Wakwanza kulia ni Bwana Gaston Kikuwi.


Jumuiya tatu za biashara nchini, Shirikisho la Biashara na Viwanda nchini (CTI), Shirikisho la Utalii nchini (TCT) na vikundi vya biashara ndogo ndogo (Vibindo), zinatarajia kuzindua ripoti ya mtazamo wa wafanyabiashara kuhusu mazingira ya biashara nchini.

Mbali na kuzindua ripoti hiyo, pia zitaendesha maonyesho ya vibonzo kuhusu mazingira hayo na kuzindua kipindi kipya cha redio kitakachozungumzia masuala yanayokwaza ustawi wa biashara  na uchumi nchini ambapo kitakuwa kikurushwa na kituo cha Radio One.

Mmoja wa waratibu kutoka Vibindo, Gaston Kikuwi, alisema uzinduzi huo utafanyika jijini Dar es Salaam ambapo wafanyabiashara na Watanzania kwa ujumla watapata fursa ya kutafakari hatua za kuchukua juu ya vikwazo vya biashara nchini.

Alisema ripoti itakayozinduliwa inajulikana kama 'Mitazamo ya Viongozi wa Biashara juu ya Mazingira ya Uwekezaji nchini ' ambapo ripoti hiyo itawahusisha pia wachoraji wa vibonzo.

“Ni matarajio yangu kwamba shughuli kama hii itawafanya wadau wote kuongeza bidii ya kuboresha mazingira ya biashara,” alisema Kikuwi.

Aliongeza kwamba mbali na uzinduzi huo, pia wataendesha shindano la wachoraji bora wa vibonzo juu ya mtazamo wa wafanyabiashara kuhusu mazingira ya biashara nchini.

Alisema wachoraji sita watakaofanya vizuri watapata zawadi ya jumla ya dola 4,000 za Marekani ambapo mshindi wa kwanza atazawadiwa dola 1,500.
source: http://wamtaanitz.blogspot.com/2012/07/jumuiya-za-biashara-nchini-kuzindua.html#.UAf-ZtprRag.facebook

Categories:

One Response so far.

  1. Your post is very interesting information about related topic is awesome. I was finding this type of information from long time. I think you should going on to make this type of blog.

Leave a Reply