SABABU ZINAZO PELEKEA HUDUMA MBAYA KWA WATEJA 1. Wafanyakazi hawajafundishwa Hii inaweza kuwa ni sababu namba moja kabisa na kubwa ya customer service mbovu, wajasiriamali wamekuwa wakiajiri watu bila kuwapa elimu matokeo yake wafanya kazi wanatuma ozoefu wao tu Mfano: Kuajiri Ndugu, jamaa, marafiki, mke/mme hawa watu mara nyingi huwekwa kwa kigezo cha undugu na si kigezo cha kuwa na uelewa wa kutosha kusimamia biashara SULUHISHO: Nilazima tuwekeze katika kufundisha wafanyakazi wetu jinsi ya kuwahudumia wateja hii ni kwa biashara ambazo huwa zina intaraction kati ya wateja na wauzaji kama Hoteli, Dukani, Baa na kazalika 2. Kuto kujari Hapa ni kwamba mjasiriamali haoni umuhimu wa kuwa na watu wa kutoa huduma au kuwahudumia wateja vizuri, hili ndo tatizo letu tunacho anagalia ni pesa imeingia jioni yanafanyika mahesabu kwisha kazi, Hata kama mfanyakazi kapigana au kutukanana na mteja tajiri hajali anacho jari ni pesa inaingia 3. HUJUMA Wafanyakazi kuwa na hasiria au kuwa na furastration ni sababu nyingine ya kuamua kufanya wanavyo jua, nazani, mafanya kazi anaweza amua kujibu mteja anavyo jisikia yeye kwa sababu tu akukomoe wewe tajiri wake, Hujuma dhidi ya tajiri mara nyingi huwa ni chnazo cha poor customer service SULUHISHO: Wewe kama mkurugenzi ni lazima kuongea na wafanya kazi wako mara kwa mara kusikiliza matatizo yao na kuyatatua ili wasihamishie hasira zao kwa wateja 4. Wafanyakazi kuto kuwa na Imani na bidhaa au huduma Hii mara nyingi hutokea pale ambapo matangazo ya dumua fulani au bidhaa hayaendani na uharisia matokeo yake wafanya kazi wanakuwa wanaogopa hata kuwahudumia wateja au wanabaki kusema subiri tukuitie mtu akupe maelezo zaidi Au utakuta matangazo yanasema vingine na wafanyakazi wamefundishwa vingine, utakuta bei ya Tangazo la Wali kuku ni buku 3, lakini ukiingia ndani mfanaya kazi anakupa bei nyingine kabisa buku 4 SULUHISHO: kuwa mkweli katika ubora wako na matangazo yako ya masoko na ikitokea tatizo li fix mara moja na wateja wajue 5. Matatizo Binafisi ya Mfanya kazi yanapo jionyesha kazini Utakuta mfanyakazi anamatatizo binafisi ya kifamilia au hata ya kiafya na yale matatizo yanakuwa yanaonekana hadi kazini, MFANO: Mfanyakazi kugombana na rafiki yake/mke wake/mme wake na kazalika na ule ugonvi unakuwa bado kichwani mwa yule mfanyakazi na unauhamishia kazini na hapa huenda akawa anatpoa huduma huku ana hasira, mawazo na kazalika SULUHISHO: Hakikisha unonana na wafanyakazi wako kabla hawajaanza kazi, au hakikisha unakuwa unawachunguza mara kwa mara ili kuona kama mfanya kazi ana mabadiliko fulani make matatizo yanaweza yakamkuta akiwa kazini kupitia simu. Saa zingine hakikisha wafanya kazi wanapo ingia kazini wanazima simu zao na wawashe muda wanaondoka, make kitendo cha simu kuwa oni wakati anawahudumia wateja anaweza pata ujumbe wa kufiwa au kupigwa chini na mpenzi wake na kupelekea hata kupia yowe kazini 6. Lawama nyingi kwa mfanayakazi Unnweza kuta kila mfanya kazi wako akikosea kidogo unampandishia, unamulaumu sana, unatishia kumfukuza kazi na kazalika, hili nalo hushusha morali ya yeye kufanya kazi vyema SOLUTION: kuongea na wafanya kazi wako vizuri na hata kama amekosea subiri amalize kazi kabisa ndo umuite na umugombeze na si kumgombeza papo kwa papo 7. KUSHINDWA KUTATUA MATATIZO YAO KWA WAKATI Kushindwa kutatua matatizo yao kutapelekea wakose molari na kazi na hivyo kukuletea hasara ndani ya kampuni 8. Wafanyakazi kuto kuona Umuhimu wao au majukumu yao Mfanyakazi anaweza asione umuhimu wa yeye kuwahudumia wateja vizuri kwa sababu haoni umuhimu wa kufanya hivyo kwanza kampuni si yake wala ya Baba yake so haoni umuhimu wowote ule SULUHISHO: Kumbuka kwamba wafanyakazi ndo hubeba image ya kampuni hivyo waelimishe wafanya kazi wako umuhimu wao kwenye kampuni, waambie hii kampuni bila wao si kitu, waambie huduma yao nzuri ndo itasababisha kampun I ipate pesa za kuwalipa mishahara 9. Top management kuto kutatua matatizo mengine yanayo husu wateja, mfano huduma au bidhaa Mfanya kazi anaweza amua kuwa na hasira au kuacha kabisa kuwahudumia wateja endapo kuna matatizo yanakuwa hayatatuliwi na kampuni kwa wakati, MFANO: Simu ya kampuni ni mbuvu na management imeshindwa kuitengeza kwa wakati, hii inaweza pelekea mtoa huduma kwa wateja kukasirika SULUHISHO: Jitahidi kutatua kwa wakati matatizo yote yanayo husiana na huduma kwa wateja 10. Mishahara midogo, hakuna malupulupu Utakuta wafanya kazi wanacho zalisha ni tofauti na wanacho lipwa hapa ni lazima wakate tamaa na waamue kutoa huduma duni kwa wateja SULUTION: Walipe vyema wafanyakazi wako ili basi na wao watoe huduma bora kwa wateja 11. UCHOVU Wafanya kazi kuchoka sana wakiwa kazini inaweza kupelekea kutoa huduma duni kwa wateja source:chasha member of jf

Categories:

Leave a Reply