Mwanafalsafa na uchumi mmoja mashuhuri sana kipindi chote Karl Marx aliwahi sema nchi huundwa na watu,na watu hupanga sheria, pia mfumo wa maisha waishi pia sheria na mfumo wa wa maisha unabadilika kutokana na haohao watu kutokana na hali ya kipindi na ugunduzi yaani mifumo na sheria za nchi hazijashuka moja kwa moja kutoka kwa Mungu bali zimetungwa na watu,Pia kuna msemo mmoja wa benki mmoja hapa duniani kuwa maisha ni ugunduzi na katika hilo mimi nikaongezea kuwa na ugunduzi ni maisha.Hivi sasa suala la uraia wa nchi mbili ambalo lilianza mud asana nchi za magharibi ingawa hapa kwetu Africa lilichelewa lakini sio kuwa tumechelewa sana,Katika nchi za afrika lilianza pata nguvu sana baada ya mataifa ya afrika mengi yao kuanza andika katiba mpya mfano Kenya nk,hapa kwetu Tanzania ndio hivi limepigiwa kelele miaka takiribani miaka mingi ivi toka miaka ya tisini mwishoni ivi sana sana lakini hali halisi hapa Tanzania ambalo mimi nimeshuhudia kuwa raia wengi hawajui nini maana ya uraia wan chi mbili,je linafaida gani kwa raia wa Tanzania ?je nini faida yake kwa taifa?je hii sio upenyo wa kuliuza taifa?na walio wengi sana wanaona hilo halina umuhimu kwao hivo hawana muda kujadili hilo,Lakini kwa hii dunia ya digitali unaweza nunia swala Fulani dunia inajadili kweli ?Mwaka jana kuna taifa lilikuwa linatoa fursa kwa dunia kutuma maombi ya kujiunga na mradi wao diversity visa,ambapo kupitia mpango huu unaweza kwenda kuishi nchi hiyo na baadae kuwa raia wa nchi hiyo kuanzia 2013,lakini wakati yote haya yanatokea ghafla fikra yangu ikawa inanirudisha nyuma wakati nikiwa namaliza chuo,nilikuwa mmoja wanachama wa taasisi fulani,kama ilivyo ada nilikuwa nataka kuomba kufanya internship yangu nchi za Asia,Ulaya,USA lakini kuna ushindani mkubwa san asana kama unataka kuwa kufanya kazi au internship sharti la kubwa ambalo unatakiwa ukidhi mara nyingi ni kuwa raia wa nchi hizo au ni raia wa nchi mojawapo wa ukanda huo,Hivyo kupelekea watanzania wengi na Africa kukosa fursa hizo kwa sababu sio raia wa taifa hilo au raia wan chi mojawapo wa ukanda huo na kweli hii inawatia gharama kwa taifa kukosa fursa ya raia wao kutumika nje ya nchi na kuleta mitaji na ujuzi ndani ya Tanzania na kweli kipindi hicho kili ni gharimu sana.
Zifuatazo ni sababu za kiuchumi za kuwa na uraia wan chi mbili kwa taifa:
Tenda za kibiashara na ajira nje ya nchi, mataifa mengi yaliyo endelea sana dunia ili uweze kupata kazi katika serikali zao na makampuni binafsi inabidi uwe raia wa nchi hiyo mara nyingi,hii sababu imewagharimu sana vijana wetu wa Tanzania wenye uwezo wa kufanya kazi nje na kuleta fedha na mitaji mikubwa sana kwa uchumi wa Tanzania,Vile vile kwa wafanyabiashara wa Tanzania wamekuwa muhanga sana kwa hili kwani kwa dunia hii ya ushindani tena wakati tena ubora karibia washindani upo sawa na sisi lakini tu sisi sio raia wa hiyo nchi huwa ni ngumu sana kupata hiyo tenda san asana serikalini za nchi za wezetu,na kuwapatia raia wan chi hizo.
Uraihisi wa kutembea nchi baada ya nchi, hatua ni ndogo sana kupata visa kwa kuwa nchi yako ndio unakuwa unatembelea hivyo kupelekea kuokoa rasilimali muda na usumbufu mwingine wakati unataka kwenda nchi Fulani huhitaji visa,ni passport tu.
Kuchochea ufanisi Kwa sababu ya makundi mbalimbali Kwa nchi (diversity),uwepo wa jamii tofauti ndani ya jamii huchochea ufanisi na ugunduzi na kupelekea kila kundi kutaka kuweka mchango na heshima ya jamii kwa wengine na hivyo hivyo kwa jamii au kundi lingine kwa jamii,hii ni kama ushindani ndani ya jamii kwa makundi ,mathalani kwa ofisi yenye mafanikio ni ile iliyo na makundi yote mfano wanawake,wanaume,vijana,wazee,wasomi na wasiosoma,waliotoka kwa familia tajiri na waliotoka kwa masikini familia hivyo kwa hapa kutengeneza manzingira ya ufanisi wa kazi maofisini,lakini ni ngumu sana kwa ofisi iliyo na wazee tu kuwa na ufanisi au ofisi iliyo na vijana tu kuwa na mafanikio lazima kuwa na mchanganyiko ili mafanikio yatokee.
Uwezo wa kumiliki ardhi na mali nyingine nje ya nchi,Nchi mbambali ni ngumu kumiliki ardi au kukodi ardi ni kinyume cha sheria kama sio raia wa nchi husika au kumiliki mali mfano nyumba na kadhalika,na hivyo kuwanyima haki za msingi mtu kuwekeza kwa gharama nafuu nje ya nchi na hivyo kupelekea kuwa na hasara au gharama kubwa za kukodi ardi kwa wazawa.
Hizi ni baadhi ya hasara za urai wa nchi mbili.
Ni fursa maadui wa nchi kuitumia kuliangamiza taifa(magaidi),Hii mara kadhaa imetokea nchi kama marekani ambapo kuna raia wengi amabao wanatumiwa na magaidi,na kufanya matukio,na hivyo hii sheria ya uraia wa nchi mbili ikawa karaaa kwa serikali.
Raia wenye uraia wa nchi mbili anaweza kuwa na masilahi(interest) kwa taifa moja,lakini anatumia nafasi aliyonayo kuisaidia masilahi(interest) ya taifa lingine kwa gharama ya taifa lake la pili,mfano kutokana na kuwepo kwa uraia wa nchi mbili Israel na USA ,raia wa aina hii wenye nyazifa kubwa marekani hutumia fursa hii kutimiza matakwa ya Israeli kwa gharama ya USA mfano vita ya Iraq ilitokana na ushawishi wa watu wenye uraia wan chi mbili marekani na isareal lakini walitumia nafasi hiyo kutimiza matakwa ya taifa lao mama Israel.
Hamna jambo nzuri lisilokosa changamoto,hizo ni changamoto uraia wa nchi mbili unafaida kubwa sana kuliko hasara ambapo hasara zinaweza kuzuilika kama mfumo ukiwa mzuri wa ulinzi,Ni wakati sasa wa kuamua kuweka historia mpya hapa Tanzania kwa mchakato huu wa katiba mpya,tuliunge mkono kwa faiada ya vizazi vya sasa na baadae.
Imeandikwa na Deogratius kilawe,
Mshauri wa mambo ya biashara hapa Tanzania ,
Facebook name:deo kilawe fans page na deo kilawe
Simu:0717109362
Twitter:afri youth organizat

Categories:

Leave a Reply