Nakushukuru Mungu muumba mbingu na dunia,kwa mambo mengi unayoendelea kunitendea mimi na ndugu yangu mdau.eeh Mungu narudisha sifa na utukufu.
Ndugu mdau leo nitataka nieleze kwa kifupi kuhusu hili la kukopesha wewe ukiwa kama mjasiri amali.
Ndugu mdau kukopesha kunaweza kuwa na faida au hasara,kwani kwa utafiti wangu nilioufanya kwa wajasiri amali kukopesha kunaleta madhara makubwa sana,kwani unakuwa unapoteza wateja,unapomkopesha mtu ni sawa na umemwambia asije tena kwenye biashara yako,unamwambia apunguze trip za kuja kwenye biashara yako,kwani huwa anabadilisha hata njia.kwahyo ndugu wajasiri amali uwe mwangalifu kuhusu ili suala la kukopesha,angalia usikopeshe kwa hasara,kwani kukopesha angalia mtu unayemkopesha kwani kukopesha inaweza kuwa fimbo ya kukuchapa wewe mwenyewe kwa sababu unampa mtu ambaye atakurudishia.

Categories:

Leave a Reply