Maisha ya mtoto yapo katika hatua ya ukuwaji kila siku. mambo yanayomzunguka na hasa anayotendewa ndio yanayomtengeneza kuwa jinsi alivyo kwasasa na hata baadaye. Msukumo wa nje ya mazingira yake ndio unaotengeneza maisha yake,tabia yake,akili yake na hata uwezo wake. mtoto ni jinsi alivyo kutokana na jinsi alivyolelewa kuwa alivyo na jinsi anavyotendewa. Atakuwa atakavyokuwa baadaye kutokana na yale anayoyashuhudia, anayoyaona,anayoyasikia,anayoambiwa,anayofundishwa na zaidi sana kwa anayotendewa.
Watoto ni viumbe vinavyokuwa  kiakili, kihisia na kisaikolojia kwa kutumia msukumo wa nje sana kuliko wa ndani.
Ni kweli kuwa uwezo wa mwanadamu maishani husababishwa sana na msukumo wa ndani, lakini katika maisha ya mtoto uwezo wake hutengenezwa kutokana na msukumo wa nje kwani anapokuwa mdogo ni kipindi cha ubongo wake kukuwa na kupewa chakula cha nje ili kujenga uwezo wake  wa ndani.   
Kutokana na hayo mazingira na mambo anayotendewa akiwa mtoto yanaweza kumtengeneza kuwa vyovyote.
Tunaishi katika jamii isiyotambua msukumo huu, jamii isiyosikiliza sauti ya mtoto, jamii isiyo na usalama katika maisha ya mtoto kutokana na uonevu ama unyanyasaji kwa mtoto pasipokujitambua. Na wengi wetu hatuna uelewa kuhusu msukumo wa nje hasa uonevu unavyoweza kubadili hatima ya maisha ya mtoto. Watoto wanayo haki ya maisha ya utoto yasio na uonevu ili kutengeneza uwezo wa ndani ya wao kuyamudu maisha ya dunia hii ambayo kwao ni mpya.
 Labda inatupasa tujue nini maana ya uonevu kwa mtoto?
tembelea hapa kwa habari zaidi
www.treasurewithinyou.blogspot.com
 http://treasurehousewithinyou.blogspot.com/2012/04/madhara-ya-uonevu-kwa-watotochild.html

Categories:

Leave a Reply