Wapendwa, Napenda kuwafahamisha kwamba tumeanzisha mafunzo ya ujasiriamali kwa watu wote. Mafunzo hayo yatafanyika kila siku ya jumamosi kuanzia tarehe 7/7/2012 kuanzia saa 4.00 asubuhi mpaka saa7.00 mchana .Mafunzo hayo yataendeshwa kwenye ofisi yetu ya Mshauri wa biashara, iliyopo eneo la barabara ya Mandela mkabala wa kituo cha daladala Mabibo Hostel, Dar es salaam. Wawezeshaji watakuwa ni Charles Nazi na Mshauri wa biashara na Mtunzi wa kitabu cha mbinu za biashara na Mshauri wa Biashara Florian Mkyanuzi . Kiingilio cha mafunzo ni Sh. 10,000 kwa kila mshiriki. Mada zitakazofundishwa ni kama ifuatavyo; 1. Namna ya kuanzisha biashara. 2. Namna ya kutafuta masoko na kutangaza biashara yako. 3. Namna ya kutafuta vyanzo vya mtaji. 4. Namna ya kupambana na vikwazo katika biashara yako. 5. Namna ya kuweka kumbu kumbu za hesabu za biashara yako. 6. Mifano hai ambayo unaweza kuifuata na kuanzisha biashara 6. Maswali na majibu. Kwa wale ambao watahudhuria wapige simu au watume ujumbe simu namba 0755394701 CHARLES NAZI Mshauri wa biashara na mtunzi wa kitabu cha Mbinu za biashara; http://www.squidoo.com/mshauricharles

Categories:

Leave a Reply