Biashara inatunzwa na Mfanyabiashara na kuzalisha mapato. Katika mapato hayo mfanyabiashara anajilipa mshahara kutokana na kupata faida. Mshahara anao jilipa ndio unatumika kwa matumizi binafsi ikiwemo kutunza familia. Katika hili ni vyema fedha ya Biashara na ya familia itengwe ili kuepuka mwingiliano wa matumizi. ilibiashara iweze kukua vizuri ni lazima mfanyabiashara aelewe namna ya kutenga fedha ya biashara na ya familia


KUTENGANISHA BIASHARA NA FAMILIA


Biashara ina nafasi kisheria kama binadamu, na inalindwa na sheria na ndiyo maana inapewa jina na kusajiliwa. Kwa kuwa biashara na mwenye biashara ni vitu viwili tofauti na matumizi yao ni tofauti pia. Kwa hiyo fedha ya biashara ni ya biashara na ya familia ni ya familia, vitu hivi viwili havichanganywi.

NJIA ZAKUBADILISHA FAMILIA IWEZE KUISAIDIA BIASHARA KUIMARIKA NA KUKUA

1. Elimisha familia yako maana na umuhimu wa biashara yako katika kuendeleza familia hiyo.Biashara ndiyo inayo itunza familia . Ili biashara iweze kuitunza familia nilazima itunzwe vizuri. Mfano Jinsi ng'ombe anavyo tunzwa vizuri ndivyo anavyotoa maziwa mengi. Yale maziwa yanauzwa na kulipa ada za shule na kadhalika.

2. Wape elimu yabiashara ili wakusaidie kusimamia biashara yako

3 Usiajiri wanafamilia ambao si waaminifu

4. Washirikishe wana familia katika kuzalisha na si katika matumizi tu

5. Kuwa muwazi namkweli kwa familia yako kuhusu kipato halali kinachopatikana kwenye biasharayako


ATHARI ZAKUENDEKEZA UNDUGU, UJIRANI, URAFIKI KATIKA BIASHARA

1 Uzoefu unaonyesha kwamba ndugu na marafiki wakikopa hawarudishi, Na wakijua kuwa weweni rahisi kutoa misaada basi kuomba hakuishi na matokeo yake ni.

- K
ujenga uadui wakati unapo kuwa huwezikuwasaidia

- Kudhoofisha biasharayako kwa kutoa misaada mingi sana

- Kuathiri maendeleo yafamilia yako

- Kushindwa kulipamikopo uliyo chukua

- Kufilisika

NJIA ZAKUELIMISHA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI

1.Waelimishe wasaidie biashara yako kukua vizuri badala ya kuiharibu

2. Unaweza kuwaelimisha kwa kuongea nao wewe mwenyewe ana kwa ana

3. Unaweza tumia mtaalaau mtu mwingine atakaye weza kuwaelimisha vizuri
source:komandoo jf

Categories:

Leave a Reply