Mikopo ni nyenzo ya uwekezaji kwa jamii ili kujikwamua kiuchumi katika kuendesha maisha .serikali na mashirika mbalimbali yamekuwa yakitoa mikopo kwa masharti nafuu kwa vijana ili waweze kuanzisha au kuendeleza biashara au miradi kama vile kilimo,ufugaji, uvuvi ujenzi na hata kutoa huduma ya simu na kadhalika,hii yote ni kujaribu kujiweka sawa kimaisha.
HUKO VIJIJINI KUKOJE?
Mkopo sio mpaka benki,hata kwa ndugu na marafiki zetu huwa tunakopa, kwa makubaliano maalum,unapovunja uaminifu wa kurejesha unaharibu nafasi ya kupata tena mkopo.vivyo hvyo mashirika na benki ndivyo wanavyofanya.
Unapopewa mkopo kwa sharti kurudisha kwa wakati ili upate mwingine na hata mtu mwingine pia apate fursa ya kukopa.hapo utakuwa umeula.
Huduma hii ya mikopo mara nyingi ilikuwa ikifanyika mijini lakini sasa baadhi ya mashirika yamefika hata vijijini na kutoa hela kwa jamii.
Kuna wateja wa huduma hiyo wengine hawafuati utaratibu uliowekwa wa kurudisha mkopo na kuwafanya watoa mikopo kutofurahishwa na kitendo hicho.
HIZI NI BAADHI YA FAIDA ZA MIKOPO.
.kuongeza mitaji itakayoendeleza mradi wako.
.itakuwezesha kununua vifaa vya kufanyia kazi.
Kugharamia shughuli za uendeshaji wa mradi au biashara

Categories:

Leave a Reply