Ivo Manuel Lemus a.k.a Cabo Snoop kutoka Angola akiwa na miaka 20 tu kwa sasa ameonekana kuiteka Afrika na nyimbo zake mbili za ''prakatatumba'' pamoja na ''windhek''. Jamaa ana jumla ya kaka 12 na anaishi Luanda Angola. Ukifika kwao unatakiwa umuite ''No Body"",hii inatokana na Mama yake kupoteza ndugu zake watatu na hivyo kila mtu alikuwa akifikiri naye angekufa. Nobody anamaanisha kufa au kuishi kwa sababu alikuwa akifikiri muda wowote angekufa au kuendelea kuishi baada ya vifo vya ndugu zake watatu.
Jamaa kabla ya kufikia hapa alipo alipata kuwa mmoja wa waanzilishi wa kikundi cha kudansi cha Crazy Boys.
Na anakumbuka siku moja alipigiwa simu na rafiki yake akimualika kujiunga na kampuni ya kutengeneza muziki na video ya Power House inayomilikiwa na Dr. Fu Hochi. Jamaa alikubali kujiunga na kampuni hiyo
Jamaa alipewa jina la Cabo ikiwa inamaanisha Captain na Snoop kwa sababu ni mwembamba na mrefu.
''Windek'' ndio wimbo ambao ulimtambulisha kwa kiasi kikubwa na ametoa albamu yake inayoitwa
"Bluetooth" na ana DVD inayokwenda kwa jina la "E-mail". Cabo Snoop amepata kufanya collaboration na msanii kutoka USA Fat Joe ya remix ya wimbo wa 'windek'.

Categories:

Leave a Reply