu angali anakumbuka kwamba
alipokuwa mdogo kilimshinda, hivyo tembo huyu atatulia hapo hapo muda
wote mpaka mtu aje amfungue.
Dale Canergie anasema,
"Develop success from failures. Discouragement and failure
are two of the surest stepping stones to success."
Kwa maana nyingine ni kwamba
kushindwa jambo fulani, iwe masomo, biashara, fursa au mahusiano mara
moja au mbili hata tatu si kushindwa bali ni kujifunza, kwamba kushindwa
huko ndio ngazi ya wewe kuelekea mafanikio, mgunduzi wa taa hizi za
umeme Thomas Edson alijaribu mara zaidi ya 999 kabla ya kufanikiwa
kugundua taa hizi tutumiazo sasa, lakini yeye anasema, "I have not failed. I've just found 10,000 ways that won't
work."
Kama Tembo Je ni wangapi wameendelea
kushikiria mapokeo ama mtazamo kwamba hili haliwezekani ama siliwezi,
kwa sababu tu ama walijaribu wakashindwa tena mara moja au mbili tu? au
kujaribu jambo ama fursa mpya tofauti na mazoea ama mapokea au mitazamo
mgando, huku wakijinadi kuwa wanaishi katika karne ya Sayansi ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ama Information Age?. Jibu utakuwa
nalo msomaji.
Katika mawazo endelevu anasema "In a growth mindset, people believe that their most basic
abilities can be developed through dedication and hard work—brains and talent
are just the starting point. This view creates a love of learning and a
resilience that is essential for great accomplishment. Virtually all great
people have had these qualities."
Hawa si watu waliokubali kuwa kigingi
hiki hawakiwezi, wamejaribu tena na tena, wamejifunza na hawakukata
tamaa na hatimaye ndio kundi la watu wenye mafanikio duniani.
Wengi wetu wa umri kama wangu na
zaidi tunaweza kukumbuka zamani kulikuwa na kampuni hii ya mafuta ya
Shell, hii ni kampuni kubwa sana ya mafuta duniani inaajiri wafanyakazi
wapatao 25,000/-,(takwimu za 2008) vituo vingi vya mafuta mpaka hii leo
vinaitwa Shell hapa nchini, sijui ni wangapi hasa vijana leo hii
wanajua kwanini vituo hivyo vinaitwa kwa jina hilo, sijui, lakini sijui
ni wangapi wanafahamu historia ama sababu ya kampuni hii ya kubwa ya
mafuta kuitwa jina hilo, iko siri kubwa na ya kutia moyo kuhusu kubadili
mtazamo au MINDSET CHANGE, fuatana nami hapa hapa kujua zaidi juu ya
hilo.
Nakutakia
usomaji mwema na mafanikio, Kwa maoni na ushauri waweza kunipigia
0784475576, 0716927070 au email: brwebangira@gmail.com
Categories: