Hiyo pesa yako iweke kwanza mpaka utakapopata au utakapojua nini majibu ya haya maswali:
1. Biashara gani ambayo una uwezo wa kuifanya (hapa tunamaanisha capacity)
2. Eneo gani unataka kuifanyia hiyo biashara-je wateja wanapatikana sehemu hiyo? na banda la kufanyia biashara, gharama ya banda?
3. Soko la hiyo bidhaa ikoje? nina maana ya je ina soko mwaka mzima au kwa kipindi fulani tu.
4. Bidhaa utakazouza zitapatikanaje?
5. Je mzunguko wa pesa katika eneo hilo ukoje?
6. Je wateja wako ni kundi gani au ni watu wa aina gani?
7. Mtaji wa biashara huo ni kiasi gani?
8. Je unataka kufanya biashara mwenyewe au kuna mtu au watu utawaajiri ili wakusaidie, kama ndivyo je ni watu wa aina gani na nini gharama zao?
9. Je hiyo biashara itahitaji kiasi gani, na unategemea kuuza kiasi gani kwa siku au kwa mwezi? na je unategmea baada ya muda gani mtaji wako ulioweka kwenye biashara iweze kurudi?
10. N.K
Kama hauwezi kujibu hayo maswali au 80 asilimia ya hayo maswali vizuri, basi hiyo pesa yako nakushauri ukatafute kiwanja eneo zuri ukanunue na mara utakapokuwa tayari unajua biashara gani ya kufanya, ndipo ukauze hicho kiwanja ili hiyo pesa utumie kwenye hiyo biashara. Kiwanja ununue sehemu ambayo ni potential ili utakapohitaji kuuza usipate shida.
Onyo.
Kamwe usipoteze pesa zako kwa kutafuta akuandalie business plan kabla hujajua bado ni aina gani ya biashara una uwezo wa kuufanya
Categories: