Ulishawahi kwenda kwa semina au mkutano wa wafanyabiashara,wakati wa mapunziko au mwisho wakati wa kubadilishana mawazo na kujenga mtandao zaidi wa kibiashara ukawa mkiwa(pekee yako)?Haupo peke yako,watu wengi huwajisikii vema wakiwa ndani na watu wasiowazoea/zoeana nao.Lakini matukio ya kutengeneza mitandao ya kibiashara(networking business events) yanasaida sana kufanya biashara yako kukua zaidi na pia yanakuwezesha wewe kufanya taifi za papo kwa hapo juu soko lako.Kujifunza kujichanganya na watu nakufuatilia mawasiliano msilio badilishana kwa matukio ya kibiashara ni muhimu sana kwa mafanikio ya biashara yako sana sana kama mtu umejiajiri mwenyewe.Zifuatazo ni dondoo ambazo zitakusaidia wewe kukuunganisha na wengine vema zaidi: KABLA YA TUKIO Jiandae kwa ajili ya tukio kwa kutengeneza business card za kutosha,peni,kitabu kidogo(note-book).Hakikisha umekula kabla ya kwenda tukio.Kama ni ni sherehe ya cocktail au chakula kinatolew/hudumiwa huko,wakati wa kubadilishana mawazo na kutengeneza mtandao wako, ni bora ukakabeba kinywaji tu pekee,kuliko kuzunguka na sahani ya chakula kila sehemu. Elewa lengo lako:Nini nia yako ya kuhudhuria tukio husika?kukutana na watu Fulani?Kutafuta wateja wako wapya watarajiwa?Kutafuta rasilimali unazohitaji?Kukutana na marafiki wapya?Kukuza uhusihano ulipo wewe na wengine? Mathalani peleka business card 20 na hakikisha unazigawa kwa watu zote kabla ya kuondoka.Ulizia pia kwa watu wengine kama wana business card kama dhahiri unataka kuendelea wasiliana nao.Sio kila mtu utakaye kutana naye atakuwa rasilimali kwako. Ongea na mwandaaji wa tukio kuhusu vazi la siku hiyo(dress code)Matukio mengine yanahitaji mtu uvae mavazi rasmi kimwonekano wa biashara zaidi kama suti.Matukio mengine yanahitaji kuvaa mavasi yasio rasmi(kawaida), na mengine ni mchanganyiko wa mitindo yote kutokana na matakwa ya mtu binafsi. Kwa kujua kwa awali(kabla) nini unatarajia ,unaongeza hamasa na hisia za kujisikia kuwa mmoja kati ya kundi la tukio husika. NDANI YA TUKIO Kwanza wasili mapema kwa tukio.Fika pale mapema sana wakati kundi likiwa dogo na nirahisi kuongozeka.Ingia kwa bwalo/ukumbi kwa tabasamu.Hata kama unajisikia vibaya/hasira siku hiyo igiza tu kama unafuraha kwa kuweka tabasamu kwa sura yako utaoneka kwa wengine unaingilika,ni rafiki kwa kila mtu,unashauku la kufahamiana na wengine.Hakikisha unajichanganya na wengine.Usijitenge na kukaa na marafiki zako pekee au washirika wako unaowajua,tembea tembea .Tumia sio zaidi ya dakika 5-6 kuzungumza na kila mtu.Wafikie watu mbalimbali na jitambulishe kwa kila mtu(kama sio mmoja wa wana kundi,waombe kwanza wahusiki ili wakuruhu kama unaweza kuwa mmoja wa wao,kisha wasalimie na kujitambulisha kwao,inakupatia nafasi ya kufungua milango kwao) Wakati ukikutana na watu wasalimie kwa kuwashikana mikono na urudie majina yao,hii haisadii tu kuyakumbuka majina yao ,bali inaonyesha uweka juhudi kusikia vema majina yao.Vaa kikadi ambacho kinaonyesha jina lako na ukiweke mbele ya shati lako ili kila mtu aweze soma vema jina lako,weka upande wa kulia wa bega lako ili iwe rahisi kilamtu kukiona wakati ukishana nao mikono.Jifunze jinsi ya kujitambulisha wewe mwenyewe,katika sekunde chini ya thalathini eleza kazi yako. Sikiliza zaidi watu kuliko kuongea.Kumbuka hamna kitu bora zaidi ya kusikila kimakini zaidi na kuonyesha moyo wa kuwakubali watu wengine.Uliza swali na sikiliza majibu kimakini sana ili uweze kumwelewa mtu.Hii itakusaidi kugundua mteja mzuri wa kufanya naye kazi kwa huduma au bidhaa zako.Chukua kumbukumbu ili uweze kukumbuka nini watu wamesema. Wakati ukirudi ofisini weka taarifa zote katika program ya mawasiliana ya uongozi. BAADA YA TUKIO Baada ya kupata business card zao,ana kufuatilia ndani ya masaa 24 baada ya tukio.Kama mnaweza kutengene muunganiko wenye manufaa kwa pande zote mbili ya kibiashara na watu ambao mmekutana nao kwa tukio,wapigie simu na kuwakaribisha kwa mlo wa mchana kwa ajili ya kuendeleza zaidi muunganikao wenu wa kibiashara. Kwenye kalenda yako wakati ukiandika semina au matukio unayotarajia kuhudhuria tenga pia masaa mawili au tatu ya kesho yake kufuatilia ili uweze fanikisha kazi nzima. Wakati ukiangalia matukio yajayo ya kibiashara yenye nia ya kutengeneza mitando baina ya wafanya biashara,fanya tafiti za soko(market research) na ujue wateja gani unatarajia kwenda kukutana nao,inaweza ni bonge la furaha badala ya huzuni.Kupangilia kitu kinakufanya wewe ufanye vema zaidi. Author:Deogratius kilawe Title:Business consultant Phone:+255717109362 Email:deogratiuskilawe@yahoo.com Blog:Tanzaniaachievers.blogspot.com Facebook/Skype ID:Deo kilawe/Kilawe 1

Categories:

Leave a Reply