Habari mwana blog na hongera kwa kuuanza tena mwezi mwingine na huu ni ujumbe wa mwezi huu wa nne
Si jambo rahisi kuanzisha kitu na kiweze kufanikiwa kwa urahisi urahisi
tu bali unatumia nguvu za ziada kuanzisha na wakati mwingine usiweze
kuona mafanikio ya papo kwa papo waweza kusubiri miaka na miaka na
mwishowe unaanza kukata tamaa.
Mpendwa wangu kufanya kitu kunahitaji ujasiri wa hali ya juu na
kunahiitaji kujitoa kwa hali ya juu sana mpaka uweze kufanikisha lile
kusudio ulilotaka kulifanya kama wewe umeamua kufanya biashara au kusoma
tumia nguvu za ziada ili uweze kufanikisha azma yako uliyokusudia kwa
wakati wako kwa ni mlia kivulini alitafutia juani hivyo una budi kukaza
buti na kufany kile ulichoshindwa kikawezekana ndo mana nasema kuwa
'UKITHUBUTU UNAWEZA FANYA MAAMUZI SASA YALIYOSAHIHI DO IT'
by ladyfurahia
Categories: