"Wanadamu wote walioweza kufanikiwa kwa kujitengenezea mafanikio wenyewe kutoka chini ni wale ambao wametambua sababu ya wao kuwa wao, wananjua ni nini wanakitaka na wanajua kuwa ili maisha yao yawe na maana lazima wafanikiwe katika hilo"
Maisha
ya mafanikio duniani ni haki ya kila mwanadamu. Hakuna binadamu
aliyeletwa duniani kuja kushuhudia wengine wakifanikiwa huku yeye akiwa
katika umaskini siku zote. Kila mwanadamu mwenye pumzi anayo
haki,nafasi, uwezo na uchaguzi wa kuwa anavyotaka kulingana na maana ya
mafanikio atakayotengeneza na mwenyewe.
Ni
kweli tunaishi katika dunia yenye utofauti kimafanikio wapo wenye
mafanikio makubwa, wapo maskini na wale wenye maisha ya kawaida. Lakini
kwa pamoja yatupasa tufahamu kuwa, kila mwanadamu anao uwezo wa
kufanikiwa , na zaidi ni kuwa kila mtu anao uchaguzi wa kuamua maisha
yake – lakini angalizo ni kuwa mtu yeyote aliyeweza kufanikiwa ametambua
kuwa , kuna vichangizi vya mafanikio / success ingredients.
Unachopaswa
kutambua ni kuwa , hali ya maisha uliyonayo sasa si kipimo cha
mafanikio yako ya baadaye, unaweza kuwa vyovyote kimafanikio kulingana
na utakavyochagua mwenyewe. Ni muhimu kuyajua maisha kwa kujua vichagizi
vinavyoweza kutufanya tuishi maisha ya mafanikio na vichangizi hivyo ni
kama ifuatavyo:
1. Fahamu Madhumuni au sababu ya kuwepo kwako: Mwanadamu
anayejua dhumuni lake duniani huishi maisha ya maana. Hatukuja duniani
kuwepo tu bali kuishi kimafanikio huku tukijua kwanini tunaishi. Ukijua
ni kwanini unaishi hutakubali kuishi kiholelaholela huku ukisubiri muda
wako wa kuishi duniani kuisha. Dhumuni la wewe kuwepo duniani ni kuishi
maisha yenye madhumuni, maisha yenye mafanikio na maisha yanoyonufaisha
wengine. Wanadamu wote walioweza kufanikiwa kwa kujitengenezea mafanikio
wenyewe kutoka chini ni wale ambao wametambua sababu ya wao kuwa wao,
wananjua ni nini wanakitaka na wanajua kuwa ili maisha yao yawe na maana
lazima wafanikiwe katika hilo.Ukitaka kutengeneza maisha yenye
mafanikio duniani, tafuta kujua dhumuni lako hapa duniani .
2. Jiamini na amini kuwa unaweza: Wanadamu
wote waliofanikiwa duniani waliamini kuwa wanaweza kuibadili dunia.
Mwanadamu anayeyarudisha maisha yako nyuma ni wewe mwenyewe, ukitaka
kufanikiwa katika lolote utakalochagua jiamini na amini kuwa unaweza.
Hakuna kitu chochote kilichowahi kutokea duniani bila kujiamini. Siyo
kwamba hatuyawezi tunayoyapanga, bali hatujatambua kuwa chochote kile
ambacho mwanadamu akiamua kukiamini kuwa anakiweza ,kitatokea na
kinawezekana. Uwezo mkubwa wa mwanadamu haupo katika umbile lake bali
katika kiwango cha kujiamini kuwa anaweza kuwa anavyotaka. Vyovyote vile
unavyotaka kuwa jiamini unaweza kuwa hivyo na dunia itakubaliana na
wewe kuwa unaweza.
3. Tafuta unachokipenda na kifurahie.
Kila
mwanadamu anayo zawadi ndani yake , zawadi hii huja kama kitu
anachokipenda na kukiweza. Ndani ya mwanadamu vipo vipawa na uwezo wa
ajabu wa kuishi maisha ya mafanikio. Kila mtu ana kitu anachopenda,
kinachoweza kutumika na kuendelezwa na kuleta mafanikio. Dunia ya sasa
ni dunia ya wanadamu wanaojua ni kitu gani wanaweza. Wapo wanaopenda
kuwa madaktari, wapo wanaopenda kuwa waimbaji nk. Kila mtu ana kitu
anachopenda kinachomfanya acheke akiwa duniani. Tafuta kitu
unachokipenda na kiendeleze , kitakuletea mafanikio.
4. Kuwa mtendaji sana
Maisha
ni vitendo na si ndoto pekee, ndoto ni mwanzo tu wa maisha. Maisha ni
kuchukua hatua na si kufikiri pekee. Maisha ni kusonga mbele na si
kupanga peke yake. Katika yote uliyochagua maishani kuwa mtendaji,
usikubali kuyaishi maneno ishi matendo. Anza mahali ulipo kwa kile
ulichonacho kwa kuwatumia watu ulionao na maisha yako yataanzia hapo.
Zaidi jifunze kuishi vizuri na wanadamu, ukifanya hivyo utayafurahia
maisha ya mafanikio.
5. Kuwa na njaa ya kutafuta maarifa siku zote.
Maisha
bila maarifa ni sawa na gari lisilo na mafuta. Ukitaka kutembea na
kuishi kimafanikio kuwa na njaa ya maarifa kila siku. Binadamu wote
wenye mafanikio duniani hawachoki kutafuta maarifa kwa kusoma vitabu,
kuuliza na kujifunaza , na hata kuhudhuria mafunzo ya kuwaendeleza mara
kwa mara. Maisha bila maarifa hayatembei.
6. Usikate tamaa.
Maisha
yana mengi, muda mwingine yale tunayapanga hayaji kama tulivyopanga
lakini yote hutokea kwasababu. Mambo yote tunayapitia katika maisha huwa
ni hatua ya ukuajia kimaisha. Ukiona biashara yako inafanya vizuri
tambua kuwa ni kweli biashara yako inakua, lakini ukiona biashara yako
inafanya vibaya tambua kuwa uwezo wako unakua zaidi. Usikate tamaa
katika kile ulichochagua, kabla hujakata tamaa jaribu tena. Maisha ni ya
kwako usikubali kupoteza hitaji la moyo wako kwasababu ya unayoyapitia.
Tafuta njia zaidi, jiendeleze na jipe moyo kuwa siku yako ya mafanikio
inakuja.
Nahitimisha kwa kusema kila mtu ana uwezo wa kuchagua kuwa anavyotaka kuwa maishani,Dunia
ina mengi ya kuyafanya na kuna kila nafasi kwa mwanadamu yeyote
anayechagua kuwa anavyotaka maishani. Chagua maisha unayotaka kuyaishi
na uyaishi kweli. Usiogope kujaribu kitu, maisha ya kuogopa kufanya kitu
ni maisha yasiyo na maana. Usikubali maisha ya ukawaida na yenye
usalama ambayo yatakufanya usiishi maisha makubwa unayostahili. Siri
kubwa ya watu wenye mafanikio duniani, ni kuwa hawaogopi maisha - wapo
tayari kuumia kwa kuchagua maisha wayatakayo. Chagua unachotaka
kukifanya na ukifanye kweli kwa moyo wote. Jiendeleze kila siku katika
ulilochagua kiasi ambacho utavunja mipaka na kuweka rekodi yako. Chagua
Kufanikiwa.
source:http://www.treasurehousewithinyou.blogspot.com/
Categories: