Wengi wanasema muda si rafiki kwa mwanadamu,wakiwa na maana kuwa jinsi unavyowapita kasi pasipo wao kujua,mara ilikua siku,ghafla wiki,mwezi,miezi mwaka miaka na kuna jambo amabalo analotoka akiwa mdogo mpaka leo hatalitimia,na umri ndio unakaribia uzeeni,lakini swali muhimu hapa kuna mtu alishwahi jiuliza kuwa yeye ana utawala muda au muda unamtawala yeye na kuwa mtuwa au muhanga wa kupoteza muda?Siku moja nikiwa ndani ya seminar moja mwezeshaji siku hiyo aliomba kabla ya kuanza semina naomba tukae kwa ukimya kwa dakika tano,baada ya dakika kupita watu wote walistaajabu walipoona wamekaa zaidi ya dakika tano za muda waotumia Katika mambo yao ya kawaida,mwezeshaji aliendelea kuuliza je mara ngapi tunapata muda wa ukimya na kupangilia mambo yetu na kwenda kama yanavyotakiwa?wengi walinisikitisha sana yeye kwa siku huwa lolote linalotokea na yeye atajua mbele ya safari.Muda ni hazina ambayo ikipotea hairudi tena,na pia lazima mtu anayepoteza muda siku atakuja lipia huo muda kwa namna yeyote ile.Mara kadhaa kwa mazingira ya hapa kwetu Afrika  mimi huwa nasema teknologia imeleta maafamakubwa sana kwa watu wasioandaliwa kwa mabadiliko,vitu kama luninga,redio,simu,komputa ,mitandao ya kijamii,magari,nk vyote hivi vimekuja kama bahari au mafuriko kuwazoa watu wasiokuwa na taarifa ya tukio kabla,wanadamu wote tuna masaa 24 je umeshawahi jiuliza katika masaa 24 umeutumia vipi kutengeneneza vitu vipya au kuongeza dhamani katika maisha yako?mathalani mmiliki wa kampuni chukulia Bakhersa yeye ana masaa 24 kama,kutokana na kuona masaa ishirini na nne haya mtoshi akamua kununua masaa kutoka kwa watu wengine kwa masaa 8 kwa kila mtu kila siku,fikiria kama kaajiri watu 1000 kwa siku yeye maisha yake ana  masaa 1018 kwa siku,hapa najaribu weka maaana ya umuhimu wa muda,je wewe muda wako wa masaa 24 unakutosha?kama sio je huo huo muda ambao haukutoshi unautumia kwa ajili yako zaidi?au unautoa bure kuangalia luninga,tamthilia,piga simu zisizo na masilahi,kuingia na kukaa mitandao ya kijamii siku nzima?kama hupo katika kipengele hichi hakika dunia inakudai deni la sababu ya kuja hapa duniani.
Kuna sababu amabazo hupelekea watu wengi kushindwa kuutawala muda vema nazo ni:
Kutokuwa na malengo;Ni ngumu sana kufanikisha jambo kama hujaweka malengo ambayo yanaeleweka mfano nini unataka,lini,wapi,kiasi gani nk
Kutokuwa na mpangilio;jambo lisilokuwa na mpangalio unaeleweka,mtiririko mzima wa hilo jambo,dalili hizo hupelekea jambo kuchukua muda ili kuweza kufanikiwa au kutofanikiwa kabisa.
Uwezo wa kushindwa kusema hapana;Wote tunapenda kusaidia wengine ili wafanikiwe kama sisi tunavyhitaji msaada kutoka kwa wengine lakini wakati mwingine mtu utakuja jambo lipo nje ya uwezo wake na kushindwa kushindwa kusema hapana kwa kumuonea huruma mtu huku mtu akijua kwa kweli jambo hilo mwishoe atashindwa kulifanikisha,pia kuharibu ratiba yako kwa ajili ya mtu mwingine mwenye ratiba yake binafsi kwa sababu ya woga wa kusema hapana.
Kuingiliana mambo;mara kadhaa tumekuwa katikati ya jambo fulani ghafla kitu fulani ambacho nacho ni muhimu kikaja mfano simu ikaita,lakini simu sio kitu cha kukutoa wewe kwenye jambo unalolifanya kupokea hiyo simu,kama ukiamua kupokea simu hili jambo ambalo unalifanya sasa itachukuamuda wako mwingi au hata kuanza mwanzo kwa lile jambo la awali,Maliza moja ufuate jambo lingine.
Namna ya kufanya ili uwe mshindi katika kutumia muda vema:
Weka malengo;malengo yakupatia ili hali yapi unaelekea,mtu mwenye malengo huwa anachukua muda mdogo sana kufanikisha jambo fulani,tengeneza sasa malengo maishani sasa,hakikisha sasa malengo yako yanaeleweka kwanza na wewe ,weka kipimo kiasi gani unataka fika ili siku ya mwisho uje upime ni kiasi gani umefanikiwa,malengo pia yanatakiwa yawe yawezekana na halisia.
Weka vipao mbele;kama kiongozi katika ofisi,familia au kikundi unaweza kuwa una mambo mengi yapo mbele yako ,ni salama kusema kuwa hutaweza kufanikisha mambo hayo yote kwa pamoja,ni busara kuyapangilia mambo  kwa listi maalumu kwa kuanzia yale muhimu na kufuatia yasio na muhimu ,na hata kama hukufanikisha yote leo yaliyobakia kesho au wakati mwingine yawekee kipao mbele cha kwanza.
Pangilia mambo yako,ukitaka jua mtu kama wewe unapangalia na kuokoa muda katika mambo yako tizama ofisi yako au nyumbani kwako jinsi vitu vilivyo,mtu ambaye anadalili ya kupoteza muda ofisini kwake kupo rafu rafu chumbani kwake vitu vipo shaghala-bagala,mtu mwenye malengo ya kweli maishani huwa anapangalia mambo yake ili aweze okoa muda,kama vitu vipo shaghala-bagala siku ukitafuta kitu kidogo unaweza chukua zaidi ya siku nzima bila hata kukipata,hivyo ni busara kupangilia mafaili,viandikio,mashine,nk katika ofisi, nk.
Jifunze ni wakati gani wakusema hapana;Kuna wakati ni mwakafa wa kusema,majukumu kwa jamii ni jambo la kawaida  sana kama sehemu ya kurudisha kwa jamii matunda ya kipaji chako au elimu,lakini utakuta wakati mwingine majukumu ni mengi kupita uwezo wako,katika wakati kama huu  ni kosa kukubali wakati unajua utakuja shindwa tekeleza kwa usahihi au kabisa,tumia hiz kanuni tatu,tambua sio kila kitu unaweza fanya,usikubali kukubali mradi au jambo ambalo hutaweza kulifanikisha kwa muda uliowekwa kulifanikisha,sito jifunga  na mambo amabayo hahusiani na malengo na madhuni yangu binafsi ,hakika ukifuata hizi kanuni utafanikiwa sana.
Tumia vema muda ule unapokuwa unasubiri kitu au jambo fulani,usifikiri muda wa aina hii unaenda kwa faida,anza sasa kuokoa muda ukiwa unasubiria  kupanda basi,ukiwa unasafiri kwenda mkoanai,ukiwa unasubiri labda kumuona dokta,bossi,kusubiri wezako wafike kwa mkutano,darasani,shereheni,kanisani,meditation.Watu wenye mafanikio hutumia vema muda ambao wanasubiria jambo fulani kutimia au tokea.
Kuna faida nyingi sana  kutawala matumizi ya muda,na hivyo kukupelekea katika mafanikio makubwaa katika mambo unayofanya,pia ni hukupatia afya njema ya mwili na akili na jambo lingine la muhimu sana huongeza ufanisi wa mambo unayofanya tofauti na watu wasio tumia vema muda.
source: http://www.tanzaniaachievers.blogspot.com/

Categories:

Leave a Reply